
Mchungaji mmoja nchini Nigeria sanjari na kuligeuza kanisa lake kuwa
msikiti, ametamka shahada mbili na kuwa mfuasi wa dini Tukufu ya
Kiislamu.
Adekunle Afolabi ambaye amesilimu na kuwa Mwislamu anasema
kuwa, amechukua uamzi huo baada ya kuota ndoto ya maajabu wakati
alipokuwa katika maandalizi ya kufanya sherehe za kila mwaka za tangu
kuasisiwa kanisa lake hilo lililokuwa likiitwa Apata Adura Cherubim
katika mji wa Ado Ekiti...