Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) alimuuliza Mtume (Swalla Llahu alayhi wa allam):
"Sababu gani inayoingiza zaidi watu Peponi?"
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:
"Ucha Mungu na Tabia njema".
Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) amesema:
"Mtume wenu Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa Akizungumza taratibu huku akifikiri (kabla hajasema), lakini nyinyi mnasema maneno mengi sana...