Sunday, April 10, 2016

UCHA MUNGU NA TABIA NJEMA.

Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) alimuuliza Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa allam):
"Sababu gani inayoingiza zaidi watu Peponi?"
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:
"Ucha Mungu na Tabia njema".
Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) amesema:
"Mtume wenu Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa
Akizungumza taratibu huku akifikiri (kabla hajasema), lakini nyinyi
mnasema maneno mengi sana".

Sehemu ya mwanzo ya hadithi hii imetolewa na Bukhari
Kumbukeni kuwa kila mtu anao Malaika waliopewa kazi ya kuandika kila
Neno tunalotamka, kwa hivyo tusitamke isipokuwa tu yale ya kheri.
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwauliza Masahaba wake watukufu
(Radhiya Llahu anhum):
"Mnamjuwa ni yupi aliyefilisika?"
Masahaba (Radhiya Llahu anhum) wakajibu:
"Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaojuwa zaidi".
Na katika riwaya nyingine Masahaba walijibu:
"Aliyefilisika ni yule aliyekula hasara katika mali yake".
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akajibu:
"Hakika aliyefilisika kikweli katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya
Kiama akiwa na (thawabu nyingi alizozichuma kutokana na) Swala zake na
Funga yake na Zaka yake, analetwa (mbele ya Mwenyezi Mungu akishtakiwa)
Akiwa amemtukana huyu, amemsingizia uwongo huyu, amekula mali ya huyu,
Amemwaga damu ya huyu akampiga huyu, kisha zinachukuliwa thawabu zake
na kupewa huyu na yule na zikimalizika thawabu zake kabla ya kumaliza deni lake,
zinachukuliwa dhambi zao na kubebeshwa nazo yeye, kisha anaingizwa nazo moja
kwa moja Motoni".
Hadith hii imepokewa na Muslim na Attirmidhiy....

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer