Friday, March 4, 2016

JE INAFAA KUMSOMEA KHITMAH MAYYIT.



kusoma khitmah ni jambo ambalo linatendeka katika jamii nyingi za Kiislamu kwa kudhani kwamba ni jambo linalofaa bila ya kuwa dalili yoyote. Na lengo linalokusudiwa la kusoma khitmah ni kuwa thawabu za kusoma Qur-aan zimfikie maiti wakati Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema kuwa hii Qur-aan imeletwa kwa ajili ya kumlingania binaadamu aliye hai na siye alikwishafariki:
((وَمَا عَلَّمْنَاهُ الشِّعْرَ وَمَا يَنبَغِي لَهُ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْآنٌ مُّبِينٌ))
((لِيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا ....))
“Wala Hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur-aan inayobainisha”
“Ili imwonye aliye hai…” [Yaasiyn: 69-70]

Binaadamu akishafariki, ‘amali zake zote huwa zimekatika ila kwa mambo matatu yaliyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث, صدقة جارية , أو علم ينتفع به, أو ولدٌ صالح يدعوا له)) مسلم
“Anapokufa mja hukatika ‘amali zake zote isipokuwa mambo matatu, Swadaqah inayoendelea, au elimu yenye manufaa kwayo, au mtoto mwema anayemuombea” [Muslim]

Hayo ndiyo mambo yanayomnufaisha maiti ikiwa atayaacha duniani. Na zifuatazo ni Du’aa katika Qur’aan na Sunnah ambazo mtoto anaweza kumuomba mzazi wake, na nyinginezo pia anaweza maiti kuombewana waislam wenzake:
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَاب
Rabbana-ghfir liy waliwaalidayya walil Mu-uminiyna yawma yaquumul hisaab.
“Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu”(Ibraahiym: 41)

رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا
Rabbir-hamhumaa kamaa rabbayaaniy swaghiyraa.
“Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni.” (Al-Israa: 24)

رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالإِيمَانِ وَلاَ تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ
Rabbanaghfir lanaa wa liikhwaaninal-ladhiyna sabaquunaa bil Iymaani wa laa Taj’al fiy quluubinaa ghillal-lilladhiyna aamanuu Rabbannaa Innaka Rauufur-Rahiym.
“Mola wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Iymaan, wala Usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.” (Al-Hashr: 10)

رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ
Rabbighfir liy waliwaalidayya
“Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu.” (Nuuh: 28)

Vile vile unaweza kusema:
اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِلْمُؤمِنِينَ وَاْلمُؤمِنات وَالْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمات اَلأَحْيَاءِ مِنْهُمْ وَالأَمْوَات
Allaahumma-Ghfir lil-Muuminiyna wal-Muuminaat wal-Muslimiyna wal-Muslimaat, al-ahyaai minhum wal-amwaat
Ewe Mwenyezi Mungu Waghufurie Waumini wanaume na Waumini wanawake, Na Waislamu Wanaume na Waislamu wanawake, Waliohai miongoni mwao na waliokufa.

Na hii ni Du’aa iliyothibiti katika Sunnah ya kumuombea maiti anaposwaliwa au hata wakati wowote mwingine unaweza kumuombea.

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه ، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه ، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه ، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه ، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما نَـقّيْتَ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه ، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه ، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه، وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة ، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir-lahu war-ham-huu, wa 'Aafihi wa'afu 'anhu, wakrim nuzulahu, wa-Wassi' mudkhalahu, wa-Ghsil-hu bil-maai wath-thalji wal-Barad, wa Naqqihi minal-khatwaaya kamaa Naqqayta-th-thawabal-abyadhw Minad-danas, wa-Abdil-hu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wa zawjan khayran min zawjihi, wa-Adkhil-huul-Jannata, wa A'idh-hu min 'adhaabil-Qabr wa 'adhaabin-Naar
“Ee Mwenyezi Mungu Msamehe na Umrehemu na Umuafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Upanue kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama Unavyoitakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Peponi na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).

Vile vile kumtolea Swadaqah na kumwendea Hajj au 'Umrah ikiwa hakuwahi kufanya hivyo wakati wa uhai wake.
NA Allah anajua zaidi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer