Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
(( شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 184]
Kwa
hivyo basi ndugu Muislamu, jitahidi ufanye ibada hii adhimu usome na
kuhifadhi Qur-aan kwa wingi kabisa kwani thawabu na fadhila zake ni
nyingi na adhimu mno kama
tunavyozinukuu humu. Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza
kuisoma) japo mara moja Qur-aan nzima kabla ya mwezi wa Ramadhaan
kwisha.
Zifautazo Ni Fadhila Mbali mbali Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
(( الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلاَوَتِهِ أُوْلَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ))
((Wale tuliowapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao ndio kweli wanakiamini)) [Al-Baqarah:121]
KUFANYA BIASHARA NA ALLAAH YENYE FAIDA TELE NA ISIYOANGUKA
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
(( إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ )) (( لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ))
((Hakika
wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasimamisha Swalah, na
wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji
biashara isiyododa (isiyoanguka))) ((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa
ukamilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni
Mwenye kusamehe Mwenye shukrani)) [Faatwir: 29-30]
MTU BORA KABISA NI MWENYE KUJIFUNZA NA KUIFUNDISHA
عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ )) خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه)) صحيح البخاريِّ
Imetoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Mbora wenu
ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhariy]
THAWABU MARA MBILI KWA MWENYE KUISOMA KWA MASHAKA
(Mwenye ulimi mzito au tabu ya kufahamu kwa haraka, lakini inambidi Muislamu ajitahidi kujifunza kuisoma sawa sawa)
عن عائشة رضي الله عنها أنَّ النبي صلى الله عليه وسلّم قال الماهرُ بالقرآن مع السَّفرةِ الكرامِ البررة، والذي يقرأ القرآنَ ويتتعتعُ فيه وهو عليه شاقٌّ له أجرانِ)) البخاري ومسلم
Imetoka
kwa 'Aisha (Radhiya Allahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi
wa aalihi wa sallam) amesema, ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma
Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu wacha
Mungu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi
kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
WATU WA QUR-AAN NI WATU BORA KWA ALLAAH (SUBHAANAHU WA TA'ALA)
عَنْ
أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ: (( إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا
رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ: ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ
اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ)) أحمد و إبن ماجه
Imetoka
kwa Anas (RadhiyaAllaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) amesema ((Allaah Anao watu Wake wa karibu katika
watu)). Wakamuuliza, ewe Mjumbe wa Allaah, nani hao? Akasema: (( Hhao
ni watu walioiandama Qur-aan na ni watu waliokuwa bora kabisa wa
Allaah)) [Ahmad, na Ibn Maajah]
TOFAUTI YA ANAYEISOMA NA ASIYEISOMA QUR-AAN
عن أبي موسى الأشْعَريِّ رضي الله عنه أنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلّم قالَ ((مثلُ المؤمنِ الَّذِي يقرأ القرآنَ مَثَلُ الأتْرُجَّةِ ريحُها طيبٌ وطعمُها طيّبٌ، ومثَلُ المؤمِن الَّذِي لاَ يقرَأ القرآنَ كمثلِ التمرة لا ريحَ لها وطعمُها حلوٌ )) البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ariy (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah harufu yake nzuri na ladha yake nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
THAWABU KWA KILA HERUFI MOJA
عن عبدالله بن مسعودٍ رضي الله عنه أن النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قال: (( من قَرأ حرفاً من كتاب الله فَلَهُ به حَسَنَةٌ، والحسنَةُ بعشْر أمْثالها، لا أقُول الم حرفٌ ولكن ألفٌ حرفٌ ولاَمٌ حرفٌ وميمٌ حرفٌ)) رواه الترمذي.
Imetoka
kwa 'Abdullahi Bin Mas'uud (Radhiya Allahu 'anhu kwamba Mtume (Swalla
Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Atakayesoma herufi moja
katika kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah
moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi
moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi
moja)) At-Tirimidhiy
KIOMBEZI SIKU YA QIYAAMAH
عن أبي أمَامةَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قال: ((اقْرَؤوا القُرآنَ فإنه يأتي يومَ القيامةِ شفيعاً لأصحابهِ)) مسلم
Imetoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah ikimuombea mwenye kuisoma)) Muslim
QUR-AAN HUMNYANYUA MTU NA HUMDHALILISHA MWINGINE
قال عمر رضي الله عنه : أما إن نبيكم صلى الله عليه وسلم قد قال: (( إن الله يرفع بهذا الكتاب أقواماً ويضع به آخرين )) صحيح مسلم
Imetoka
kwa 'Umar (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema, Mtume wenu amesema
((Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa kitabu hiki (Qur-aan) na
Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki)) [Muslim]
QUR-AAN HUMPANDISHA MTU DARAJA YA PEPO
عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( يقال لصاحب القران اقرأ و ارتق ورتل كما كنت ترتل في الدنيا فإن منزلتك عند آخر آية تقرؤها )) . (صحيح الجامع
Imetoka
kwa 'Abdullah bin 'Umar (Radhiya Allahu 'anhuma) kwamba Mtume (Swalla
Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Huambiwa rafiki wa
Qur-aan (Aliyeiandama Qur-aan) soma na panda (juu katika daraja za Pepo)
na
uisome kwa 'Tartiyl' (utaratibu na utungo) kama ulivyokuwa ukiisoma
(kwa Tartiyl) ulipokuwa duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika
katika aya ya mwisho utakayoisoma)) [Sahiyh Al-Jaami'i]
MWENYE KUHIFADHI QUR-AAN HUTANGULIA KABURINI (KWA AJILI YA MWANGA ANAOJAALIWA NAO)
عن جابر رضي الله عنه كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يجمع بين الرجلين من قتلى أحد في ثوب واحد ثم يقول : أيهم أكثر أخذاً للقرآن ؟ فإذا أشير إلى أحدهما قدمه في اللحد . (صحيح البخاري)
Imetoka
kwa Jaabir (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba alikuwa Mtume (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwakusanya watu wawili waliokufa katika
vita vya Uhud katika nguo moja kisha anauliza, ((Nani katika hao mwenye
Qur-aan zaidi? Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza kaburini))
[Al-Bukhaariy]
KUTEREMKA MALAIKA KWA UTULIVU NA RAHMA KWA WANAOSOMA QUR-AAN
عن أبى هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال ((ما اجتمع قوم في بيت من بيوت الله يتلون كتاب الله ويتدارسونه فيما بينهم إلا نزلت عليهم السكينة وغشيتهم الرحمة وحفتهم الملائكة وذكرهم الله فيمن عنده)) . صحيح مسلم
Imetoka
kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Hawakusanyiki pamoja watu katika
miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma kitabu cha Allaah, na
wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na hufunikwa na rahma na Malaika huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya aliokuwa nao)) [Muslim]
KUHIFADHI NA KUJIFUNZA MAANA YAKE NI BORA KULIKO MAPAMBO YA DUNIA
عن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال: خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال((أيغدو أحدكم كل يوم إلى بطحان العقيق, فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم? فقلنا يا رسول الله نحب ذلك قال : أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيتعلم أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين, وثلاث خير له من ثلاث , وأربع خير له من أربع , ومن أعدادهن من الإبل)) رواه مسلم وغيره
Imetoka
kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema, Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia wakati tulikuwa
katika Suffah akauliza, kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda soko
la But-haan-Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili (wa thamani kabisa
wa kike) bila ya kutenda dhambi au kukata undugu? Tukajibu kwamba sote
tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema, basi aende mmoja wenu
msikitini akajifunze au asome aya mbili katika kitabu cha Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia (wa
thamani kabisa wa kike). Na aya tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na
aya nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa aya kwa
ngamia )) [Muslim]
MWENYE KUHIFADHI QUR-AAN HUVALISHWA TAJI SIKU YA QIYAAMAH
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((يجيء القرآن يوم القيامة فيقول: يا رب حله, فيلبس تاج الكرامة ثم يقول: يا رب زده, فيلبس حلة الكرامة, ثم يقول: يا رب ارض عنه فيرضى عنه فيقول: اقرأ وارق ويزاد بكل آية حسنة)) رواه الترمذي والحاكم وصححه الألباني
: kwa hisani ya alhidaaya
0 comments:
Post a Comment