SEHEMU
YA I: UHUSIANO WA SERIKALI, DINI NA MASHIRIKA YA KIDINI
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
1
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui kuwepo
kwa Mwenyezi Mungu na uhalali wa mamlaka ya Mwenyezi Mungu
|
Katiba mpya itambuwe kuwepo kwa
Mwenyezi Mungu na Mamlaka yake juu ya Wanaadamu (kwa mnasaba huu, wananchi wa
Tanzania
|
2
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui uhalali
wa Sheria za Mwenyezi Mungu. Hii inajidhihirisha kwa kauli ya serikali
kutokuwa na dini.
|
Katiba mpya iweke wazi kutambua kwake
uhalali wa sheria za Mwenyezi Mungu na kuziheshimu. Maana ya serikali
kutokuwa na dini iainishwe na kuwekwa wazi kikatiba.
|
Kwamba Katiba iliyopo inamlazimisha mtu
kufuata sheria zote hata kama zinakwenda kinyume na imani ya dini ya raia
husika.
|
Katiba mpya isimlazimishe mtu kufuata
taratibu au sheria ambazo inakwenda kinyume na imani yake na hivyo kupelekea
kuvunja sheria za dini yake.
|
|
4
|
Kwamba Katiba iliyopo haitoi
tafsiri yakinifu juu ya maana ya ibada na dini. Tafsiri sahihi ya maneno dini
na ibada ni muhimu ili kuzuia bughudha kwa wananchi wanapokuwa katika matendo
ya dini na ibada.
|
Katiba itoe tafsiri yakinifu ya ibada
na dini kwa mujibu wa tafsiri ya dini husika.
|
5
|
Kwamba Katiba iliyopo inatenganisha
mamlaka ya nchi na mamlaka ya dini. Huu ni mfumo Kristo.
|
Katiba mpya iruhusu kuchanganya mamlaka
ya nchi na ya dini. Mfano uwepo wa Mahakama ya Kadhi itakayoendeshwa kwa
hazina ya serikali.
|
6
|
Kwamba Katiba iliyopo imetoa tafsiri
potofu ya neno HALALI. Kwa mfano neno rizki halali linajumuisha mathalani
hata rizki ipatikanayo kwa kuuza pombe na kucheza bahati nasibu ni halali.
|
Katiba mpya itoe tafsiri sahihi ya neno
HALALI kwa mujibu wa imani ya dini na tafsiri hiyo iwe ni yenye kukubalika
kiutendaji na katika mahusiano baina ya mwananchi wa dini husika na wananchi
wengine nje ya dini husika.
|
7
|
Kwamba Katiba iliyopo haiilazimishi
serikali kuitambua siku ya Ijumaa kama siku rasmi ya ibada kwa Waislamu. Hii
inasababisha usumbufu mkubwa kwa Waislamu kutekeleza ibada hii hususan
wafanyakazi na wanafunzi.
|
Katiba mpya itambue na kuipa heshima
siku ya Ijumaa kuwa ni siku maalum ya ibada kwa Waislamu. Hivyo shughuli zote
za serikali zisimamishwe wakati wa kutekelezwa ibada hiyo.
|
8
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui kuwepo
kwa Mahakama ya Kadhi. Hii imepelekea Waislamu kutohukumiana kwa sheria za
Kiislamu ambayo ni sehemu ya ibada kwao na vile vile kukosekana kwa msimamizi
wa haki inapotea mzozo baina ya Waislamu.
|
Katiba mpya iruhusu na itambue uwepo wa
mahakama za kadhi zitazoendeshwa chini ya usimamizi wa Kadhi Mkuu na Naibu
Kadhi Mkuu wataokao chaguliwa na Waislamu kwa kuzingatia sifa za kielimu
katika fani ya sheria ya Kiislamu na kutambuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano.
|
9
|
Kwamba Kutokana na Katiba iliyopo
kutokutambua mahakama ya kadhi ajira rasmi za makadhi hazipo.
|
Katiba mpya itambue uwepo wa tume ya
ushauri wa uteuzi wa makadhi na ajira ya makadhi kwa mahakama za kadhi
Tanzania ambayo kikatiba itaitwa Tume ya Utumishi ya Mahakama ya Kadhi.
