Imewekwa na yusouf
-Anza kwa
kuzingatia mwezi huu mtukufu uwe wa kujihesabu, kutenda amali nyingi na
kujirekebisha hali yako na uhusiano wako na Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) uwe bora zaidi:
- Kumbuka
kwamba huu mwezi ni mgeni ambaye amekutembelea kisha ataondoka, hivyo
mpokee mgeni wako na mkirimu kwa mazuri yote anayostahiki.
-Tahadhari
na kutokufunga bila ya sababu au udhuru wowote, kwani kufanya hivyo,
Swawm yako haitolipika hata ukifunga mwaka mzima.
-Swali
kwa wakati wake, usiache Swalah ikakupita. Na jua kuwa ukiwa huswali
Ramadhaan huna Swawm kwa mujibu wa fatw za Maulamaa wengi.
-Soma sana
Qur-aan kadiri uwezavyo kwani ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan. Kamilisha
msahafu mzima japo mara moja, ukishindwa basi hata nusu yake, robo
yake.
-Zidisha ibada za Sunnah, kama Sunnah zilizo Muakkadah (zilizosisitizwa) na zile Ghayri Muakkadah (zisizosisitizwa). Tazama ratiba katika kiungo kifuatacho:
-Chukua fursa kuomba du'aa sana
kila mara nyakati za kukubaliwa du'aa, khaswa ukiwa bado katika Swaum.
Tumia wakati wa baina ya adhana na iqaamah kuomba du'aa na haja zako
kwani ni wakati wa kukubaliwa du'aa. Vile vile nyakati za thuluthi ya
mwisho ya usiku.
-Iborishe Swalah yako kwa kuiswali ipasavyo na kuzidisha khushuu (unyenyekevu).
-Usiache kuswali Taarawiyh pamoja na jama‘ah, usiondoke hadi Imaam amalize
-Tahadhari na kufanya israaf ya mali, chakula na neema nyinginezo, kwani israaf ni mbaya na itakuondoshea neema ulizojaaliwa.
- Tumia wakati wako vizuri na zingatia kwamba umri wako unazidi kupunguka.
-Mwezi huu ni wa ibada na sio kula, kulala na kufanya ya upuuzi.
-Zoesha ulimi wako uwe umerutubika kwa kumtaja Mola wako, usiwe miongoni mwa wasiomkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ila kidogo tu.
-Chukua
fursa kufanya da‘awah. Amrisha mema na kataza maovu, kwani yule
unayemuongoza atakapotekeleza mema, utazibeba nawe thawabu zake pia.
Tuma ujumbe wa dini kwa wenzako. Chapisha idadi nyingi ya makala zenye
mafunzo ya dini, chapisha du'aa ugawe misikitini, vyuoni, majumbani.
-Fanya kila aina ya wema uwezavyo, patanisha waliokhasimiana, msaidie mwenye haja na muokoe mwenye shida.
-Wakumbuke
wazazi, ndugu, jamaa na marafiki katika du'aa zako kwani kuwaombea wao
bila ya wao kujua Malaika hukuombea na wewe vile vile.
-Wasiliana na ndugu, jamaa kwani ni jambo lililosisitizwa sana na lenye kukuongeza umri, kheri na baraka nyingi. Walio mbali na wewe wasiliana nao kwa simu.
-Unapohisi njaa, wafikirie masikini wasio na uwezo wa kula, na utambue kuwa uko katika neema ya Mola wako.
-Muombe msamaha uliyemdhulumu kabla hajalipwa mema yako.
-Mfuturishe aliyefunga upate thawabu zake juu ya thawabu zako.
-Omba maghfirah na msamaha kwa Mola wako, kwani tambua kwamba Yeye ni Mwingi wa Msamaha na Mwingi wa Rahma.
-Ikiwa
umetenda maasi kisha Akakusitiri Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), tambua
kuwa hiyo ni onyo utubie na weka azma kutokurudia tena.
- elimu ya dini yako kwa kujifunza tafsiyr ya Qur-aan, Hadiyth, Fiqhi n.k. upate kuongeza taqwa.
-Sikiiza mawaidha japo moja kwa siku kwani kusikiliza kunaleta taathira kubwa ya kuongeza Imaan na Ucha Mungu.
-Jiepushe na marafiki waovu na vikao vyao na ungamana na marafiki wema na vikao vya kheri.
-Usipoteze
muda wako kutazama televisheni vipindi visivyokupa faida na dini yako,
bali tumia wakati wako kwa yatakayokuongezea elimu na ucha Mungu.
-Usiharibu
Swaum yako kwa kunena ya upuuzi, au Ghiybah (kusengenya), au kubishana
au kupandisha sauti. Jizuie unapokuwa na hamaki.
-Fika msikitini mapema zaidi, kwani hivyo ni dalili ya hamu na mapenzi ya ibada na kuwa karibu na Mola wako
-Waamrishe na kuwafunza mema ya dini yao walio katika majukumu yako; mke, mume, watoto, ndugu, jamaa n.k. kwani wako karibu yako zaidi na kukutii.
-Usijaze tumbo sana
katika suhuur (daku) kwani itakufanya uwe mvivu na ushindwe kukaa macho
nyakati za asubuhi na mchana na ushindwe kufanya ibada vizuri na kusoma
sana Qur-aan.
-Usijaze tumbo sana katika iftwaar (kufuturu) kwani itakushinda kusimama Qiyaamul-Layl au kuzingatia Aayah za Qur-aan zinaposomwa na Imaam.
-Tilia hima kubwa kuswali Qiyaamul-Layl kumi la mwisho upate Laylatul-Qadr, usiku ambao ibada yake ni bora kuliko miezi elfu.
-Jitahidi
ufanye I'tikaaf msikitini katika kumi la mwisho japo siku chache, upate
fadhila zake na uchume mema mengi pamoja na kupata Laylatul-Qadr.
-Tambua kwamba siku ya 'Idd ni siku ya kumshukuru Mola wako na sio siku ya kutenda yale uliyojizuia ya maovu katika Ramadhaan.
-Siku ya 'Idd , wafanyie wema wazazi, watembelee ndugu, jamaa na marafiki kuboresha uhusiano wako nao.
-Usiache
kutoa Zakatul-Fitwr - wakumbuke maskini, yatima na wanaohitaji na
wasaidie na kuwagawia chochote wabakie katika furaha.
-Tamka
Takbiyrah siku ya 'Idd kwa sauti unapokwenda msikitini ili kuwakumbusha
wengine wanaokwenda au kufuatana nawe ili nawe waweze kupiga Takbiyrah
hizo.
-Weka
azma baada ya Ramadhaan kujiendeleza katika hali ya ibada uliyokuwa
nayo katika Ramadhaan, ukifanya hivyo itakuwa ni dalili ya kukubaliwa funga yako.
- Funga Sita Shawwaal upate thawabu za Swaum ya mwaka mzima
0 comments:
Post a Comment