Wednesday, December 24, 2014

PICHA ZA MSIKITI WA MWENGE - MOSHI



Sehemu ya Kuchukulia udhu kwa wanaume


Upande wa mbele wa msikiti


Upande wa Kibla wa Msikiti




Monday, December 8, 2014

SWALA YA KUOMBA MVUA.

Ukame ni alama ya watu kuwa mbali na Utiifu kwa Mwenyezi Mungu (SW) na ishara wazi yakukithiri maasi. Kumuasi Mwenyezi Mungu (SW) kunaleta shari na kunafuta Baraka. Na miongoni mwa rehema zake kwa waja wake na kule kuwawekea Swala ya kuomba mvua, wakapata kurudi kwa Mola wao na kutaka msamaha kwake awaondolee shida waliyonayo, ili mvua iwateremkie ikiwa ni rehema kutoka Kwake kwa waja wake. 

Kila ugonjwa una tiba yake, ardhi ikiwa kavu na kupatikana ukame. Uislamu unamaanisha kuswali swalatul Istiskai nayo ni Swala ya kumuomba Mwenyezi Mungu kuteremsha mvua. Leo Swala hii imesahulika kabisa katika Umma wa kislamu. Waislamu wakipata matatizo ya uhaba wa Mvua, moja kwa moja wanaelekea kuomba majini na mashetani. Mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) yako wazi kabisa kuwaelekeza Waislamu katika njia ya Allah (Subhaanahu wa Taala) wakati wowote na hali yoyote sawa wakati wa raha au shida. Kumtii Mwenyezi Mungu ndio mambo yote. Amesema Mwenyzi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :
قال تعالى) : وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِمْ مِنْ رَبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِنْ فَوْقِهِمْ وَمِنْ تَحْتِ أَرْجُلِهِمْ مِنْهُمْ أُمَّةٌ مُقْتَصِدَةٌ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ) [المائدة: 66] {{Na kama wangalisimamisha Taurati na Injili na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao, kwa yakini wangalikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Lakini wako watu miongoni mwao washikao njia nzuri. Lakini wengi wao wanayoyafanya ni mabaya kabisa}}.
Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى : (وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِمْ مِنْ رَبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِنْ فَوْقِهِمْ وَمِنْ تَحْتِ أَرْجُلِهِمْ مِنْهُمْ أُمَّةٌ مُقْتَصِدَةٌ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ ) [المائدة: 66]
{{Nikawaambia; Ombeni msamaha kwa Mola wenu. Hakika Yeye ni Mwingi wa msamaha. Atakuleteni mawingu yanyeshayo mvua nyingi}}.
Na akasema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آَمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ )[الأعراف: 96] {{Na lau kama watu wa miji wangaliamini na kuogopa, kwa yakini tungaliwafungulia baraka za mbingu na ardhi. Lakini walikadhibisha; tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma}}.
Kumuasi Mwenyezi Mungu ndio sababu ya kuleta shari na kuondoka kwa baraka.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَنْ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَى مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ) [آل عمران: 135] {{Na ambao wanapofanya uchafu au kudhulumu nafsi zao, hukumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha kwa dhambi zao. Na nani anayesamehe dhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu}}.
Ametaja Ibn Qayyim baadhi ya maafa yanayoletwa na maasi; huleta udhalifu, huharibu akili, huwaondosha haya, hudhoofisha moyo, huondosha neema, hutia maradhi moyo, huleta nuksi, hupotosha ya moyo, hufanya moyo kuwa mdogo, huondosha karama, pia Baraka, na kulaumiwa, kutishika, huondosha hima ya kumcha Mwenyezi Mungu.
Ukame ni alama ya kuwa watu mbali na twaa ya Mwenyezi Mungu, na ishara ya kuzidi maasi. Hali ya anga inabadilika kutokana na maasi.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى): ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُمْ بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ) [الروم: 41]
{{Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Awaonjeshe adhabu ya baadhi ya mambo waliyofanya, huenda wakarudi wakatubia kwa Mwenyezi Mungu}}.
Na anasema Anas bin Malik: Upepo ukiwa mkali hujulikana hilo kwa uso wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Amepokea Abu Huraira hadithi: kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Hakisimami Qiyama mpaka iondoke ilimu, na kuzidi Zilzaal, na zahama kuwa karibu, na kudhihiri fitna, na kuzidi mauaji, mpaka itakua kwenu mali nyingi]. Ufupisho ni kujirudi nafsi, na kuomba msamaha kwa Allah pamoja na kufuata sheria za Allah (Subhaanahu wa Taala).
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : يُنَبَّأُ الْإِنْسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ13 بَلِ الْإِنْسَانُ عَلَى نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ 14وَلَوْ أَلْقَى مَعَاذِيرَهُ 15)[القيامة13: 15]
{{Siku hiyo ataambiwa mwanadamu aliyotanguliza na aliyoyaakhirisha. Bali mtu ni shahidi juu ya nafasi yake}}.
Na neno lake Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Tunajilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wa nafsi zetu, na uovu wa matendo yetu]. Imepekewa kwa Masahaba wakisema: Alitusalisha Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) swala ya usubuhi Hudeibiyah kukiwa na mawingu usiku, baada ya hapo akatukabili na kusema: Je mnajua alivyosema Mwenyezi Mungu? Wakajibu maswahaba: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua. Akasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Baadhi ya waja wangu wamekua waumini ni wale waliosema tumeteremshiwa mvua kutokana na fadhila zake Mwenyezi Mungu, na makafiri tumeteremshiwa mvua kutokana na nyota fulani].
 Namna ya kuswali Swala ya Istiskai (Swala ya Mvua)
Ametoka ‘Abdillah ibn Yazid pamoja na Burai Bin ‘Azib na Zeid Bin Arkam kuswali ya Swala ya istiskai, akasimama na kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha, kisha wakaswali rakaa mbili, kudhihirisha kisomo, bila adhani wala ikama. Na kama alivyopokea ‘Abdillah bin Zaid kwamba Mtme (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ameswali swala ya Istiskai kuelekea kibla, na kugeuza kishali chake na kuswali rakaa mbili. Amepokea Anas Bin Malik kuwa Mtume hainui mkono wake anapo omba isipokuwa katika swala ya istiskai, na alikuwa akiinua mkono wake mpaka ikionekana weupe wa makwapa yake.
Na ni sunna kuwalingania Waislamu wote kumcha Mwenyezi Mungu na kutaka radhi zake Mwenyezi Mungu kwa kutoa sadaka na kuunga kizazi. Amepokea Anas Bin Malik akisema: nimemsikia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [ Amesema Mwenyezi Mungu ewe mwanaadamu unaponiomba na ukataraji kutoka kwangu nitakusamehe kwa yale uliyo nayo bila kujali, ewe mwanaadamu madhambi yako yakafika mbinguni kisha ukaniomba msamaha nitakusamehe. Ukifanya madhambi kiasi cha ‘arshi na hukunishirikisha Mwenyezi Mungu nitakusamehe madhambi hao]. Walipopatwa Makureish na ukame na kula mfu na mifupa. Abu Sufyan alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumuambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu umetuamrisha kuunga kizazi. Na waja wako wanaangamia, tuombee Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu akaomba, ikateremka Mvua mpaka wakaogopa watu.
Amesema Hassan Basri: ‘Zidisheni kutaka msamaha kwa Mwenyezi Mungu nyumbani kwenu, kwenye meza zenu, njiani, sokoni, makao yenu, na popote mlipo, kwani hamjui wakati gani utashuka msamaha wa Allah.
Mwisho
Ndugu katika Imani, Sababu kubwa ya kukosekana mvua ni kudhihiri machafu baharini na nchi kavu. Ili tuweze kupata rehma ya Mwenyezi Mungu na kuteremshiwa mvua kutoka mbiguni ni wajibu juu ya kila Muislamu kurudi kwa Allah kwa kuomba msamaha na kuendelea kufanya mambo ya kheri na kujiepusha na mambo mabaya.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Atuteremshie mvua na rehma na Baraka. Naelekeza wito wangu kwa watu wote kumuomba Mwenyezi Mungu Atubariki. Namuomba Mwenyezi Mungu kuteremsha mvua na kuwarehemu waja wake na miji yake.