Tume hii itachaguliwa na Waislamu. Wajumbe wa Tume hiyo watakuwa wafuatao:
1. Kadhi Mkuu ambaye atakuwa mwenyekiti
kutoka bara au visiwani;
2. Naibu Kadhi Mkuu ambaye atakuwa
naibu Mwenyekiti kutoka bara au Visiwani;
3. Kadhi mmoja wa Mahakama ya Kadhi ya
Rufaa atakayechaguliwa na Waislamu;
4. Wajumbe watatu kutoka mahakama ya
kadhi.
|
10
|
Kwamba suala la kugharimia uendeshaji
wa mahakama za kadhi linapaswa liwe jukumu la serikali kupitia mfuko wa hazina
ya serikali. Hii kwa sababu Waislamu ni sehemu ya walipa kodi. Kama walivyo raia
wengine, wanastahili kufaidika kutokana na kodi wanazolipa.
|
Katiba mpya iilazimishe serikali
kugharimia gharama za kuendesha mahakama za kadhi na gharama za watumishi wote
kutoka kwenye mfuko wa hazina ya serikali.
|
11
|
Kwamba Mahakama ya Kadhi haipaswi
kuingiliwa na mahakama ya aina yoyote isiyohukumu kwa sheria ya Kiislamu.
Kwamba upo umuhimu wa kuunda kwa Mahakama ya Rufaa ili kusikiliza kesi za
rufaa kutoka kwenye mahakama ya kadhi.
|
Katiba mpya itambuwe uwepo wa Mahakama
ya Rufaa ya Kiislamu.
|
12
|
Kwamba Waislamu kwa sheria zilizopo
wanakwazika katika kutekeleza dini yao kikamilifu. Inawawia vigumu kutekeleza
sheria kwa mnasaba wa dini yao. Kufuata sheria za Kiislamu ni sehemu ya dini
na ibada ya lazima kwa Muislamu, haki ambayo katiba iliyopo imetoa uhuru.
|
Katiba mpya itambue haki ya Waislamu
kutekeleza nakufuata sheria ya Kiislamu katika ukamilifu wake. Katika sehemu
zenye Waislamu wengi sheria ya Kiislamu ifuatwe katika ukamilifu wake. Kila
Muislamu katika maeneo haya atalazimika kuhukumiwa kwa sheria za Kiislamu.
Katika maeneo yenye Waislamu wachache mahakama za kadhi ziwahukumu Waislamu
katika sheria zote za Kiislamu isipokuwa za jinai.
|
13
|
Kwamba Katiba iliyopo haitoi muongozo
juu ya ushirikiano baina ya serikali na dini au madhehebu ya dini, hali
iliyopelekea kuwepo kwa malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo maalum
unaoneemesha Ukristo (hususan Ukatoliki) hususan katika sekta ya elimu na
afya kwa kutumia hazina ya taifa. Mathalani kwa kupitia mkataba wa ufahamiano
[MoU] baina ya serikali na kanisa serikali hutenga mamilioni ya fedha za umma
kila mwaka kunufaisha mipango ya afya na elimu ya kanisa.
|
Katiba mpya iweke uthibiti wa matumizi
ya fedha za umma kwa utaratibu wa upendeleo wa madhehebu ya dini yoyote ama
kinyemela au kwa njia ya urasimishaji kupitia mikataba au makubaliano.
|
SEHEMU
YA II: MASUALA YA MUUNGANO NA SERIKALI YA MUUNGANO
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
14
|
Kwamba Katiba iliyopo inatambua uwepo
wa serikali mbili katika Jamhuri ya Muungano, jambo ambalo limesababisha
utata na kero kubwa ya muungano hususan kwa upande wa serikali ya Zanzibar.
Yapo malalamiko kwa upande wa Zanzibar kuwa wameporwa madaraka ya kiinchi
(sovereignity) na serikali ya muungano. Hii imepelekea mpaka baadhi yao kudai
muungano uvunjwe.
|
Katiba mpya itambue uhalali wa serikali
tatu: Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano.
|
15
|
Kwamba Katiba iliyopo inaainisha tu
maeneo ya muungano ambao chimbuko lake ni makubaliano baina ya viongozi wa
iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar bila ridhaa ya wananchi wa pande mbili hizi.
