Thursday, May 30, 2013
Tuesday, May 14, 2013
NINI HUKMU YA KUWA NA RAFIKI WA KIKE/KIUME(BOYFRIEND & GIRLFRIEND)
BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIIM
Assalam
alaykum!!!
Utangulizi
Kila sifa njema anastahiki kushukuriwa
Allah(s.w),Rehma na amani zimuendee kiongozi wa ummah huu Mtume Muhammad(s.a.w)
na juu ya aali zake na maswahaba zake wote(r.a
Napenda kuchukua fursa hii katika kuielimisha na
kuikumbusha jamii juu ya suala hili ambalo sasa limechukuliwa kama jambo la
kawaida katika jamii zetu na hali sio kutokana na mafunzo ya dini yetu.
UMUHIMU WA UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA UISLAMU
BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIIM
Utangulizi
Kila
sifa njema anastahiki kushukuriwa Allah(s.w),Rehma na amani zimuendee kiongozi
wa ummah huu Mtume Muhammad(s.a.w) na juu ya aali zake na maswahaba zake
wote(r.a
Napenda kuchukua fursa hii tukufu ili
niweze kuufikisha ujumbe huu kwa waislam juu ya Umuhimu wa kuwa na umoja na
mshikamano baina yetu.Suala la umoja na mshikamano baina ya waislamu ni jambo
ambalo Allah( s.w) analisisitiza sana katika kitabu chake kitakatifu.Hivyo basi
umoja baina ya waislamu ni jambo la LAZIMA.Ukiangalia katika ibada zote
alizotuwekea Allah(s.w) zinahimiza suala la kuwa na umoja na mshikamano baina
yetu waislamu.Angalia tu katika nguzo za uislamu jinsi Allah alivyoziweka na
zinavyohimiza umoja baina yetu ni wazi kuwa suala la umoja na mshkamano ni
muhimu sana katika uislamu.Ibada ya Swala, Funga , Zakat, Hijjah n.k, hizi zote
zina himiza umoja na mshikamano baina yetu. Katika kusisitiz suala hilo Allah
anasema katika sura ya 49:10
“Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya
ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe. “