UMUHIMU WA SWALA

swala ni nguzo ya pili katika uislamu baada ya shahada,na ni amali ya kwanza atakayo ulizwa siku ya kiyama swala ikiwa mzuri basi amali zake zote nyingine zitakuwa mzuri na swala ikiwa ni mbaya basi amali zake nyingine zitakuwa mbaya,na swala ni ndio inamtafautisha muislamu na asiekuwa muislamu ,na mwenye kuisimamisha swala huwa amesimamisha dini na mwenye kuacha swala huwa ameivunja dini 

 

Dini ya kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu ameitukuza na kuridhia nayo, na ameweka malipo makubwa kwa vile vinavyotamani nafsi na uislamu umejengwa na misingi na hatosalimika anaekeuka misingi hayo na adhabu iumizayo, na atakae fuata misingi hayo atapata utukufu na heshima hapa duniani na kesho akhera, na miongoni mwa misingi hayo ni swala, swala ambao ni msingi wa dini na nguzo ya pili baada ya kutamka shahada mbili, na swala ni fadhila kubwa ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [ Swala ni bora, na atakae weza kuzidisha basi na azidishe].
Swala ni nguzo ya pili katika uislamu. Imepokewa na Anas akisema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [Nimependekezwa na wanawake mafuta mazuri na nikajaaliwa kuwa swala ndio kitulizo cha macho yangu]. Na ni ibada ya kwanza aliyofaradhisha Mwenyezi Mungu, na mwanzo atakayohisabiwa mwanadamu, na ndio wasia wa mwisho ambao Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ameusia umma wake akisema: [ Swala, swala na watumwa wenu]. Na ndio mwanzo itakayopotea na ikipotea imepotea dini.
Na kuonyesha umuhimu wa swala kufaradhishwa katika mbingu ya saba, na ndio inaowekwa mafungamano kati ya mja na mola wake, na inakataza maovu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ( [العنكبوت: 45] {{Hakika Swala humzuilia huyo mwenye kusali na mambo machafu na maovu}}
Wengi miongoni mwa watu wanaswali swala ya ghurabu (kudonoa), hawana utulivu, wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kwa uchache, kugeuka katika swala kujikuna, mfanya biashara kufikiria mali yake anaposwali.
Hadithi iliopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akimuambia mtu ambae hakua na utulivu katika swala “Rejea ukaswali kwani hujaswali”
Mambo Ambayo Husababisha kuhudhurisha Moyo unapokuwa katika Swala
Mambo ambayo husababisha kuhudhurisha moyo ni kujua unacho kizungumza au unachokifanya, mfano;
Unapotoa Takbir na kuinua mikono miwili hii inamaanisha kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Na ukiweka mkono wa kulia juu ya kushoto ni kujidhalilisha mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na ukirukuu inamaanisha kumuadhimisha Mwenyezi Mungu.
Na ukisujudu ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu.
Anaposema: “Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu” anaitikia Mwenyezi Mungu amenishukuru mja wangu, na anaposema “ Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo” anasema Mwenyezi Mungu: amenisifu mja wangu, na anaposema mwenye kumiliki siku ya mwisho, anasema Mwenyezi Mungu: amenitukuza mja wangu., anaposema kwako wewe nakuabudu na kwako wewe nataka msaada, anasema Mwenyezi Mungu: haya ni kati yangu na mja wangu.
Anaposema ametakasika Mola wangu aliekua mkubwa, na ukisema ametakasika mola wangu alie juu, Mwenyezi Mungu anasikia hata kama ni kwa sauti ya chini, anasikia kila neno unalolisema na hata kama ni kwa sauti ya chini.
Kumuomba Mwenyezi Mungu usaidizi wa kufanya amali nzuri, imepokewa na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie katika kukutaja na kukushukuru, na kufafanya uzuri ibada yako].
Kujua kuwa unyenyekevu ni roho ya swala, Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى (الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ) [المؤمنون: 2]
{{Ambao katika Sala zao huwa ni wanyenyekevu}}.
Wito wa kuhifadhi Swala
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَى). [البقرة: 238]
{{Angalieni sana Sala – zote kuzisali kwa jamaa- Na khasa ile Sala ya kati na kati}}.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى : قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ1 الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ [المؤمنون1: 2]
{{Kwa hakika wamefaulu waumini. Ambao katika Sala zao huwa ni wanyenyekevu}}.
Na akasema tena Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ 9أُولَئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ 10الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ )[المؤمنون9: 11]
{{Na ambao Sala zao wanahifadhi. Hao ndio warithi. Ambao watarithi pepo; wakae humo milele}}.
Ndugu Waislamu, Hakika Sala ni nguzo muhimu katika dini ya kiislamu. Bali Uislamu wa mtu haukamiliki bila ya Sala. Na Nguzo hii ndio ya kutafautisha baina ya Muislamu na kafiri. Amepokea Jabir hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: “Kati ya Muislamu na kafiri ni kuwacha swala” na akasema tena Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Tofauti kati yetu na wao ni kuacha swala, atakae wacha swala ni amekufuru]. amepokea ‘Abdillah bin Shakik Ukeili, amesema maswahaba yake Mtume walikuwa hawaoni ukafiri isipokua ni kuacha swala.
Umuhimu wa kuswali Swala ya Jamaa.
Ndugu katika imani, Sala ya jamaa ni wajibu kwa wanaume. Hadithi za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) zimeweka wazi jambo hili. Amepokea Ibn Abbas hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [ Mwenye kusikia adhana na asijibu basi hana swala isipokua mwenye udhuru]. Amepokea Abu-Hureira amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [ nimeazimia kuamrisha pote la watu waniletee kuni, kasha niwaendee waja wasiokuja kuswali swala kwa jamaa nichome nyuma zao].
Kuwahimiza Watoto kuswali na kuwalea kwa Mfumo huo
Watoto ni neema ya Allah (Subhaanahu wa Taala) kwa waja wake. Na neema ikiwa ni ya Allah ni lazima ichungwe kulingana na matakwa yake Allah. Mwenyezi Mungu Alipotupatia neema hii, Hakutuacha tuitumie neema hii kama tunavyotaka sisi, bali Yeye Mwenyewe Alichukua jukumu la kutufundisha namna ya kuitunza neema hii kupitia kwa mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Na miongoni mwa mafundisho hayo, ni kuwafundisha watoto Sala wakiwa wadogo kuanzia miaka saba. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, na wapigeni wakiwa na miaka kumi].
Na Mwenyezi Mungu Akututahadharisha tusiwe ni wenye kupuuza jukumu hilo.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا ([التحريم: 6]
{{Enyi mlioamini, Jiokoeni nafsi zenu, na watu wenu, na moto ambao kuni zake ni watu na mawe}}. Na ameseme Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
وقال تعالى) : وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ([طه: 132]
{{Na waamrishe watu wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo}}.
Mwisho
Ndugu katika imani, Sala ni jambo kubwa lina uzito mkubwa katika Dini yetu. Muislamu akiacha kusali basi ajuwe yuko katika hali mbaya, ikiwa ataendelea na hali hiyo mpaka afikiwe na mauti basi mwisho wake ni mabaya. Kwa hivyo, tufanyeni bidii kuhifadhi Sala kwa wakati wake. Na miongoni mwa kuhifadhi sala ni kuisoma na kuifahamu kama alivyofundisha Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), ili uweze kuitekeleza kama alivyo kuwa akitekeleza Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Tunamuomba Allah Atupe tawfiq ya kuweza kutekeleza sala kwa wakati wake. Na tuweze kusali kama alivyo kuwa akisali Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).


FADHLA ZA KUSOMA QUR’ANI

Qur'ani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni kitabu Chake kitukufu. Si kama maneno yoyote wala kitabu chochote, ni Teremsho kutoka kwa Mwingi wa hekima Mwenye kuhimidiwa. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kushinda Ameweka adabu ambazo yatakikana zitungwe wakati wa kuisoma, kwa kuitukuza na kuiheshimu, Akamuamuru Mwenye kuisoma awe na tohara na awe mnyenyekuvu na mwenye kukizingatia anachokisoma na adabu nyinginezo ambazo yapaza kuzitunga wakati wa kusoma Qur'ani. 



  Ewe Muislamu ulipoumbwa na ukaletwa hapa Duniani uliwekewa katiba na mfumo wa kuishi na njia ya kupita mwanzo mpaka mwisho, nzuri na mbaya, yote hayo utayapata kwenye Qur’an ukifundishwa na Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).
Kusoma Qur’an na Adabu zake
Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehema Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na kutakia radhi Maswahaba na waliokuja baada hao mpaka qiyama.
Ama baadu: mazungumzo yetu ni kuhusu kitabu ambacho ndio msingi wa kufaulu kwenu, chenye kuwatoa kwenye kitua, ndani yake kuna khabari ya waliokuja kabla yenu na watakaokuja baada yenu na hakimu kati yenu, chenye kupambanua baina ya haki na batili. Mwenye kukiacha ameumia, mwenye kutaka uongofu kwa hicho ataongoka, na mwenye kutaka kuongoza na kitabu kingine amepotea; ni kamba ya Allah ya kuaminika isiyokatika; ni utajo wa Mwenyezi Mungu ni njia iloyonyoka, mwenye kuifuata hapotei na mwenye kuifuata hachanganyikiwi. Hawashibi nayo wanavyuoni na maajabu yake hayapungui. Atakaye ukweli ataupata humo na mwenye kuhukumu nacho atahukumu kwa usawa. Matakwa ya Allah ni tuisome Qur’an ili atuongoza na atuingize peponi.
Enyi waumini, Someni Qur’an na muwasomeshe watoto wenu au wenzenu, muwe mumebebwa na mazingira yake, frikra zenu na mawazo yawe katika mazingira ya Qur’an, muwahifadhisha watoto wenu kwa udogoni, kwani mkifanya hivyo, inaifanya igande vizuri zaidi ndani ya nyoyo zao, kwani kuhifadhi udogoni ni kama kutia naqshi kwenye jiwe.
Ewe waja wa Mwenyezi Mungu, Muongopeni Mola na muwe na hamu na Kitabu hiki. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال الله عز وجل: (إنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنْفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَنْ تَبُورَ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ) [فاطر: 30]
{{Hakika wanaosoma hiki Kitabu cha Allah na wakasimamisha swala na wakatoa kwa mali yao tulizowapa kwa siri na dhahiri, wanatarajia biashara isiofilisika, na hakika Allah atawalipa awaongeze, kwani yeye mweyekusamehe saana na ni mwenye kushukuriwa}}. Na mke wa Mtume ‘Aisha akazidi kutufafanulia akisema: ‘Kusoma kwa Qur’an kunatafautiana, kuna anayesoma hodari. Hivyo, thawabu zake ni nyingi kiasi cha kutangamana na Malaika na anayesoma akigongagonga atapata malipo mara mbili. Vilevile Abi Umama akamwambia amemsikia Mtume akisema: [Someni Qur’an, itakufaa siku ya Qiyama kuwaombea shufaa. Haya yote ni fadhila za Qur’an na fadhila za kusoma Qur’an]. Na Mtume wetu (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alimuusia Abu Said akimwambia : [Nakuusia umche Mwenyezi Mungu, kwani hilo ndio kichwa cha kila kitu, na utoke kwenda Jihad kwani hilo ndio daraja kuu la Uislamu na umtaje Mwenyezi Mungu kwa wingi, na usome Qur’an ukifanya hivyo roho yako itakuwa mahali pazuri mbinguni na utakuwa na utajo upo ardhini].
Adabu za kusoma Qur’an
Kusoma kwa ajili ya Allah (Subhaanahu wa Taala)
Waja watalipwa kulingana na nia zao. Mtume anatutolea khabari kuwa watu watalipwa vibaya japokuwa tunawaona wakifanya mema, nao ni sampuli tatu:-
Mtu anajishughulisha na Qur’an kuisoma vizuri, kuikusanya n.k
Mtu aliyeuliwa jihad fi sabilillahi.
Mtu tajiri anaye toa sana.
Kumbe wote hawa watatu, wanafanya riya, Allah atamwambia msomaji Qur’an: Si nilikufundisha Qur’an? Atajibu: Ndio ewe Mola; baadaye ulifanya nini? atajibu nilikua nikiisoma usiku na mchana, Mwenyezi Mungu atasema: ‘Umesema urongo, na Malaika watazidi kumkaripia ‘muongo we, na watasema Ewe Mola: huyu bwana, alikuwa akisoma kwa ajili ya watu, na tukaachia watu wamlipe kule kule duniani. Mungu atawaamrisha Malaika wamtie motoni (Mwenyezi Mungu atulinde na hayo)
Kusoma hali akiwa na utwahara
Hapana shaka kuyasoma maneno ya Allah ukiwa msafi, ndio bora kama vile kupiga mswaki, kutawadha n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakika midomo yenu, ndiyo njia za kusoma Qur’an, isafisheni kwa miswaki]. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema tena: [Ikiwa mja anaswali, Malaika humjia, na wakamsimamia nyuma yake wakimsikiliza Qur’an na wanaendelea hivyo mpaka anyamaze]. Na je ikiwa mja kinywa chake chanuka? Malaika watakaa kando.
Kusoma kisawasawa
Mola wetu anatuamrisha kuisoma Qur’an na Mtume wetu anatushinikiza hivyo, na maswahaba wakisoma Aya Aya, mmoja wao ni Anas bin Malik Anatuambia Mtume akiwafundisha hata kuvuta Bismillahi na kadhalika. ‘Abdallah bin Masuud amesema, “Kusoma haraka haraka ni mbaya bali ni usome pole pole, ipate kugonga ndani ya moyo, na usimame katika Aya za maajabu, igonge moyo”. Albara amesema: ‘Nimemsikia Mtume akisoma Wattini Wazzaytuni kwenye Swala ya Ishaa. Sijawahi kusikia sauti nzuri kama hiyo’. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Tengenezeni sauti zenu mnaposoma Qur’an]. Na hizo hadithi ni swahihi. Ni vizuri asome kwa sauti ya kuimbia ya kughani, imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Si katika sisi yule mtu atasoma Qur’aan na haghani]. Na kughani kwenyewe ni mume kwa sauti ya kiume na mke ajikaze, sio sauti kuwavutia wengine, na asome asimame kwenye mwisho wa kila Aya kama anavyotueleza mke wa Mtume Ummu Salama.
K usoma kwa kwa sauti ya chini
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alitufundisha, tusisome kwa sauti ya juu, mpaka tukawaudhi wengine. Kwa mfano, wengine wanaswali na majirani wamelala, soma kwa kiasi. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) anatuambia katika maana ya hadithi: “Nyote mtaitwa na mola wenu, msiudhiane wala msipandishiane sauti nyingi na kama mtu anasinzia aache kusoma alale, asije akasoma makosa makosa asijijue, na asiache sura zile fadhila zaidi kama suratul-Ikhlas, ambayo ni theluthi ya Qur’an. Na katika riwaya kadhaa Mtume amekuwa akisema: [Suratul-Ikhlas, ni theluthul ya Qur’an. na alikuwa akisoma Suratul Sajdah na Suratul Insaan katika Sala ya Alfajiri, na Tabaraka na Surat Al-Falaq na An-Nisa kabla ya kulala. Na vile vile akisoma Surat Al-Falaq na An-Nisa na Ayatul-Kursiyu baada ya kila swala].
Kukatazwa kusoma Qur’an katika rukuu na Sijida
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) mwenyewe ametukataza hilo kwenye hadithi swahihi akisema: [Enyi watu, hakukubakia kwenye bishara za mitume isipokua ndoto za watu wema, nami nimekatazwa kusoma Qur’an kwenye rukuu na sijida. Mtukuzeni Allah na mjitah idi kwa dua]. Na sababu yake ametaja Sheikhul-Islam, kukaa rukuu na sijida ni pahali pa kujidhalilisha Muislam kwa Mola wake.
Ewe Muislamu ulipoumbwa na ukaletwa hapa Duniani uliwekewa katiba na mfumo wa kuishi na njia ya kupita mwanzo mpaka mwisho, nzuri na mbaya, yote hayo utayapata kwenye Qur’an ukifundishwa na Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).
Kusoma Qur’an na Adabu zake
Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehema Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na kutakia radhi Maswahaba na waliokuja baada hao mpaka qiyama.
Ama baadu: mazungumzo yetu ni kuhusu kitabu ambacho ndio msingi wa kufaulu kwenu, chenye kuwatoa kwenye kitua, ndani yake kuna khabari ya waliokuja kabla yenu na watakaokuja baada yenu na hakimu kati yenu, chenye kupambanua baina ya haki na batili. Mwenye kukiacha ameumia, mwenye kutaka uongofu kwa hicho ataongoka, na mwenye kutaka kuongoza na kitabu kingine amepotea; ni kamba ya Allah ya kuaminika isiyokatika; ni utajo wa Mwenyezi Mungu ni njia iloyonyoka, mwenye kuifuata hapotei na mwenye kuifuata hachanganyikiwi. Hawashibi nayo wanavyuoni na maajabu yake hayapungui. Atakaye ukweli ataupata humo na mwenye kuhukumu nacho atahukumu kwa usawa. Matakwa ya Allah ni tuisome Qur’an ili atuongoza na atuingize peponi.
Enyi waumini, Someni Qur’an na muwasomeshe watoto wenu au wenzenu, muwe mumebebwa na mazingira yake, frikra zenu na mawazo yawe katika mazingira ya Qur’an, muwahifadhisha watoto wenu kwa udogoni, kwani mkifanya hivyo, inaifanya igande vizuri zaidi ndani ya nyoyo zao, kwani kuhifadhi udogoni ni kama kutia naqshi kwenye jiwe.
Ewe waja wa Mwenyezi Mungu, Muongopeni Mola na muwe na hamu na Kitabu hiki. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال الله عز وجل: (إنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنْفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَنْ تَبُورَ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ) [فاطر: 30]
{{Hakika wanaosoma hiki Kitabu cha Allah na wakasimamisha swala na wakatoa kwa mali yao tulizowapa kwa siri na dhahiri, wanatarajia biashara isiofilisika, na hakika Allah atawalipa awaongeze, kwani yeye mweyekusamehe saana na ni mwenye kushukuriwa}}. Na mke wa Mtume ‘Aisha akazidi kutufafanulia akisema: ‘Kusoma kwa Qur’an kunatafautiana, kuna anayesoma hodari. Hivyo, thawabu zake ni nyingi kiasi cha kutangamana na Malaika na anayesoma akigongagonga atapata malipo mara mbili. Vilevile Abi Umama akamwambia amemsikia Mtume akisema: [Someni Qur’an, itakufaa siku ya Qiyama kuwaombea shufaa. Haya yote ni fadhila za Qur’an na fadhila za kusoma Qur’an]. Na Mtume wetu (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alimuusia Abu Said akimwambia : [Nakuusia umche Mwenyezi Mungu, kwani hilo ndio kichwa cha kila kitu, na utoke kwenda Jihad kwani hilo ndio daraja kuu la Uislamu na umtaje Mwenyezi Mungu kwa wingi, na usome Qur’an ukifanya hivyo roho yako itakuwa mahali pazuri mbinguni na utakuwa na utajo upo ardhini].
Adabu za kusoma Qur’an
Kusoma kwa ajili ya Allah (Subhaanahu wa Taala)
Waja watalipwa kulingana na nia zao. Mtume anatutolea khabari kuwa watu watalipwa vibaya japokuwa tunawaona wakifanya mema, nao ni sampuli tatu:-
Mtu anajishughulisha na Qur’an kuisoma vizuri, kuikusanya n.k
Mtu aliyeuliwa jihad fi sabilillahi.
Mtu tajiri anaye toa sana.
Kumbe wote hawa watatu, wanafanya riya, Allah atamwambia msomaji Qur’an: Si nilikufundisha Qur’an? Atajibu: Ndio ewe Mola; baadaye ulifanya nini? atajibu nilikua nikiisoma usiku na mchana, Mwenyezi Mungu atasema: ‘Umesema urongo, na Malaika watazidi kumkaripia ‘muongo we, na watasema Ewe Mola: huyu bwana, alikuwa akisoma kwa ajili ya watu, na tukaachia watu wamlipe kule kule duniani. Mungu atawaamrisha Malaika wamtie motoni (Mwenyezi Mungu atulinde na hayo)
Kusoma hali akiwa na utwahara
Hapana shaka kuyasoma maneno ya Allah ukiwa msafi, ndio bora kama vile kupiga mswaki, kutawadha n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakika midomo yenu, ndiyo njia za kusoma Qur’an, isafisheni kwa miswaki]. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema tena: [Ikiwa mja anaswali, Malaika humjia, na wakamsimamia nyuma yake wakimsikiliza Qur’an na wanaendelea hivyo mpaka anyamaze]. Na je ikiwa mja kinywa chake chanuka? Malaika watakaa kando.
Kusoma kisawasawa
Mola wetu anatuamrisha kuisoma Qur’an na Mtume wetu anatushinikiza hivyo, na maswahaba wakisoma Aya Aya, mmoja wao ni Anas bin Malik Anatuambia Mtume akiwafundisha hata kuvuta Bismillahi na kadhalika. ‘Abdallah bin Masuud amesema, “Kusoma haraka haraka ni mbaya bali ni usome pole pole, ipate kugonga ndani ya moyo, na usimame katika Aya za maajabu, igonge moyo”. Albara amesema: ‘Nimemsikia Mtume akisoma Wattini Wazzaytuni kwenye Swala ya Ishaa. Sijawahi kusikia sauti nzuri kama hiyo’. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Tengenezeni sauti zenu mnaposoma Qur’an]. Na hizo hadithi ni swahihi. Ni vizuri asome kwa sauti ya kuimbia ya kughani, imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Si katika sisi yule mtu atasoma Qur’aan na haghani]. Na kughani kwenyewe ni mume kwa sauti ya kiume na mke ajikaze, sio sauti kuwavutia wengine, na asome asimame kwenye mwisho wa kila Aya kama anavyotueleza mke wa Mtume Ummu Salama.
K usoma kwa kwa sauti ya chini
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alitufundisha, tusisome kwa sauti ya juu, mpaka tukawaudhi wengine. Kwa mfano, wengine wanaswali na majirani wamelala, soma kwa kiasi. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) anatuambia katika maana ya hadithi: “Nyote mtaitwa na mola wenu, msiudhiane wala msipandishiane sauti nyingi na kama mtu anasinzia aache kusoma alale, asije akasoma makosa makosa asijijue, na asiache sura zile fadhila zaidi kama suratul-Ikhlas, ambayo ni theluthi ya Qur’an. Na katika riwaya kadhaa Mtume amekuwa akisema: [Suratul-Ikhlas, ni theluthul ya Qur’an. na alikuwa akisoma Suratul Sajdah na Suratul Insaan katika Sala ya Alfajiri, na Tabaraka na Surat Al-Falaq na An-Nisa kabla ya kulala. Na vile vile akisoma Surat Al-Falaq na An-Nisa na Ayatul-Kursiyu baada ya kila swala].
Kukatazwa kusoma Qur’an katika rukuu na Sijida
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) mwenyewe ametukataza hilo kwenye hadithi swahihi akisema: [Enyi watu, hakukubakia kwenye bishara za mitume isipokua ndoto za watu wema, nami nimekatazwa kusoma Qur’an kwenye rukuu na sijida. Mtukuzeni Allah na mjitah idi kwa dua]. Na sababu yake ametaja Sheikhul-Islam, kukaa rukuu na sijida ni pahali pa kujidhalilisha Muislam kwa Mola wake.