Hali hii imepelekea malalamiko kwamba wananchi hawakuhusishwa.
|
Katiba mpya iweke utaratibu utaofanya
masuala yatakayokubalika kuwa ya muungano yapitishwe kwa kura ya maoni
(referandum) kwa kuzingatia uwiano wa sehemu hizi za muungano. Kila upande
ukubali masuala hayo kwa asilimia 75 au zaidi ya wananchi wake ndipo
yaingizwe katika orodha ya maeneo ya Muungano
|
16
|
Kwamba Katiba iliyopo iko kimya juu ya
mgawo wa madaraka ya rais na naibu rais, mawaziri, manaibu waziri kutoka
pande mbili za muungano. Hii imepelekea Wazanzibari kulalamika kwamba huenda
muda mrefu rais wa jamhuri ya muungano akatoka bara tu.
|
Katiba mpya iweke utaratibu utakaowezesha
cheo cha rais wa jamhuri ya muungano kiwe cha kupokezana baina ya pande mbili
za muungano yaani Tanganyika na Zanzibar. Vyeo vya mawaziri na manaibu
mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na makatibu wakuu wasaidizi katika
serikali ya muungano vitolewe kwa uwiano uliosawa. Mathalani waziri akiwa
mtanganyika naibu wake awe mzanzibari.
|
17
|
Kwamba Katiba iliyopo haikuweka wazi
mgao wa maliasili baina ya pande mbili za muungano. Hii imepelekea kuwe na
mvutano kwamba iwapo mafuta yatapatikana yawe ni ya muungano au la.
|
Katiba mpya iweke wazi kwamba mali ya
asili kama vile madini, gesi na mafuta n.k. havitakuwa katika masuala ya
muungano. Kila upande mmoja wa muungano uwe unamiliki mali ya asili yake.
|
18
|
Kwamba Katiba iliyopo iko kimya kuhusu
mahusiano ya serikali ya Zanzibar katika medani za kimataifa kwa maeneo
yasiyo ya muungano. Hii imepelekea kuwepo kwa malalamiko upande wa Zanzibari
kuwa hawanufaiki na wanabanwa kuwa na mahusiano na nchi na taasisi nyingine
za kimataifa, mathalani kujiunga na OIC ambayo ingesaidia utekelezaji miradi
ya mambo yasiyokuwa ya muungano.
|
Katiba mpya iweke utaratibu za
kuziwezesha pande zote mbili za muungano (Tanganyika na Zanzibar) kuwa na
mahusiano na mashirikiano na serikali za nje na taasisi za kimataifa bila
pingamizi kutoka kwenye serikali ya muungano.
|
19
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui kuwepo
kwa Mahakama Kuu ya Katiba. Hii imepelekea kukosekana kwa suluhusho la utata
unapojitokeza wa masuala mbali mbali ya muungano na mengineyo. Mathalani,
utata wa Zanzibar kama nchi kamili au vinginevyo unashindwa kupewa ufumbuzi
wa kisheria.
|
Katiba mpya itambue uwepo wa Mahakama
Kuu ya Katiba ambayo itakuwa na uwezo na nguvu za Kisheria za kutafsiri
vipengere mbalimbali vya Katiba vyenye utata na pia kubatilisha sheria yoyote
itakayotungwa ambayo inapingana na Katiba.
|
20
|
Kwamba Katiba haitambui kuwepo kwa
Mahakama Kuu ya Rufaa ya Katiba ambayo itahusika na kesi za rufaa kutoka
Mahakama Kuu ya Katiba.
|
Katiba mpya itambue uwepo wa Mahakama
Kuu ya Rufaa ya Katiba.
|
21
|
Kwamba Katiba iliyopo iko kimya juu ya
nafasi ya Spika na Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Tangu kuasisiwa kwa muungano nafasi hizo zimekuwa zikihodhiwa na
watanganyika. Hii imepelekea kuwa ni moja ya kero kubwa za muungano.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa
kupokezana nafasi ya spika na naibu spika baina ya sehemu mbili za muungano.
Yaani spika akiwa mtanganyika naibu wake awe mzanzibari. Nafasi hizo
zibadilishwe kila baada ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.
|
22
|
Kwamba Katiba iliyopo inamtambua Rais,
Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kama viongozi wa juu wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania. Waziri mkuu kwa utaratibu wa sasa hana shughuli na mamlaka yakinifu
upande wa Zanzibar. Cheo hiki si muafaka kwa hivyo kisiwe katika muungano.
|
Katiba mpya itambue kuwepo kwa mawaziri
wakuu kwa kila upande wa muungano kama wakuu wa shughuli za serikali zao.
Kisiwepo cheo cha waziri mkuu wa serikali ya muungano. Shughuli zake zifanywe
na makamu wa rais wa serikali ya muungano, ambaye ndiye msaidizi mkuu wa rais
katika serikali ya muungano
|
23
|
Kwamba Katiba iliyopo iko kimya juu ya
uwezekano wa kuvunjika muungano.
|
Katiba iweke utaratibu wa kuvunjika kwa
muungano iwapo itatokea dharura ya jambo hilo na ianishe sababu zinazoweza
kupelekea kuvunjika kwa muungano.
|
24
|
Kwamba Katiba iliyopo hairuhusu chama
cha siasa chenye lengo la kuvunja muungano na chenye lengo la kutumia nguvu
au mapambano kufikia malengo ya siasa.
|
Katika kudumisha uhuru wa maoni chama
chochote hata kama kina malengo ya kuvunjwa muungano kiandikishwe endapo
kinaona kuna maslahi kwa wananchi juu ya hilo na kwamba kuvunjika kwa
muungano ndiyo njia iliyobaki ya kuondoa dhuluma. Chama kiruhusiwe kutumia
nguvu kufikia malengo ya kisiasa endapo njia ya amani na mazungumzo
imeshindikana kuondoa dhuluma.
|
25
|
Kwamba Katiba iliyopo hairuhusu
kusajili chama cha siasa chenye wafuasi katika upande mmoja tu wa muungano au
kuendesha shughuli zake katika upande mmoja tu wa muungano.
|
Katiba mpya iruhusu kuwepo kwa chama
cha namna hiyo. Hii itatoa uhuru kamili kwa raia wa pande mbili hizi kutoa
maoni na kutetea maslahi na maendeleo yao hata kama ni wachache [bila kujali
idadi yao]
|
SEHEMU
YA III: HADHI NA MADARAKA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
26
|
Kwamba Katiba iliyopo inampa rais hadhi
na mamlaka makubwa kiasi cha kuwa juu ya sheria (asiyeweza kushitakiwa) kwa
kosa la aina yoyote akiwepo madarakani au hata akiwa nje ya madaraka
|
Katiba mpya iruhusu rais kufunguliwa
mashtaka kwa kosa lolote akiwa ndani au nje ya madaraka. Hii itasaidia katika
uwajibikaji wa rais na kuzuia ufisadi na ubadhirifu wa mali za wananchi kwa
kutumia madaraka aliyopewa na wananchi.
|
27
|
Kwamba Katiba iliyopo imempa mamlaka
Rais kutoa misamaha kwa watenda kosa lolote.
|
Katiba mpya isimpe Rais madaraka ya
kutoa msamaha kwa kuwa hili linapelekea kuingilia maamuzi ya mahakama.
|
28
|
Kwamba Serikali haizingatii uwiano wa
kidini katika uteuzi wa nyadhifa mbalimbali serikalini na vyombo vyake
(viongozi na watendaji waandamizi). Hii inapelekea kuwepo hisia za upendeleo
na udini.
|
Katiba mpya iweke masharti ya
kuzingatia uwiano wa kidini kwa wateuzi katika uteuzi wa nyadhifa mbalimbali
(viongozi na watendaji waandamizi serikalini) kuondoa hisia za kuwepo
upendeleo wa kidini.
|
29
|
Kwamba Katiba iliyopo inampa madaraka
rais kuchagua mawaziri kutokana na wabunge waliochaguliwa na wananchi. Hii
imepelekea wabunge kushughulikia maslahi ya majimbo yao zaidi kuliko maslahi
ya kitaifa.
|
Katiba mpya iweke wazi kuwa baraza la
mawaziri halitatokana na wabunge waliochaguliwa na wananchi, Rais achague
mawaziri kama watendaji wa serikali nje ya bunge. Mawaziri waingie bungeni
kama wawakilishi wa serikali na siyo wawakilishi wa majimbo na serikali kama
ilivyo sasa.
|
30
|
Kwamba Katiba iliyopo inampa madaraka
makubwa rais kiasi cha kuwaweka watu kizuizini bila kufikishwa mahakamani.
Huu ni uvunjifu wa haki za binaadamu.
|
Katiba mpya isimpe madaraka rais, mkuu
wa Mkoa na wa wilaya ya kumuweka mtu kizuizini bila kufikishwa mahakamani.
Katiba mpya isimpe rais mamlaka ya kimahakama.
|
31
|
Sheria imempa madaraka rais kuteua
watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kuondoa Rushwa. Hii imepelekea Taasisi hiyo
kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na kuingiliwa utendaji wake na
Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa kuteuliwa
watendaji wa TAKUKURU na Bunge na bila kuingiliwa utendaji wake na Mkurugenzi
wa Mashitaka ya Jinai.
|
32
|
Katiba iliyopo inampa madaraka rais
kuteua Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Hii imepelekea kuwepo kwa malalamiko ya
kutokuwepo tume huru ya uchaguzi. Kwamba kwa ajili hii matokeo ya uchaguzi wa
rais pindi yanapotangazwa na tume ya uchaguzi hayawezi kuhojiwa mahakamani.
|
Katiba mpya itoe madaraka kwa bunge
badala ya rais kuteua Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Katiba mpya vilevile
itoe fursa kwa raia kuhoji matokeo ya uchaguzi ya rais mahakamani. Mahakama
na sio tume ya uchaguzi kiwe ndicho chombo cha kuthibitisha uhalali wa
matokeo ya uchaguzi wa rais.
|
33
|
Kwamba Katiba iliyopo inampa madaraka
rais ya kulivunja bunge. Hii ni kuwanyima haki wananchi ya kuendelea kuwa na
viongozi waliowachagua kwa ridhaa yao.
|
Katiba mpya isimpe mamlaka rais
kulivunja bunge.
|
34
|
Kwamba Katiba iliyopo inampa madaraka
rais ya kuteua Jaji Mkuu, Jaji Kiongozi, Jaji wa Mahakama Kuu na Jaji wa
Mahakama ya Rufaa bila ya idhini ya bunge. Hii imepelekea kuwepo kwa
malalamiko ya mahakama hizo kutokuwa huru katika kutekeleza majukumu yake.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa uteuzi
wa nyadhifa hizo uwe kwa kushauriana Rais na Tume ya Utumishi wa
Mahakama na kuidhinishwa uteuzi huo na bunge.
|
SEHEMU
YA IV: UWAKILISHI WA RAIA KATIKA MIHIMILI MIKUU YA DOLA
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
35
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui umuhimu
wa kuwepo wawakilishi wa dini katika vyombo vifuatavyo: Bunge, Baraza la
Wawakilishi, na Baraza la Madiwani, Mabaraza ya Usalama. Hii inapelekea
kufanywa maamuzi ambayo yako nje na maadili na sheria za dini husika.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa kuwepo
uwakilishi wa dini katika vyombo hivyo vilivyotajwa kwa ajili ya kulinda
maadili na maslahi ya dini husika.
|
36
|
Kwamba Katiba iliyopo inaruhusu mtu
kujitangaza kufaa kwake katika kugombea uongozi na hivyo kupelekea mazingira
ya rushwa na uongo. Hii imepelekea wanasiasa kujipachika sifa na uwezo wasio
nao.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa wananchi
kupendekeza wagombea kupitia vyama vya siasa au vikundi maalum (wagombea
binafsi) ili kupigiwa kura. Wananchi wapendekeze na wawanadi wapigiwa
kura.
|
37
|
Kwamba Katiba iliyopo inamzuia raia
yeyote kugombea uongozi katika nafasi yoyote mpaka awe ni mwanachama wa chama
cha siasa kilichosajiliwa. Hii inawanyima raia wasio wanachama wa
vyama vya siasa kushiriki katika shughuli za uongozi na bila shaka kuzuia
wenye sifa za kuongoza taifa kwa kigezo cha kutokuwa mwanachama wa chama cha
siasa.
|
Katiba mpya itoe nafasi kwa mgombea
binafsi kugombea katika nafsi zote za uongozi kwa sharti ya
kupendekezwa na kundi la watu raia wa Tanzania wasiopungua kumi na moja.
|
38
|
Kwamba Katiba iliyopo inapiga marufuku
kuwepo wa vyama vya kisiasa vya kidini.
|
Katiba mpya iruhusu uwepo wa vyama vya
kisiasa vya kidini kama ilivyo katika nchi nyingine mathalani Ujerumani.
|
39
|
Kwamba Katiba iliyopo inapiga marufuku
kuandikishwa chama cha siasa chenye malengo ya kutetea maslahi na maendeleo
ya dini. Hii inatoa tafsiri potofu ya dini kutorandana na siasa
|
Katiba mpya iruhusu kuandikishwa chama
cha kisiasa chenye lengo la kupigania haki, maendeleo na maslahi ya imani ya
dini husika. Katiba itambue uhalali wa raia kupigania maslahi na maendeleo ya
dini yake.
