BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIIM
Utangulizi
Kila
sifa njema anastahiki kushukuriwa Allah(s.w),Rehma na amani zimuendee kiongozi
wa ummah huu Mtume Muhammad(s.a.w) na juu ya aali zake na maswahaba zake
wote(r.a
Napenda kuchukua fursa hii tukufu ili
niweze kuufikisha ujumbe huu kwa waislam juu ya Umuhimu wa kuwa na umoja na
mshikamano baina yetu.Suala la umoja na mshikamano baina ya waislamu ni jambo
ambalo Allah( s.w) analisisitiza sana katika kitabu chake kitakatifu.Hivyo basi
umoja baina ya waislamu ni jambo la LAZIMA.Ukiangalia katika ibada zote
alizotuwekea Allah(s.w) zinahimiza suala la kuwa na umoja na mshikamano baina
yetu waislamu.Angalia tu katika nguzo za uislamu jinsi Allah alivyoziweka na
zinavyohimiza umoja baina yetu ni wazi kuwa suala la umoja na mshkamano ni
muhimu sana katika uislamu.Ibada ya Swala, Funga , Zakat, Hijjah n.k, hizi zote
zina himiza umoja na mshikamano baina yetu. Katika kusisitiz suala hilo Allah
anasema katika sura ya 49:10
“Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya
ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe. “
Katika aya hii tunajifunza kuwa waislamu
wote ni nduga, pale linapotokea tatizo basi hapana budi watu wapatane ili
tuweze kujenga umoja utakao kuwa madhubuti baina yetu.Lakin leo ni tofauti
waislam wao kwa wao ndio hugombana, hitiliana fitna, majungu n.k hii ni
kuonyesha leo hakuna umoja na mshikamano uliopo baina yetu.
Kaika maubile ya wanaadamu suala la
ikhtilafu ni la kawaida.Allah ametuumba tofauti tfauti wapo wanene,
wembamba,warefu, wafupi, weupe, weusi , hizi ni tofauti.Kuzuia ikhitilafu
hutoweza kwa sababu ndio maumbile ya
mwanaadamu,asichotaka Allah ni FARQA.
FARQA baina ya waislam in jambo ambalo
Allah alikemea na halipendi anachotaka yeye ni umoja (I’TISWAM) na mshikamano baina yetu.Anasema katika
Qur-an sura 3:103-105
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote
pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu:
vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa
neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni
nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate
kuongoka”.Anaendela nakusema
.”Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania
kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa”.Anaendelea
nakusema
.”Wala msiwe kama wale walio farikiana na
kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na
adhabu kubwa. “.
Hizi ni aya ambazo Allah anasisitiza
waislam tuwe na umoja na mshikano na yeye hapendi kufarikiana katika masiala ya
dini na ndio maana yeye anatuambia pale tunapo ikhtilafiana katika masuala ya
dini tufanye yafuatayo.Qur-qn 4:59
‘Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini
Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi
lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na
Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.”
Hivi ndivyo Allah anavyo tufundisha
tufanye pale tu tunapo ikhtalifiana katika masuala ya dini yetu nayo ni
kuirejea QUR-AN na SUNNAH hiyo ndiyo suluhisho litakalopelkea kupatana
kwetu.Sasa basi kwa nini mpaka leo waislamu wamefarakana?.Jibu ni kwamba
waislamu tumeacha kuifuata QUR-AN na SUNNAH na ndio maana leo tupo kwenye hali
hii.
Hivyo basi Allah anatutaka tuifuate
QUR-AN na SUNNAH kwani ndio vitu viakavyo tuletea umoja wa kweli na mshikamano
baina yetu waislamu.Allah katika Qur-an anatuelelea kwamba yeye anawapenda watu
walioshikamana katika dini yake.Anasema katika sura ya 61:4
“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana
katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana”
Allah anaupigia mfano umoja na JENGO
jinsi (material) yaliyo tumika kulitengeneza jingo yalivyo shikamana,.Kama
hivyo ndivyo mtume (s.w) anasisitiza katika hadithi ifuatayo:
Imepokelewa hadithi kutoka kwa Nu’uman
bin Bashiir (r.a).Mtume anasema”Waumini ni sawa kama macho yanauma (yana
matatizo)mwili mzima unaumwa (una matatizo) kama kichwa chake kinauma basi
wmili mzima unauma”(Muslim)
Ndugu zangu katika imani hivi bado
hujaelewa tu jinsi suala la umoja na umoja na mshikamano lilivyo kuwa muhimu
katika uislamu.
Mafunzo
tunayoyapata kutokana na aya hizi na hadithi hii ya mtume(s.w)
1.
Umoja ni jambo la
lazima
2.
Atakaye vunja umoja
amekeuka amri ya Allah
3.
Kpendana baina yetu
4.
Umoja na mshikmano ndio
ngao kwa waislam.
Allah anatukataza katika Qur-an kuwa na
makundi makundi makundi katika dini yetu kwani kila kikundi kitasifia upande
wake na FARQA itatokea.Allah ansema
katika sura ya 30:31-33
“ Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na
shikeni Sala, na wala msiwe katika washirikina”.Anaendelea
“. Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao,
na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho”Anaendelea
“ Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi
nao wametubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi
miongoni mwao humshirikisha Mola wao Mlezi,”
Ili tuwe na umoja na mshikano kama
alivyokuwa mtume na maswahaba zake uliopelekea kuwashinda maadui wa zama zao,
Allan anasema sura ya 48:29
“Muhammad ni
Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na
wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na
radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu.
Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio
toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya
ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri.
Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na
ujira mkubwa.’
ni lazima umoja huo upitie upitie hatua TATU:
1. Tuwe
na lengo moja.(9:33, 61:9, 48:28)
2. Kufanyiana
wema baina yetu(hadithi ya mtume)
3. Kutofanyiana
mabaya
·
Dhulma
·
Kusengenyana
·
Kuchukiana
·
Kuvunjiana heshma
Sababu za kutokuwa na umoja na mshikamano
1. Hatuna
lengo moja
2. Ufahamu
wetu juu ya dini tofauti
3. Ufahamu
wetu juu ya qQur-an ni tafauti
4. Ufahamu
wetu juu ya sunnah ni tofauti
Hitimisho:Hivyo
basi waislamu ni lazima tushkamane na tuwe na umoja wa kweli baina yetu ili
tuzishinde kaumu za makafiri
Imeandaliwa na
Abuu
Nashfaty,Hassan Aufi Kidege
1st year student in
Barchelor of Arts in Sociology and Social work.
Contacts; 0719020847/0787101413/0764002024
Email:aufihassan@ymail.com/aufihassan@yahoo.com
WABILLAH TAWFIQ
0 comments:
Post a Comment