Saturday, January 7, 2017

ADABU ZA NDOA KATIKA SUNNAH ILIYOTAKASIKA.

Darsa :01
( UTANGULIZI WA DARSA LETU )
Sifa zote zamstahiki Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Ambaye Amesema katika aayah iliyo wazi kwenye Kitabu Chake:
(( ﻭَﻣِﻦْ ﺁﻳَﺎﺗِﻪِ ﺃَﻥْ ﺧَﻠَﻖَ ﻟَﻜُﻢ ﻣِّﻦْ ﺃَﻧﻔُﺴِﻜُﻢْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟًﺎ ﻟِّﺘَﺴْﻜُﻨُﻮﺍ ﺇِﻟَﻴْﻬَﺎ ﻭَﺟَﻌَﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢ ﻣَّﻮَﺩَّﺓً ﻭَﺭَﺣْﻤَﺔً ﺇِﻥَّ ﻓِﻲ ﺫَﻟِﻚَ ﻟَﺂﻳَﺎﺕٍ ﻟِّﻘَﻮْﻡٍ ﻳَﺘَﻔَﻜَّﺮُﻭﻥَ ))
((Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri))
(Ar-Ruum 30: 21).
Na Swalah na Salaam zimwendee kipenzi Chake Muhammad ambaye amesema katika Hadiyth Swahiyh:
(( ﺗَﺰَﻭَّﺟُﻮﺍ ﺍﻟْﻮَﺩُﻭﺩَ ﺍﻟْﻮَﻟُﻮﺩَ ﻓَﺈِﻧﻲ ﻣُﻜَﺎﺛِﺮٌ ﺑِﻜُﻢُ ﺍﻷَﻧْﺒِﻴَﺎﺀَ ﻳَﻮْﻡَ ﺍﻟْﻘِﻴَﺎﻣَﺔِ ))
((Oeni wapenzi wazaao, kwani nitashindana na Mitume wengine kwa idadi ya wafuasi siku ya Qiyaamah)).
Ahmad na At-Twabaraaniy kwa
isnaad iliyo hasan, na Ibn Hibbaan amekiri kuwa ni Swahiyh kutoka kwa Anas.
BAADA YA UTANGULIZI HUU:
Katika Uislamu kuna desturi na taratibu ambazo zatakikana kufuatwa na za mtu anayeoa au anayetaka kufunga ndoa.
Waislamu wengi leo hata wale ambao wanajitahidi katika ibada mbali mbali, hawajui kabisa hizi desturi za Kiislamu.
Kwa hiyo, nimeamua kuandika makala hii ndefu yenye faida kwa kuelezea wazi mambo haya katika mnasaba wa harusi ya mtu ambaye ni kipenzi changu.
Natumai kuwa itamsaidia yeye na ndugu wengineo waumini katika kumfuata Bwana wa Mitume alivyotuamrisha kutokana na amri ya Mola Wa Ulimwengu.
Baada ya hapo nimetahadharisha kuhusu baadhi ya mas-ala muhimu kwa kila anayeoa, na ambayo yamekuwa ni mitihani kwa wake wengi.
Namuomba Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Ajaaliye kitabu hiki kiwe ni chenye manufaa na Ajaaliye kazi hii iwe ya ikhlaas yenye kumridhisha Yeye Pekee kwani Yeye Ndiye Mwema na Rahiym.
Ifahamike kwamba kuna desturi nyingi katika sherehe za ndoa, lakini yaliyonishughulisha zaidi katika uandishi huu wa haraka, ni yale mambo yaliyo Sahihi katika Sunnah za Mtume ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ Muhammad ambayo hayawezi kukanushwa kutokana na msimamo maalumu wa mfululizo wa usimulizi (sanad) ambao hauna shaka katika muundo wake na maana yake.
Hivyo yeyote atakayesoma na kufuata maelezo haya atakuwa katika msingi uliothibiti wa Dini yake na atakuwa katika hali ya matumaini ya uhalali wa vitendo vyake.
Namuomba Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Amkhitimishe kwa furaha na thawaab kwa kuanza maisha yake ya ndoa kwa kufuata Sunnah na Amjaaliye miongoni mwa waja Wake Aliyewaelezea katika kauli Yake:
(( ﻭَﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻳَﻘُﻮﻟُﻮﻥَ ﺭَﺑَّﻨَﺎ ﻫَﺐْ ﻟَﻨَﺎ ﻣِﻦْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟِﻨَﺎ ﻭَﺫُﺭِّﻳَّﺎﺗِﻨَﺎ ﻗُﺮَّﺓَ ﺃَﻋْﻴُﻦٍ ﻭَﺍﺟْﻌَﻠْﻨَﺎ ﻟِﻠْﻤُﺘَّﻘِﻴﻦَ ﺇِﻣَﺎﻣًﺎ ))
((Na wale wanaosema: Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho, na Utujaalie tuwe waongozi kwa wachaji Allaah))
(Al-Furqaan 25: 74)
Na mwisho mwema ni wa waja wanaomcha Allaah kama Anavyosema Mola wa Ulimwengu:
(( ﺇِﻥَّ ﺍﻟْﻤُﺘَّﻘِﻴﻦَ ﻓِﻲ ﻇِﻠَﺎﻝٍ ﻭَﻋُﻴُﻮﻥٍ ﴿ 41 ﴾ ﻭَﻓَﻮَﺍﻛِﻪَ ﻣِﻤَّﺎ ﻳَﺸْﺘَﻬُﻮﻥَ ﴿42 ﴾ ﻛُﻠُﻮﺍ ﻭَﺍﺷْﺮَﺑُﻮﺍ ﻫَﻨِﻴﺌًﺎ ﺑِﻤَﺎ ﻛُﻨﺘُﻢْ ﺗَﻌْﻤَﻠُﻮﻥَ ﴿43 ﴾ ﺇِﻧَّﺎ ﻛَﺬَﻟِﻚَ ﻧَﺠْﺰِﻱ ﺍﻟْﻤُﺤْﺴِﻨﻴﻦَ ))
((Hakika wachaji Allaah watakuwa katika vivuli na chemchem. Na matunda wanayoyapenda. Kuleni na
kunyweni kwa furaha kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. Hakika ndio kama hivyo Tunavyowalipa watendao mema))
(Al-Mursalaat 77: 41-44).
Adabu na desturi hizo ni darsa letu lajao In Shaa Allaah.
Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Wabillaahi Tawfiyq.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer