Tuesday, May 14, 2013

NINI HUKMU YA KUWA NA RAFIKI WA KIKE/KIUME(BOYFRIEND & GIRLFRIEND)



BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIIM

Assalam alaykum!!!
Utangulizi
 Kila sifa njema anastahiki kushukuriwa Allah(s.w),Rehma na amani zimuendee kiongozi wa ummah huu Mtume Muhammad(s.a.w) na juu ya aali zake na maswahaba zake wote(r.a
 Napenda kuchukua fursa hii katika kuielimisha na kuikumbusha jamii juu ya suala hili ambalo sasa limechukuliwa kama jambo la kawaida katika jamii zetu na hali sio kutokana na mafunzo ya dini yetu.

Waislam wa leo wanawaiga mayahudi na manaswara juu ya suala la kuwa na uchumba kabla ya ndoa(bond) kitu ambacho kinawapelekea watu kufanya zinaa na kuzaa watoto wa zinaa(nje ya ndoa).Hivyo basi kuwa na uhisiano wa kimapenzi kabla ya ndoa ni kuwaiga mayahudi na manaswara na pia ni kuikurubia zinaa,kitu wanachokitaka mayahudi na manaswara ni ni sisi kufuata mila zao na hapo wamefaulu,sasa basi kila mmoja aiulize nafsi yake je,amewaiga au la?Allah anasema”Hawatokuwa radhi juu yako mayahudi na manaswara mpaka ufuate mila(dini) yao”
Aya na dalili za kukataza jambo hili zipo nyingi zikiwa zinazoashiria makatazo moja kwa moja na nyenginezo zenye uhusiano na makatazo haya.Kuwa na (boyfriend ) bila shaka kutasababisha yatendeke maasi baina ya mwanamke na mwanaume kwani shetani huwa pamoja nao akiwachochea kuingia katika kumuasi mola wao.
Kutoka kwa Umar(r.a)kutoka kwa Mtume(s.a.w) amesema”Hachanganyiki mwanaume na mwanamke ila shetani huwa ni watatu wao”(At-Tirmidhy)
Ndio maana Mtume(s.a.w) ameonya kukaa faragha mwanamke na mwanamume.Mtume(s.a.w) amesema(”Hawi faragha mmoja wenu pamoja na mwanamke ila awepo mahram wake”.(Al-bukhary na Muslim)
Matokeo yake ni shetani kuwafikisha kuingia katika maasia ya zinaa na ndio maana sheria ya kiislam haikuruhusu jambo hilo au kufunga  uchumba inavyojulikana(Engagement).Bali inatakiwa kufunga ndoa moja kwa moja baada ya kuwafikiana pande zote mbili.Sio hivyo tu mtume(s.a.w) anaendelea kusema juu ya huku kukaa faragha,”Hakai faragha mwanamke na mwanaume ambao wanaweza kuoana ispokuwa watatamaniana”(Bukhary& Muslim).Hivyo muislam vipi mtakaa faragha pasi na ruhusa ya kisheria?kitu ambacho kitawapelekea kuingia katika maaswia ya KUSHIKANASHIKANA na wakati mtume anasema,”Kukitwa kwa mmoja wenu kwenye kichwa chake kwa shazia ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke ambaye siyo halali kwake”
(Bukhary&Muslim)Hivyo ndugu yangu muislam kila mmoja anaijua nafsi yake kama Allah(s.w) anavyosema katika surul Qiyama”Bali mwanaadam juu ya nafsi yake ni mjuzi mno”
Anasema Allah(s.w)”Wanawake wema miongoni mwa waumini na wanawake wema miongoni mwa waliopewa kitabu kabla yenu.mtakapo wapa mahari yao,mkafunga nao ndoa,bila ya kufanya uasharati (jimai)wala kuwaweka kinyumba.Na anaye kataa kuamini bila shaka amali yake imepotea,naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara”(2:120)

Msichana wa kiislam anapokabiliwa na .mvulana kutaka kufanya urafiki ajiepushe kabisa bali amshauri kwanza awasiliane na wazazi wako na baada ya kumjua kuwa ni mtu  mwenye DINI na TABIA nzuri basi wazazi wasichelewe kukuozesha nawe uridhike kwani hivyo ndivyo ipasavyo na tulivyopewa mafunzo na Mtume(s.a.w)”Atakapo posa kwenu Yule mtakaeridhika na dini yake,na tabia yake basi muozeni kwani kutofanya hivyo itapatikana fitna katika ardhi na ufisadi mkubwa”(Tirmidhy).
Hivyo muislam BADILIKA kuwa muislamu wa kweli unaye fuata maamrisho na kuacha makatazo ya Allah(s.w) na Mtume wake(s.a.w).Allah said”Verily Allah will never change the condition of the people until change themselves”(13:11)

                                                       Imeandaliwa na
                                    Abuu Nashfaty,Hassan Aufi Kidege       
                1st year student in Barchelor of Arts in Sociology and Social work.
                            Contacts; 0719020847/0787101413/0764002024
                        Email:aufihassan@ymail.com/aufihassan@yahoo.com
                                                 WABILLAH TAWFIQ



                                                    
           









9









0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer