Friday, March 4, 2016

AINA MBALIMBALI ZA SADAKA.



Mwenyezi Mungu S.W.T. hakujaalia sadaka za kujipatia malipo mema kwa kutoa mali au fedha tu. Kwani si watu wote hapa duniani ni matajiri wenye kuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Ndio maana Mtume .S.A.W. hakuwakatisha tamaa wala kuwavunja moyo watu mafakiri bali amewapa moyo wa kufanya vitendo fulani kuwa ni aina za sadaka za kujipatia malipo mema ya kesho Akhera. Kama ilivyotubainishia Hadithi iliyotolewa na Muslim na kupokelewa na Abu Dharr R.A.A. kasema: Baadhi ya Masahaba walimwambia Mtume S.A.W., “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wenye mali wameondoka na fungu kubwa (la thawabu), wanasali kama sisi, wanafunga kama sisi, na wanatoa sadaka ya ziyada ya mali zao. Mtume .S.A.W. akasema kuwajibu, “
"أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ؟ إنَّ بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَة.ً" قَالُوا: "يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ: "أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ“.
Maana yake, “Jee, Mwenyezi Mungu hakukufanyieni vya kutoa sadaka? Hakika kila Tasbihi (Subhaana Llaah) ni sadaka, na kila Takbiri (Allaahu Akbar) ni sadaka, na kila Tahmidi (Alhamdu Lillaah) ni sadaka, na kila Tahlili (Laa ilaaha illa Llaah) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza mabaya ni sadaka na katika kuwaingilia (wake zenu) kila mmoja katika nyinyi ni sadaka. Wakasema (Masahaba): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Jee, mtu anapojitosheleza shahawa yake atapata malipo kwa ajili yake? Akasema (Mtume S.A.W.): Jee, mnaona angekuwa anajitosheleza kwa njia ya haramu si angelipata dhambi? Na hivi ndivyo ilivyo ikiwa kafanya kwa njia ya halali basi atapata thawabu.”
Na pia katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari na Muslim na kupokelewa na Abu Huraira R.A.A. kasema, “Mtume S.A.W. kasema, “
"كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ، كُلُّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَيْنَ اثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وتُعينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْها أو تَرْفَعُ لهُ عَلَيْها متَاَعَهُ صَدَقَةٌ، والْكَلِمةُ الطَّيِّبةُ صَدَقَةٌ، وبكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيها إلى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ، وتُمِيطُ الأَذَى عنِ الطَّرِيِق صَدَقَةٌ".
Maana yake, “Kila kiungo cha mtu lazima kitolewe sadaka kila siku jua linapochomoza, kufanya haki (uadilifu) baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu kupanda (mnyama) kwa kumsaidia kumnyanyua au kumnyanyulia mizigo yake ni sadaka, neno jema ni sadaka, kila hatua unayokwenda (Msikitini) kusali ni sadaka na kuondosha dhara katika njia ni sadaka.”

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer