Imeandaliwa na Ummu 'Abdil-Wahhaab na kuwekwa na yusouf sanga
Shukrani zote ni za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
Ni
katika baraka zake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa Muislamu
Kumuwezesha kufunga mwezi wa Ramadhani na kuutumia wakati wake wa usiku
kwa Swalah. Ni mwezi ambao ndani yake amali njema huzidishwa malipo na
watu hupandishwa daraja (vyeo). Ni wakati ambao Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) Huwaachia huru baadhi ya watu kutokana na Moto. Kwa hivyo
Muislamu ni lazima ajitahidi sana
kufanya mambo mema katika mwezi huu; ni lazima afanye hima katika
kuutumia wakati wa uhai wake wenye ibada. Kuna watu wangapi ambao
wamenyimika katika mwezi huu kutokana na maradhi, mauti au kukosa
maelekezo mema.
Muislamu
ni lazima ajitahidi sana (kufanya matendo mema) katika wakati wake wote
ndani ya mwezi huu; anayo majukumu yasiyoweza kuepukika juu ya watoto
wake, kuwalea vizuri na kuwatunza vyema, kuwahimiza kufanya kila aina
ya vitendo vyema na kuwafanya waendelee kukuwa navyo – kwa sababu mtoto
hukulia katika mwenendo ambao wazazi wake wamemzoeza.
Katika
wakati wa siku hizi zilizobarikiwa, baba na mama wana nafasi adhimu ya
kufanya yenye manufaa, na tunaweza kutoa ushauri ufuatao kwa wazazi:
1 - Kuzifuatilia Swawm za watoto wao na kuwapa moyo wale wanaoshindwa kufanikisha.
2
- Kuwahimiza kuhusu Swawm halisi inavyotakiwa, na sio tu kujizuilia
kula na kunywa, lakini ni njia ya kufikia kwenye Kumcha Mwenyezi Mungu
(Taqwa), na hiyo ni nafasi maalumu ya kusamehewa madhambi na kulipwa
malipo mema.
Imesimuliwa
kutokana na Abu Hurayrah kwamba Mjumbe wa Allaah (Rehma na Amani
Zimshukiye Juu Yake) alishuka kutoka juu ya minbar na akasema : “Aamiyn,
Aamiyn, Aamiyn.” Akaulizwa, “Ewe Mjumbe wa Allaah, kwa nini umefanya
hivyo?” Akasema, “Jibriil alinambia, ‘amekula khasara yule ambaye
Ramadhaan imemfikia na akawa hakusamehewa dhambi zake, na nikasema ,
‘Aamiyn’. Baadaye akasema, ‘amekula khasara yule ambaye ameishi na hali
ya kuwa amewaona wazazi wake mpaka wakawa vizee, mmoja wao au wote
wawili, lakini ikawa hajaingia peponi,’ na nikasema, ‘Aamiyn’. Baadaye
akasema, ‘amekula khasara yule ambaye wakati unapotajwa ikawa yupo na
asikutakie Rehma juu yako,’ na nikasema, ‘Aamiyn’.”
Imepokelewa na Ibn Khuzaymah, 1888; at-Tirmidhiy, 3545; Ahmad, 7444; Ibn Hibbaan, 908. Angalia Sahiih al-Jaami’, 3501.
3
– Wafundishe (watoto) adabu nzuri na namna ya kula, kwa mfano kula kwa
kutumia mkono wa kulia na kunywa kwa kutumia mkono wa kulia na kuchukua
chakula kutoka mbele ya nafasi zao (wasichukue upande wa mwengine);
wakumbushe kwamba kufanya israfu katika chakula ni Haraamu na ni
madhara kwa mwili.
4 – Usiwaachie kutumia wakati mrefu katika kula futari ikafikia hadi wakakosa Swalah ya jamaa ya Maghribi.
5 – Wakumbushe kuhusu hali za masikini na mafaqiri ambao hawawezi kumudu hata tonge ya chakula angalau wakaondosha moto wa njaa yao;
Wakumbushe hali za wale wote ambao aidha huhama au hupigania Jihadi kwa
ajili ya kutaka ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika sehemu
zote.
6
– Mikusanyiko hii (ya mwezi wa Ramadhaan) inatoa nafasi nzuri ya
kuwajumuisha jamaa pamoja na kuthibitisha mshikamano wa koo. Mazoea
kama haya yapo katika baadhi ya nchi, na vile vile ni nafasi nzuri ya
kupatanisha na kutengeneza uhusiano uliovunjika baina ya jamaa.
7 – Inamsaidia mama (kupata nafasi nzuri ya) kutayarisha chakula, kusafisha na vilevile kukiweka chakula muweko unaostahiki.
8 –Wawahimize watoto kuswali Swalah ya Taarawiyh na kujiandaa kwa ajili ya hiyo Swalah kwa kutokula sana na kujiweka tayari kwa wakati ili kwenda msikitini.
9 – Kwa kuzingatia Daku, wazazi ni lazima wawafundishe watoto baraka za daku na kwamba daku humpa mtu nguvu ya kufunga.
10
– Waruhusu kuwa na wakati wa kutosha kabla ya Swalah ya Alfajir ili kwa
wale ambao hawakuswali Swalah ya Witri waweze kufanya hivyo kwenye
wakati ule, na vile vile kwa wale wanaochelewesha Swalah zao hadi
wakati wa mwisho wa usiku, waweze kusali na pia kila mmoja aweze kuomba
du’aa kwa Mwenyezi Mungu vyovyote vile mtu apendavyo.
11
– Pawepo mazingatio ya kwenda msikitini kwa ajili ya Swalah ya jamaa ya
Alfajir, kwa wale wanaowajibika kufanya hivyo. Tunaona watu wengine
ambao huamka katika mwisho wa usiku kwa ajili ya kula daku, huwa
wanarejea tena kulala na kupuuza (kupitwa) na Swalah ya Afajir.
12
– Ilikuwa ni kawaida ya Mtume (Rehma na Amani Zimshukie Juu Yake)
katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani kukesha usiku na kuwaamsha
watu wake. Hii inamaanisha kwamba familia ni lazima izingatie kufanya
jitihada kwenye wakati huu adhimu (wenye baraka) ili kufanya matendo
ambayo yanamridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), huenda mtu
Akatukuzwa na Kupandishwa daraja (za Amali zake njema). Kwa hivyo Mume
ni lazima awaamshe Mkewe na Watoto wake ili kuyafanya yale ambayo
yatawapelekea kuwa karibu na Mola Wetu (Subhaanahu wa Ta’ala).
13
– Hutokezeya wakati mwengine ikawa kuna watoto wadogo katika nyumba
ambao wanahitaji kupewa moyo ili waweze kufunga, kwa hivyo baba ni
lazima awahimize kuamka kwa ajili ya kula daku, na vile vile awape moyo
kwa kuwasifu na kuwatunukia pindi wakimaliza mwezi mzima au hata
wakifikisha nusu yake, na vinginevyo (robo ya mwezi au wiki moja).
Imesimuliwa
kwamba Ar-Rubayyi’ bint Mu’awwidh alisema: Ilikuwa asubuhi ya mwezi wa
‘Ashuraa’ Mtume (Rehma na Amani Zimshukie Juu Yake) alipeleka habari
kwenye vijiji vya Answaar akasema, “
Yeyote aliyeamka bila ya kufunga, basi na asile kwa muda wote
uliobakia kwa siku ile, na yeyote aliyeanza kufunga basi na aendelee na
Swawm yake.” Akasema (bibi huyu): Tulikuwa tukifunga na kuwafungisha
watoto wetu, [na tulikuwa tukiwachukua msikitini] na tukiwatengenezea
vitu vya kuchezea vya sufi , ili ikiwa mmoja wao atalilia chakula basi
humpa kile kitu cha kuchezea (ili kimliwaze) mpaka ufike wakati wa
kuftari.
Imepokelewa na al-Bukhaariy, 1859; Muslim, 1136 – Maneno ya kwenye mabano yamepokelewa na Muslim.
An–Nawawiy amesema:
Hadiyth
hii inaonyesha kwamba ni lazima tuwafunze watoto wetu juu ya kufanya
matendo ya ibada na tuwaendeleze ili wakulie nayo, ijapokuwa wao
hawahesabiwi (kwa ajili ya umri wao kuwa mdogo). Al-Qaadhi amesema:
Imesimuliwa kutokana na ‘Urwah kwamba pale wanapokuwa wao wanaweza
kufunga basi huwa ni lazima juu yao kufunga. Hili ni kosa ambalo halina
uthibitisho wa hadiyth sahihi, “Kalamu huondoshwa kutokana na (mambo) matatu: kutoka mtoto anapozaliwa mpaka afikiapo kuwa msichana/mvulana …….” Na Allaah ni Mjuzi Zaidi.
Sharh Muslim, 8/14
14
– Ikiwa inawezekana, baba na mama ni lazima wende na watoto wao kwenye
‘Umrah (Hijja ndogo) wakati wa Ramadhaan, na kufanya hivyo ni manufaa
juu yao na katika maisha ya baadae, kwa nafsi zao wenyewe wazazi na
familia yao pia. Ibada ya Umrah katika mwezi wa Ramadhaan ina ujira sawa
na Hijja. Ni bora kwenda kufanya ‘Umrah katika wakati wa mwanzo wa
mwezi wa Ramadhaan ili kuepuka misongamano ya watu.
15
– Mume asimbebeshe kazi nyingi kupita uwezo wake mkewe kwa kupika
vyakula vingi. Watu wengi huuchukulia mwezi wa Ramadhaan kuwa ni mwezi
wa kubuni vyakula na vinywaji (vya kila aina) na huwa wanazama zaidi
kwenye hayo. Hii inapunguza thamani ya uzuri wa mwezi huu na inakwenda
kinyume na madhumuni ya kufunga, ambapo ni kufikia Ucha Mungu (Taqwa).
16
– Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Qur-aan, kwa hivyo tunashauri kila
familia iwe inajikusanya pamoja kwa ajili ya kusoma Qur-aan. Baba
aifundishe familia yake namna ya kusoma na maana ya ayah za Qur-aan.
Katika mkusanyiko huo huo kuwe kunafundishwa (aidha kwa njia ya usomaji
wa vitabu juu ya) adabu za kufunga. Katika mwezi wa Ramadhaan Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala) Huwawezesha wengi katika wanavyuoni na watafutao
elimu kuandika vitabu ambavyo hutumika kwa ajili ya mihadhara na
kufundishia; vitabu hivyo hugaiwa katika sehemu thelathini ambapo kila
sehemu huwa na mada isomwayo kwa siku moja na huleta manufaa kwa kila
mtu.
17 – Ni lazima wahimizwe kuutumia wakati wao kuwapitia majirani na wenye shida (kuhitaji).
Imesimuliwa
kwamba Ibn ‘Abbaas Amesema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ( Rehma na
Amani Zimshukie Juu Yake) alikuwa ni Mkarimu sana kwa watu, na alikuwa
katika kiwango kikubwa zaidi cha ukarimu wakati wa mwezi wa Ramadhaan.
Wakati Malaika Jibriyl alipomjia. Alikuwa akimjia kila usiku akimzoeza
Qur-aan pamoja naye. Mjumbe wa Allaah (Rehma na Amani Zimshukie Juu
Yake) alikuwa Mkarimu sana kuliko hata mvumo wa upepo.
Imepokewa na al-Bukhaariy, 6; Muslim, 2308.
18
– Wazazi ni lazima wazikinge familia zao na watoto wao kutokana na
kukaa muda mrefu wakati wa usiku na kuupoteza muda katika matendo
yasiyokuwa na manufaa, vitu vya kumpumbaza mtu ni haramu? Waovu miongoni
mwa watu katika mwezi wa Ramadhaan huwa zaidi ni kishawishi kikubwa
katika kuchochea waliofunga ili wafanye vitendo vibaya na viovu, usiku
na mchana.
0 comments:
Post a Comment