Friday, March 4, 2016
Home »
» KATIKA DINI MTAZAME ALIYE JUU YAKO – KATIKA DUNIA MTAZAME ALIYE CHINI YAKO.
KATIKA DINI MTAZAME ALIYE JUU YAKO – KATIKA DUNIA MTAZAME ALIYE CHINI YAKO.
Abdurazak Ngowo 2:11 PM
Katika Dini Mtazame Aliye Juu Yako – Katika Dunia Mtazame Aliye Chini Yako
Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
“Na wala usikodolee
macho yako kwa yale Tuliyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwani hayo ni mapambo ya uhai wa dunia tu ili Tuwafitinishe kwavyo. Na riziki ya Mola wako ni bora zaidi na ni yenye kubakia.” (20:131)
Usiikodolee macho dunia, ukataka kuwapokonya wenye nayo na ukatamani kupata mfano wa walionayo.
Kuhusu dunia mtazame yule aliye chini yako. Kuhusu Dini mtazame yule aliye juu yako ili uweze kushindana naye. Dunia mtazame yule aliye chini yako ili upate kuona neema za Allaah juu yako. Kuna watu wako chini katika maisha haya ya dunia, sawa inapokuja katika mali, siha, afya na nyumba. Utapowatazama watu hawa [na ukaona tofauti kubwa kati yako wewe na wao], basi zikumbuke neema za Allaah juu yako na uziadhimishe na kuzishukuru.
Related Posts:
Mashindano ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar Masjid Afraa Bint Issa -Kidongochekundu Zanzibar. Mwanafunzi kutoka Zanzibar, Nassir Rashid Seif (15) akishiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur-an Juzuu 30 Tashjii akiwa ameshinda nafasi ya Pili kwa kupata Alama 98.Mwanafunzi kutoka Zanzibar Masoud Khamis Sultan… Read More
'ARAFAH ITAKUWA JUMAPILI (11.09.2016) NA 'IYD AL-ADHW-HAA NI JUMATATU (12.09.2016M) Tunapenda kuwajulisha kuwa tarehe 1 Dhul-Hijjah itakuwa ni Jumamosi 03.09.2016. Vilevile tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kufunga siku ya 'Arafah ambayo itakuwa siku ya Jumapili tarehe 9 Dhul… Read More
UCHA MUNGU NA TABIA NJEMA. Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) alimuuliza Mtume (Swalla Llahu alayhi wa allam): "Sababu gani inayoingiza zaidi watu Peponi?" Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema: "Ucha Mungu na Tabia njema". Bibi Aisha (Rad… Read More
SIKU KUMI BORA KABISA ZA ALLAAH - 01 - 10 DHUL-HIJJAH. Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo vitendo vyake vyema huwa na thawabu nyingi sana. Na hivi tunakaribia kabisa… Read More
TAHIYYATUL MASJID NA SUNNATUL UDHUI TAHIYYATUL MASJID Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Yeyote miongoni mwenu atakapoingia Msikitini, hapaswi kukaa mpaka aswali rakaa mbili.” [Al-Bukhaariy na Muslim] Jaabir (Radhiya Allaahu '… Read More
0 comments:
Post a Comment