|
40
|
Kwamba Katiba iliyopo inatambua
mgawanyo wa nchi katika mikoa na wilaya n.k. kiutawala. Wakuu wa mikoa na
wakuu wa wilaya wanateuliwa na rais.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa kuigawa
nchi katika majimbo yatayoongozwa na serikali za majimbo zitakazochaguliwa na
wananchi. Mkuu wa jimbo achaguliwe na wananchi.
|
41
|
Kwamba Katiba iliyopo inaruhusu kuwepo
kwa viti maalum vya wanawake bungeni kwa misingi ya jinsia. Yamekuwepo
malalamiko ya kwamba baadhi ya wanaoteuliwa kwa kigezo cha jinsia hawana sifa
na uwezo wa kuongoza na kwamba watu wa jinsia ya kiume hawapewi upendeleo na
kwamba ipo hatari ya kuzuka mfumo jike (kama Kenya inakoelekea).
|
Katiba mpya ifute uwakilishi kupitia
viti maalum katika bunge kwa misingi ya jinsia. Mtu achaguliwe kwa sifa za
kiutendaji na siyo jinsia yake.
|
42
|
Kwamba Yapo malalamiko dhidi ya wabunge
kutowajibika katika majimbo yao na hakuna utaratibu unaowawezesha wapiga kura
kuwaondoa wabunge hao. Kwamba wabunge hawana makazi katika sehemu
wanazoziwakilisha.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa
kuwawezesha wapiga kura kuwadhibiti na kuwawajibisha wabunge wao ambao
hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Katiba mpya iwawezeshe wapiga kura
kuwaondoa wabunge wasiotekeleza ipasavyo wajibu wao bila kusubiri kipindi cha
uchaguzi mpya. Katiba iweke masharti ya mbunge kuwa na makazi katika jimbo
analoliwakilisha.
|
43
|
Kwamba Katiba iliyopo inatambua kuwepo
kwa uchaguzi mdogo wa mbunge pindi zinapotokea sababu mbalimbali kama vile
kufariki kwa mbunge n.k. Hii imepelekea taifa kugharimika sana kwa ajili ya
chaguzi hizi.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa kujaza nafasi
ya mbunge inapokuwa wazi. Nafasi ya mbunge ijazwe mathalani kwa utaratibu wa
chama husika au kikundi husika kumteuwa mwanachama au mtu mwingine kurithi
nafasi ya mbunge aliyeondoka.
|
44
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui uwepo
wa serikali ya mseto. Hii inapelekea serikali kuundwa kwa uwakilishi wa watu
wachache na hivyo kukosa sifa ya serikali ya umoja wa kitaifa.
|
Katiba mpya iweke utaratibu wa kuunda
serikali ya mseto.
|
SEHEMU V:
HIFADHI NA MATUMIZI YA ARDHI NA RASILIMALI ZA TAIFA
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
45
|
Kwamba Katiba iliyopo imempa haki mtu
ya kumiliki na kutumia mali zake atakavyo bila kuchunga sheria na imani ya
dini yake au za watu wengine. (Mathalani mtu kurithithisha mali yake atakavyo
yeye kinyume na sheria ya dini yake)
|
Katiba mpya iweke bayana haki ya mtu
kumiliki na kutumia mali yake kwa kuzingatia sheria ya imani ya dini yake.
|
46
|
Kwamba Katiba iliyopo haizungumzii
umuhimu wa sensa katika kujua takwimu za watu. Hii imepelekea kutolewa
takwimu zisizokuwa rasmi na zenye malengo ya upotoshaji.
|
Katiba iitake serikali kufanya
sensa baada ya kila miaka mitano kujua idadi ya watu, hali zao na idadi ya
wafuasi wa dini mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kuweka uwiano
katika kutoa haki sawa na huduma kwa raia wake.
|
47
|
Kwamba Katiba iliyopo imetoa mwanya
kwa ardhi yetu kutumika kwa malengo ya ukoloni mamboleo. Mathalan
haitoi pingamizi kwa mataifa ya nje kuweka vituo vya kijeshi na upelelezi
katika ardhi ya Tanzania.
|
Katiba mpya isiruhusu kwa hali yoyote
kuwekwa kwa vituo vya kigeni vya kijeshi na upelelezi katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
|
48
|
Kwamba Katiba iliyopo imeimilikisha
ardhi kwa serikali yaani kikatiba ardhi ni mali ya serikali. Hii imepelekea
serikali kuwa na mamlaka ya kumilikisha ardhi kwa yeyote bila ridhaa ya wananchi,
hata kama ikiwa wanaomilikishwa ni wageni. Imerahisisha pia uporwaji
unaofanywa na wageni (mataifa ya kigeni wakishirikiana na baadhi ya viongozi)
wa maliasili zilizoko chini ya ardhi (madini) na juu yake (wanyama pori,
misitu, mazao ya baharini n.k.)
|
Katiba mpya iweke wazi kwamba ardhi ni
mali ya raia (wananchi) na serikali ni wakala tu wa raia katika kugawa ardhi
kwa uadilifu na kwa ridhaa ya raia. Umiliki wa ardhi uweze kuondolewa kwa
mmiliki iwapo atashindwa kuiendeleza ardhi kwa miaka mitatu mfululizo. Raia
aweze kuuza ardhi aliyomilikishwa kwa raia mwingine au kukodisha kwa asiye
raia kwa mkataba unaoweza kuhuishwa kila baada ya miaka mitatu. Rais aweze
kusitisha umiliki wa ardhi wa mtu au kikundi kidogo cha watu kwa manufaa ya
waliyo wengi maadam mmliki au wamiliki watalipwa fidia inayolingana na
thamani ya ardhi wanayopoteza umiliki na vilivyomo kwa wakati huo
|
49
|
Kwamba Katiba iliyopo haitambui
umilikishaji wa ardhi kwa uwiano wa kidini. Hii imepelekea mathalani upimaji
wa maeneo mapya kupitishwa bila kuainisha maeneo maalum kwa dini husika na
hivyo kupelekea mivutano isiyo ya lazima. Zipo hisia za umilikishaji wa ardhi
kwa upendeleo wa kidini.
|
Katiba mpya itoe maelekezo kwa sheria
za mipango miji kulenga ugawaji wa ardhi kwa kuainisha maeneo ya dini kwa
mujibu wa uwiano wa kidini katika eneo husika.
|
50
|
Kwamba Sheria za nchi hazimpi madaraka
Mkaguzi Mkuu wa Serikali kumfungulia mashitaka mtumishi wa serikali
anayetuhumiwa kufanya ubadhirifu na ufisadi katika mali ya umma.
|
Katiba impe mamlaka huru Mkaguzi Mkuu
wa Serikali kumfungulia mashitaka yeyote anayetuhumiwa kwa ubadhirifu au
ufisadi wa mali ya umma.
|
51
|
Kwamba Katiba iliyopo iko kimya juu ya
umiliki, ulinzi, matumizi na udhibiti wa mali za asili za Tanzania, zikiwepo
madini, mazao ya baharini, wanyama pori, misitu n.k. Hii imepelekea matumizi
ya kiholela, ubadhilifu na uporaji wa mali hizi unaofanywa na mafisadi wa
ndani na nje na hivyo kuendelea kusababisha hali ya umasikini kwa Watanzania.
|
Katiba mpya ibainishe wazi kwamba mali
za asili ni mali za raia wa Tanzania tu kwa kila upande wa muungano na iweke
utaratibu madhubuti wa kulinda mali hizi dhidi ya ufisadi wa ndani na nje.
|
SEHEMU
YA VI: VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WA RAIA
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
52
|
Kwamba Katiba iliyopo imetoa mwanya
kwa ardhi yetu kutumika kwa malengo ya ukoloni mamboleo. Mathalan haitoi
pingamizi kwa mataifa ya nje kuweka vituo vya kijeshi na upelelezi katika
ardhi ya Tanzania.
|
Katiba mpya isiruhusu kwa hali yoyote
kuwekwa kwa vituo vya kigeni vya kijeshi na upelelezi katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
|
53
|
Kwamba Katiba iliyopo haidhibiti
kikamilifu uundwaji kiholela wa tume na majeshi ya ulinzi nje ya yale ya
serikali. Mathalani tume ya majeshi ya Kikatoliki katika Jeshi la Ulinzi la
Tanzania na kuwepo kwa Jeshi la Wokovu la Wakristo
|
Katiba mpya iendelee kupiga marufuku
kuwepo kwa tume na majeshi haya yasiyo rasmi na kuweka utaratibu thabiti wa
kuziba mianya ya kuundwa mengine ya mfano huo.
|
SEHEMU
YA VI: USAWA, HAKI YA KUISHI NA HAKI ZA BINADAMU
NA.
|
HOJA
|
MAONI
|
54
|
Kwamba Katiba iliyopo inaitambulisha
Tanzania kama nchi ya ujamaa tofauti na uhalisia wa mazingira ya
kisiasa na kiuchumi na kiitikadi yaliyopo nchini
|
Katiba mpya isitishe kuitambulisha
Tanzania kama nchi ya kijamaa na Watanzania kama wajamaa. Ubaki mfumo wa
siasa ya kujitegemea (kutokuwa tegemezi na ombaomba).
|
55
|
Kwamba Katiba iliyopo haitoi tafsiri
yakinifu ya neno USAWA (mfano usawa katika mirathi, usawa katika majukumu ya
mwanamke na mwanamume katika jamii n.k).
|
Katiba mpya ianishe tafsiri sahihi ya
USAWA kwa mujibu wa imani za dini ya mtu. Hii itasaidia wananchi kutafsiri
USAWA kwa mnasaba wa mafundisho ya imani ya dini zao.
|
56
|
Kwamba Katiba iliyopo inatoa uhuru na
haki ya kuishi usio na mipaka na usiotilia maani uhuru na haki za wengine
kuishi.
|
Katiba mpya iweke mipaka ya uhuru na
haki ya kuishi yenye kuzingatia uhuru na haki ya kuishi ya wengine. Mathalani
iweke sheria ya kuuawa kwa mtu aliyeuwa mwingine au watu wengine kwa dhulma.
|
57
|
Kwamba Katiba iliyopo haikatazi
mahusiano ya jimai na kimapenzi nje ya ndoa pamoja na mahusiano ya namna hiyo
kwa watu wa jinsia moja. Hii imepelekea kuporomoka kwa maadili na
mparaganyiko katika jamii, kuenea kwa watoto wa mitaani na maradhi ya ukimwi
na maradhi mengine ya zinaa.
|
Katiba isiruhusu mahusiano yoyote ya
kimapenzi nje ya ndoa na mahusiano ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja na
ndoa ya watu wa jinsia moja. Katiba ipige marufuku vitendo au utengenezaji wa
mazingira yanayopelekea au kurahisisha mahusiano ya namna hiyo.
|
58
|
Kwamba Mfumo wa Elimu uliopo hauwapi
fursa Waislamu kuchunga maadili na itikadi ya dini yao. Ipo mitaala ya elimu
iliyotofauti na ile ya elimu ya Mtanzania ambayo imeruhusiwa (Cambridge,
Marekani n.k). Kwamba Waislamu wana haki ya msingi ya kufuata mfumo wa elimu
wa Kiislamu kama sehemu ya ibada katika Uislamu.
|
Katiba mpya iruhusu watu wa dini
mbalimbali kuwa na mfumo wa elimu utakaozingatia imani, maadili, mila,
itikadi na desturi za dini zao.
|
43
|
Kwamba Sheria za nchi zinampa mamlaka
makubwa Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai [DPP] kiasi cha kuwa na hiari
kuifikisha kesi mahakamani au kutoifikisha au hata kuifuta kabisa bila idhini
ya hakimu.
|
Katiba mpya impunguzie madaraka
Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai. Imlazimishe kupeleka kesi mahakamani na
isimpe uwezo wa kufuta kesi kwa matakwa yake. Uamuzi wa kuendelea au kufuta
kesi uwe ni wa mahakama.
|
ANGALIZO:
MAONI HAYA YAMEKUSANYWA KWA LENGO LA KUFANIKISHA MCHAKATO WA KUANDIKWA KATIBA
MPYA. HIVYO BASI MUISLAMU YEYOTE ANAWEZA KUENDELEA KUCHANGIA KWA KUZIDISHA
VIPENGELE AMBAVYO VIMESAHAULIWA AU KUPUNGUZWA NA VIMEKOSEWA KWANI UKAMILIFU NI
WA ALLAH [S.W.]
WAKUSANYAJI
NA WARATIBU WA HOJA NA MAONI
1.
Sheikh Salim A.
Barahiyaan [LLB Shariah, LLM Shariah & Law]
2.
Dr. Abu-Malik
Juma [PhD Economics]
TAKWIMU
IDADI
YA MIKOA ZILIPOFANYIKA SEMINA SHIRIKISHI
TANZANIA
BARA 17
ZANZIBAR 1
Published by yusouf Hassan
0 comments:
Post a Comment