DALILI ZA KUKARIBIA KWA SIKU YA QIYAAMAH

Mwenyezi Mungu Amemleta Mtume wake Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akiwa kama ni mletaji habari njema na muonyaji ambaye hakuacha jambo lolote la kheri isipokuwa ametujuulisha nalo na kutuhimiza kulikimbilia, na hakuacha jambo lolote la shari isipokuwa ametutahadharisha nalo.


Na kwa vile Ummah huu ni Ummah wa mwisho, basi Mtume huyu mtukufu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ametuletea kutoka kwa Mola wake dalili za kutosha zilizo wazi, zenye kutujuulisha juu ya kukaribia kwa Siku ya Qiyaamah. Akatubainishia kwa ulimi wake, tena kwa ufasaha kabisa, juu ya baadhi ya yatakayotokea katika mwisho wa zama. Akatuhakikishia kuwa yote hayo lazima yatatokea, haya yote yakiwa ni dalili juu ya ukweli wa Utume wake (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) utakayowafanya watu wajitayarishe vizuri na Siku hiyo. Siku ambayo mtu hatovuna isipokuwa kile alichochuma, na hatokuwa na wakumlaumu isipokuwa nafsi yake.

Mwenyezi Mungu Anasema:

{{“Isije ikasema nafsi (asije akasema mtu); “Eee majuto yangu kwa yale niliyopunguza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaoyafanyia mzaha (mambo ya diyn)”.



Au ikasema; “Kama Mwenyezi Mungu angeniongoa bila shaka ningekuwa miongoni mwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu”.

Au ikasema ionapo adhabu; “Kama ningepata marejeo  (ya kurejea tena duniani) ningekuwa miongoni mwa wafanyao mema”.

(Ataambiwa) “Kwa yakini! Bila shaka zilikujia Aayah (dalili) zangu ukazikadhibisha na ukajivuna na ukawa miongoni mwa wanaotakabari”.}}

[Az-Zumar: 56-59]

Katika kuzijua dalili hizo kisha kuziona zikitendeka hapa duniani kunampatia mtu faida nyinigi sana zikiwemo zifuatazo:

·         Kuwa na uhakika juu ya ukweli wa Utume wake Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).
·         Kujitayarisha vizuri na Siku ya Qiyaamah. Kwani kwa mfano mtu   anapopewa habari juu ya meli inayokaribia kuwasili bandarini, huingoja        meli hiyo huku akiwa na wasi wasi mwingi. Lakini anapoisika sauti ya         selo ya meli hiyo, anakuwa na uhakika usio na shaka kuwa meli sasa   imekaribia kweli kuwasili.

Mfano huu ni sawa na mtu aliyejuulishwa juu ya dalili ya kukaribia kwa Siku ya Qiyaamah, kisha akaziona dalili hizo zikitendeka mbele ya macho yake kama zilivyoelezwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Mtu huyo anakuwa na uhakika usio na shaka wa kuwepo kwa siku ya Qiyaamah.

·         Kwa ajili hiyo, kuzijua na kuziona dalili za kukaribia kwa Siku ya    Qiyaamah kunaongeza pia yakini juu ya ukweli wa kukaribia kwa Siku hiyo.
·         Kunamsaidia mtu kutoyumbishwa na masaibu, mitihani na machafuko    yanayotekea kila siku. Kwani akirudi katika mafundisho ya Mtume wa      Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ataona kuwa yote hayo yamekwishatajwa kuwa yatakuja kutokea.
·         Kunamsaidia mtu aliyejisahau akawa anaikimbilia dunia, anapoziona       dalili hizo zikitokea kikweli humkumbusha mtu huyo akawa anaifanyia          kazi Akhera yake badala ya kuikimbilia dunia.

Kutokana na haya na mengi mengineyo, Mwenyezi Mungu Akamfunulia Mtume wake (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) baadhi ya dalili ya yale yatakayotokea kabla ya kuja kwa Siku ya Qiyaamah.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa anapozungumza juu ya dalili za kukaribia kwa Siku ya Qiyaamah, mashavu yake yanageuka kuwa mekundu huku akiipaza sauti yake juu kwa ghadhabu mfano wa Amiri Jeshi mwenye kulipa amri jeshi lake.

<iframe width="420" height="315" src="//www.youtube.com/embed/x8IOJ89vAGA" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>


Alikuwa pia akisema:

((“Nimeletwa baina yangu na Qiyaamah kiasi kama hiki”, huku akiashiria kwa kidole chake cha shahada na cha pili yake.))

Zipo dalili zinazoitwa ‘dalili ndogo’ na zipo pia ‘dalili kubwa’ za Siku ya Qiyaamah. Nyingi katika dalili ndogo zimekwisha tokea na kuonekana, jambo lililowafanya Waislamu waongezeke imani na kumsadiki zaidi Mtume wao (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Wakati zitakapoanza kuonekana dalili kubwa, basi zitatunga na kufuatana moja baada ya nyingine mpaka Qiyaamah kitakaposimama. Lakini sisi tutazitaja hapa baadhi yake na chache sana miongoni mwa ‘dalili ndogo’ tu.


Fitan

Neno ‘Fitan’ ambalo ni wingi wa (plural ya) Fitnah; maana yake ni Mitihani. Lakini neno hili linaongezeka maana yake kila linapozidi kutumika. Kwani neno hili linaweza kumaanisha misiba, madhambi, kufru, mauaji, kuchomwa moto n.k.

Neno ‘Fitan’ pia linamaanisha vita vya wenyewe kwa wenyewe (civil wars). Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ametujuulisha juu ya Fitnah nyingi sana zitakazotokea baada yake zikiwa kama ni dalili ya kukaribia kwa Siku ya Qiyaamah. Fitnah zitakazomfanya mtu asiweze kutambua ipi haki na ipi baatwil. Fitnah zitakazozitetemesha nyoyo na kuiyumbisha imani, hadi kufikia kwamba mtu anaweza akaamka asubuhi akiwa ni Muislamu na jioni yake akageuka kuwa kafiri, au anaweza kuamka asubuhi akiwa kafiri na jioni yake akawa Muislamu.
Kila inapotokea fitnah, mtu hudhani kuwa hii ndiyo itakayoangamiza, kisha humalizika na kutokea nyingine kubwa kuliko ile. Na hali itaendelea hivyo mpaka kitakaposimama Qiyaamah.

Anasema Abu Muusa Al-Ash’ary (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
((Kinapokaribia Qiyaamah zitatokea Fitnah nyingi mfano wa vipande vya usiku wenye kiza kizito, mtu ataamka ndani yake akiwa Muislamu na jioni yake anakuwa kafiri, au anakuwa wakati wa jioni Muislamu na asubuhi anakuwa kafiri. Aliyekaa katika mtihani huo anakuwa bora kuliko aliyesimama, na aliyesimama anakuwa bora kuliko mwenye kutembea taratibu, na mwenye kutembea anakuwa bora kuliko anayekwenda mwendo wa kukazana.)) [Imepokewa na Imaam Ahmad, Ibni Maajah, Al-Haakim na wengineo]

Imetolewa na Muslim pia kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Kimbilieni kufanya ‘amali njema kabla ya kuja kwa Fitnah mfano wa vipande vya usiku wenye kiza kizito, mtu ndani yake anaamka akiwa Muislamu na jioni yake anakuwa kafiri, au jioni anakuwa kafiri na asubuhi anakuwa Muislamu. Mtu ndani ya Fitnah hizo anaiuza diyn yake kwa thamani ndogo ya dunia.)) [Imepokewa na Muslim]

Na maana ya neno ‘vipande vya usiku wenye kiza kizito’, ni ule ubaya wa Fitnah hizo utakaomfanya mtu achanganyikiwe asiweze kutambua baina ya haki na baatwil.

Kutoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ‘Anha) amesema kuwa usiku mmoja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliamka akiwa na hofu nyingi huku akisema: ((Subhaana Llaah! Hazina ngapi alizoteremsha Mwenyezi Mungu, na mitihani mingapi aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu? Nani atakayewaamsha waliolala vyumbani mwao (akimaanisha wake zake), huenda mtu akawa amevaa duniani akaenda uchi Akhera.))

Maulamaa wamelitafsiri neno ‘amevaa duniani akaenda uchi Akhera’, tafsiri nyingi sana zikiwemo zifuatazo:

·         Mtu tajiri mwenye nguo nyingi hapa duniani lakini hana ‘amali njema za           kumsitiri huko Akhera.
·         Wengine wakasema kuwa maana yake ni mtu mwenye kuvaa nguo
zisizomsitiri hapa duniani na huko Akhera hatokuwa na cha kumsitiri.


Kuvunjwa Kwa Mlango

Nitaanza kwa kutaja baadhi ya Hadiyth alizozungumzia ndani yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) Fitnah za mwanzo katika Uislamu, Fitnah zilizotokea miaka michache baada ya kufariki kwake, mara baada ya kuuliwa kwa Khaliyfah wa pili wa Waislamu ‘Umar bin Khatwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu).

Kutoka kwa Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) amesema kuwa:
‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu) aliuliza siku moja: “Yupi kati yenu aliyehifadhi kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) juu ya Fitnah?”.

Hudhayfah akasema: “Mimi nimehifadhi kama alivyosema”.

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akamwambia: “Tuhadithie, kwani wewe ni jasiri”.

Hudhaifah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akasema: “Fitnah ya mtu katika ahli yake (watu wa nyumba yake) na mali yake na jirani zake zinaondoka kwa kuswali na kutoa Sadaka na kwa kuamrisha mema na kukataza mabaya”.

‘Umar akasema: “La, mimi sikusudii (fitnah) hizi, bali zile zinazorusha mawimbi (makubwa) kama mawimbi ya bahari”.

Akasema: “Ewe Amiri wa Waislamu! Wewe umeepukana nazo Fitnah hizo, kwani baina yako na baina yake (Fitnah hizo) upo mlango uliofungwa”.

‘Umar akauliza: “Mlango huo utafunguliwa au utavunjwa?”

Akasema: “La, bali utavunjwa”.

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akasema: “Kwa hivyo hautofungika tena...” Na katika riwaya nyingine akasema: “Kwa hivyo hautofungika mpaka Siku ya Qiyaamah?”

Wakamuuliza (waliokuwa wakimsikiliza Hudhayfah baada ya kufa kwa ‘Umar): “Aliujua?” Na katika riwaya nyingine: “’Umar alikuwa akiujua mlango huo?”.

Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akawaambia: “Naam kama (anavyojua kuwa) usiku wa leo unakuja kabla ya usiku wa kesho)”.

Masruuq bin Al Ajda-a alipomuuliza Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu): “Nani mlango huo”.

Akasema: “(Mlango huo ni) ‘Umar.”

Kisha Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akawaambia: “Mimi nilimuhadithia ‘Umar Hadiyth (hii) kama nilivyomsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) bila makosa.”

Ikawa kama alivyotujuulisha Msemakweli Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), kwani mlango huo ulivunjwa mara baada ya kuuliwa Khaliyfah wa pili wa Waislamu ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu). Kuanzia hapo Fitnah zikafunguka na kuenea na kukithiri, na Fitnah ya mwanzo ilikuwa kuuliwa kwa Khaliyfah wa tatu wa Kiislamu- Mwenye Nuru mbili ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu).

[Imepokewa na Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

Kuuliwa Kwa ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliwahi kumbashiria ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa atakumbwa na mtihani mkubwa.

Kisa chenyewe ni kama ifuatavyo:

Anasema Abu Muusa Al-Ash’ary (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa siku moja alimuona Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akielekea katika kisima kilichozungushiwa ukuta.

Abu Musa Al-Ash’ary anasema: “Nikasema: Leo mimi nitakuwa mlinzi wa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).” Nikamuona Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akielekea kisimani, akakidhi haja yake kisha akakaa juu ya kisima huku akining’iniza miguu yake.  

Akaja Abu Bakr akataka ruhusa ya kuingia ndani, nikamwambia: “Hapo hapo ulipo, ngoja kwanza usiingie mpaka nikakuombee ruhusa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)”. Nikamwendea Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na kumwambia: “Abu Bakr anataka ruhusa ya kuingia”, Akanambia: ((Mruhusu aingie, na mbashirie Pepo)). Nikafanya hivyo, akaingia na kukaa juu ya kisima kuliani kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na kuining’iniza miguu yake kama alivyofanya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).

