Wednesday, December 21, 2016

MWANAFUNZI WA KIKE WA KIISLAMU AGOMA KUMPA MKONO RAIS WA UJERUMANI.

Mwanafunzi wa kike wa kiislamu mwenye asili ya Syria wa shule ya Theodor Heuss nchini Ujerumani amekataa kusalimiana kwa kumpa Rais wa nchi hiyo pale alipozuru katika shule yao.



Tukio hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi uliopita pale Rais Joachim Gauck alipotembelea mji wa Offenbach na shule hiyo inayounganisha wahamiaji na jamii ya kijerumani.

Rais Joachim alitembelea shule ya Theodor Heuss kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuwasaidia na kusomesha watoto wa wahamiaji lugha ya kijerumani na tamaduni za nchi hiyo.


Kamera za TV zilichukua tukio hilo pale Rais alipoanza kuwasalimia wanafunzi waliojipanga kumpokea ndipo alipofika kwa binti huyo aliyevaa Baibui na hijabu. Jina la binti huyo halikuweza kupatikana mara moja.

Alipojaribu kutoa mkono kumsalimia, binti huyo hakutoa mkono wake bali aliweka mkono wake kifuani na kutingisha kichwa chake kama ishara ya kumsalimu rais huyo badala ya kumpa mkono.


Kimsingi binti huyo hakumvunjia heshima Rais wa Ujerumani bali alitekeleza mafundisho ya Kiislamu ambayo yanaharamisha mwanamke Mwislamu kumpa mkono mwanaume ajnabi kama ambavyo mwanaume Mwislamu haruhusiwi kumpa mkono mwanamke ajnabi.

Hali hiyo ikamfanya Rais kuendelea na mwanafunzi mwingine.

Katika mafundisho ya dini ya kiislamu hairuhusiwi kushikana

mkono mwanamke na mwanaume ambao hawajaoana.

Tukio hilo limeibua maoni ya watu wengi nchini Ujerumani ambapo Mwanasaikolojia Annette Trebel amezitaka mamlaka zinazohusika kujifunza tamaduni zingine kutoka kwa wahamiaji badala ya wahamiaji kujifunza tamaduni za kijerumani.

Aidha wengi walitoa wito kwa wajerumani kujifunza kiarabu ili kusaidia wahamiaji ambao hawataki kujifunza kijerumani. Pia kuweka ishara za lugha ya kiarabu ili kusaidia wahamiaji wanaowasili nchini humo.

Powered by Blog - Designer