Mlango ukagongwa tena. Nikatamani mgongaji awe ndugu yangu. Nikauliza: “Nani?”, “’Umar bin Al-Khattwaab”, Nikamwambia: “Hapo hapo ulipo, usiingie mpaka kwanza nimjulishe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)”. Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akanambia: ((Mruhusu aingie, na mbashirie Pepo)). Nikafanya hivyo, na ‘Umar naye akaingia na kukaa juu ya kisima kushotoni kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na kuining’iniza miguu yake kama walivyofanya wenzake.

Haujapita muda mlango ukagongwa tena: Nikatamani mgongaji awe ndugu yangu. “Nani?” “‘Uthmaan bin ‘Affaan”. Nikamwambia: “Hapo hapo ulipo, usiingie mpaka kwanza nimjulishe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)”. Nilipomjulisha, Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akanyamaza muda kidogo, kisha akanambia: ((Mruhusu aingie na mbashirie Pepo baada ya kupambana na mtihani mkubwa)). Nilipomwambia hivyo, ‘Uthmaan akasema: “Allaahul-Musta’an”, (na katika riwaya nyingine alisema: “Tutakuwa na subira In shaa Allaah”). Kisha akaingia, lakini ‘Uthmaan hakupata pa kukaa, akaenda upande wa pili akakaa akiwa amekabiliana nao.

Anasema Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘Anhu): “Nikahisi kama hivi ndivyo makaburi yao yatakavyokuwa, na nikatamani ndugu yangu naye aje”.
[Imepokewa na Al-Bukhaariy]

Ingawaje ‘Umar bin Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu) aliuliwa kama alivyouliwa ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu), lakini ‘Umar aliyeuliwa na kafiri anayeabudu moto wakati akiswalisha Swalah ya Alfajiri hakupata misukosuko kama aliyopata ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kabla ya kuuliwa kwake.

Baada ya kuuliwa ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) Fitnah zikawa nyingi, khitilafu zikaongezeka, hata Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) walishiriki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.


Mnayaona Ninayoyaona Mimi?

Siku moja alipokuwa akisimamia ujenzi wa ngome katika mji wa Madiynah, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliyekuwa akiyajuwa yote hayo kuwa yatatokea, aliwauliza Maswahaba wake: ((Mnaona ninayoyaona?))

Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘Anhum) wakasema: “Hatuoni (kitu) ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: ((Mimi naona mapigano mengi yakitokea baina ya nyumba zenu, wingi wa nyumba kubwa kubwa (zinazowakusanya watu wengi ndani yake).))


Fitnah Zitokazo Upande Wa Mashariki

Fitnah nyingi zilizowakumba Waislamu zilitokea upande wa Mashariki ya dunia, na Fitnah ya mwanzo iliyoleta mfarakano baina ya Waislamu ilitokea upande huo wa Mashariki, jambo ambalo bila shaka lilimfurahisha sana Shaytwaan. Na haya yanakubaliana na maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliyetujuulisha kuwa huko ndiko kwenye pembe ya Shaytwaan.

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema huku akiashiria upande wa Mashariki: ((Fitnah ipo huku, Fitnah ipo huku, kutakapotokeza pembe ya Shaytwaan.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Habari hizi alizotujuulisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) zilianza kuonekana tokea mwanzo wakati yalipotokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, jambo ambalo bila shaka yoyote lilimfurahisha sana Shaytwaan.

Anasema Shaykh Yuusuf bin ‘Abdillaah Al-Waabil kuwa: “Kutoka upande wa mashariki Fitnah nyingi sana zilitokea. Kwani huko ndiko yalipoanza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe baina ya Waislamu. Kutoka huko umekuja Ukadiani, Ukoministi. Matartar pia wametokea huko katika karne ya saba ya Hijriyyah, wakaangamiza na kueneza shari kubwa sana”.
“Hadi hii leo”, anaendela kusema Shaykh Yuusuf: “Fitnah zinaendelea kutujia kutokea upande huo wa Mashariki ya dunia na hata Yajuju na Majuju watatokea upande huo huo”.


Kupotea Kwa Amaanah

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Uaminifu utakapoondoka basi isubirini Sa’ah (kingojeeni Qiyaamah).)) Akaulizwa: “Vipi unapotea (uaminifu) ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?”
Akasema: ((Mambo yakiegemezwa kwa wasiostahiki, basi isubirini Sa’ah.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy, Kitaabur-Riqaaq]

Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akatubainishia pia kuwa uaminifu utatoweka katika nyoyo na kubaki athari yake tu.

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amenihadithia mambo mawili, na mojawapo katika hayo nimekwishaliona likitokea na ninalisubiri la pili (nilione pia). Amenihadithia kuwa uaminifu utatoweka. Amenihadithia kuwa amaanah (ilipoteremshwa), iliteremshwa ndani ya mizizi ya nyoyo za watu, kisha iilipoteremshwa Qur-aan wakaijua zaidi, kisha wakaijua (vizuri zaidi) kupitia katika Sunnah (Mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)).”

Kisha akatuhadithia juu ya kunyanyuliwa (kupotea) kwa amaanah akasema: ((Mtu analala usingizi huku amaanah inafutwa moyoni mwake na kubaki athari yake tu, mfano wa doa lisilokuwa na rangi. Kisha analala usingizi (mwingine) na amaanah inafutwa (‘tena’ - yaani hilo doa lililobaki). Kisha itabaki amaanah mfano wa alama (ya ngozi iliyokunjika) inayobaki mkononi baada ya mtu kunyanyua kitu”, (inayotoweka baada ya kupita muda mdogo) (au) maumivu yanayobaki mguuni baada ya kukanyaga kijinga kidogo cha moto (pakafanya lenge lenge kisha likakauka).))

Kisha Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: ((Kisha watu watakuwa wanafanya biashara na hapana hata mmoja kati yao atakayekuwa muaminifu, itafika hadi kusemwa; “Katika watu wa kabila Fulani yupo mtu mmoja muaminifu. Na hata itafika hadi watu watakuwa wakimsifia mtu huku wakisema: ‘Mwanamume kweli huyu, mkarimu kweli huyu, ana akili kweli huyu’, (atapewa sifa zote hizo) wakati mtu huyo hana imani (wala uaminifu) hata yenye uzito wa hardali.))

Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akaendela kusema: “Nimekwishaiona zama ambayo ndani yake uaminifu baina ya watu ulikuwepo. Na sikuwa nikijali ninafanya biashara na nani (kwa sababu watu wote waaminifu), akiwa mtu huyo ni Muislamu basi Uislamu wake utamfanya asiipoteze amaanah yake. Na kama mtu huyo ni Mkiristo au Myahudi, basi atakuwa anafanya kama anavyotakiwa (kutonidhulumu haki yangu). Ama wakati huu wa leo, uaminifu umeondoka, na khiyaanah imedhihiri na sitofanya biashara isipokuwa na fulani au fulani (tu)”.
Yaani alikuwa akifanya biashara na baadhi ya watu wachache tu alokuwa akiwaamini.

Hudhayfah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) aliishi muda baada ya kuuliwa kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu).
[Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Anasema Shaykh Yuusuf bin ‘Abdillaah Al-Waabil aliyeandika kitabu cha Ashraatwus-Sa’ah kuwa: “Miongoni mwa dalili za kupotea kwa amaanah ni kule kupewa ufalme, uongozi au uhakimu watu wasiokuwa waadilifu wala waaminifu. Kwani viongozi wanapotengenea, raia nao hutengenea. Ama huko juu kukiharibika, basi chini nako kutaharibika pia. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekwishatujuulisha kuwa utafika wakati wa hadaa, mambo yatakapokwenda kinyume. Wakati huo, muongo ndiye atakayesadikiwa na mkweli atakadhibishwa, na muaminifu ataitwa haini na haini ndiye atakayeaminiwa”.

Kubebeshwa mzigo wa uongozi watu wasioijali Dini yao, ni dalili ya watu kutojali maamrisho ya Dini yao. Na dalili ya upungufu wa Ma’ulamaa na kuongezeka kwa ujinga, na hizi pia ni katika dalili za kukaribia kwa Qiyaamah alizozitaja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Katika dalili za kukaribia kwa Qiyaamah ni kupotea kwa elimu na kuongezeka ujinga.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy]


Kushindana Na Kujisifia Katika Kuipamba Misikiti

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
((Katika dalili za kukaribia kwa Qiyaamah ni watu kushindana na kujisifia katika kuipamba misikiti.)) [Imepokewa na An-Nasaaiy]

Anasema Al-Bukhaariy: Amesema Anas (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa: “Watu wataipamba (Misikiti) lakini hawaendi kuswali ndani yake isipokuwa wachache”.

‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikataza watu kuipamba sana Misikiti kwa sababu mapambo yanawababaisha watu ndani ya Swalah zao. Alipokuwa akisimamia utengenezaji wa Msikiti wa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akiwaambia wajenzi:
“Wakingeni watu na mvua na msitie rangi nyekundu wala manjano mkawababaisha watu”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy]

“Mwenyezi Mungu Amrehemu ‘Umar bin Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu)”, anasema Shaykh Yuusuf Al-Waabil, “kwani watu hawakutoshelezeka na kuwakinga watu na mvua wala hawakutoshelezeka na rangi za manjano na nyekundu, bali Misikiti siku hizi inapambwa na kujazwa nakhshi mfano wa nguo inavyonakshiwa”.


Mauaji

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Qiyaamah hakitosimama mpaka ‘Haraj’ ikithiri.)) Wakamuuliza: “Ni nini hii ‘Haraj’ ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ((Mauaji, mauaji!.)) [Imepokewa na Muslim]

Na katika riwaya nyingine iliyosimuliwa na Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Kabla ya Qiyaamah kusimama kutatokea ‘Haraj’.)) Wakamuuliza: “Ni nini hii ‘Haraj’ ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ((Mauaji)). Wakamuuliza: “Kuliko tunavyoua? Tunaua (vitani) katika mwaka mmoja zaidi ya alfu sabini?” Akasema: ((Si kama kuuwa kwenu washirikina, bali huko ni kuuana nyinyi wenyewe kwa wenyewe.)) Wakasema: “Tutakuwa na akili zetu siku hiyo?” Akasema: ((Zitaondolewa akili za wengi wa watu wa zama hizo. Watakuwa na wafuasi wengi kama vumbi, wengi wao watadhani kuwa wameshika chochote (katika haki), lakini (ukweli ni kuwa) hawana chochote.)) [Imepokewa na Imaam Ahmad na Ibn Maajah]

Halikadhalika, imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurayrah kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, haitotoweka dunia mpaka iwajie watu siku ambayo ndani yake muuaji hatojua kwa ajili gani ameua na wala aliyeuliwa kwa ajili gani ameuliwa.)) Akaulizwa: “Yatakuwaje hayo?” Akasema: ((Al-Haraj! aliyeuwa na aliyeuliwa (wataingia) Motoni.))

Haya yote yashatokea kweli katika zama zilizopita na tunayaona yakitokea katika zama zetu hizi pia. Hasa baada ya kuvumbuliwa kwa silaha zinazoangamiza.

Na katika Hadiyth sahihi iliyomo katika Mustadrak ya Al-Haakim, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Ummah wangu ni Ummah utakaohurumiwa, hawatokuwa na adhabu huko Akhera, kwani adhabu zao ni za dunia, mauaji na mashaka na mitetemeko.))


Mtu Atatamani Kufa

Imepokelewa kuwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘Anhu) amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Hakitosimama Qiyaamah mpaka mtu atakapopita penye kaburi la mtu akasema: “Yareti mimi ndiye ningelikuwa mahali pake”.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy]

Na kutoka kwa Abu Hurayrah pia, kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, dunia haitotoweka mpaka mtu atakapopita penye kaburi akasimama na kusema: ‘Yareti ningelikuwa mimi ndani ya kaburi hili”. Si kwa ajili ya Dini, bali kwa ajili ya mitihani.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy]

Amesema Ibni Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘Anhu): “Utakupitikieni wakati, mtu akiyakuta mauti yanauzwa, basi atayanunua”.

Wanasema Ma’ulamaa kuwa mambo kama haya si lazima yatokee katika kila nchi. Lakini yanaweza kutokea katika zama mbali mbali kutokana na mitihani mizito mbali mbali. Mtu anapokumbwa na mitihani hiyo atakapopita makaburini atahisi kama kwamba yule aliyelala ndani mule ndiye aliyestarehe. Ama yeye anajiona yumo katika adhabu, misukosuko mashaka na mitihani mikubwa isiyomalizika.


Kupigana Na Warumi (Wakiristo)

Kutoka kwa ‘Awf bin Maalik Al-Ashjaiy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Hesabu mambo sita, lazima yatatokea kabla ya kusimama Qiyaamah, miongoni mwa mambo sita hayo akasema: Kisha vita vitasimamishwa baina yenu na watu wa manjano (Wakiristo), kisha watakufanyieni khiana, watakujieni chini ya bendera themanini, chini ya kila bendera (watu) elfu kumi na mbili.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy]

Siku moja alikuja mtu kwa ‘Abdullaah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akamwambia: “Ewe ‘Abdullaah! Qiyaamah kitasimama (karibu sana)”. ‘Abdullaah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘Anhu) aliyekuwa amekaa akiwa ameegemea, akakaa vizuri kisha akamwambia: “Hakika ya Qiyaamah hakitosimama mpaka kwanza mirathi isigawiwe na ngawira isifurahiwe”.

Kisha akasema huku akiashiria upande wa Shaam (upande wa Mashariki): “Maadui watajikusanya kuwapiga vita Waislam, na Waislam watajikusanya kwa ajili ya kupambana nao”. Nikamuuliza: “Warumi? (Wakristo?)” Akasema: “Ndiyo, na katika vita hivyo wengi watartaddi, na Waislamu watatayarisha jeshi litakalokuwa tayari kufa lisilokubali kurudi nyuma bila ushindi, watapigana vita mpaka usiku utakapoingia, kisha watarudi nyuma hawa na wale, hapana mshindi kati yao, kisha jeshi litaangamia. Kisha Waislamu watatanguliza jeshi (lingine) litakalokuwa tayari kufa, watapigana vita mpaka wakati wa jioni, kisha watarudi nyuma hawa na wale, hapana mshindi kati yao, kisha litaangamia jeshi. Itakapoingia siku ya nne, Waislamu waliobaki watakuja kuwasaidia, na Mwenyezi Mungu Atawajaalia ushindi uwe upande wao, watapigana vita visivyopata kuonekana namna yake, hata ndege akipita juu yao, basi ataanguka akiwa amekufa”. [Imepokewa na Muslim]


Kuja Kwa Qahtwaaniy

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Hakitosimama Qiyaamah mpaka kwanza aje mtu kutoka kabila la Qahtwaan (kabila la watu wa Yemen), atawaongoza watu kwa bakora (yaani atawaongoza na wataongoka vizuri na wote watampenda).)) [Imepokewa na Imaam Ahmad, Al-Bukhaariy na Muslim]

Imetayarishwa na Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Powered by Blog - Designer