Monday, September 5, 2016

'ARAFAH ITAKUWA JUMAPILI (11.09.2016) NA 'IYD AL-ADHW-HAA NI JUMATATU (12.09.2016M)




 Tunapenda kuwajulisha kuwa tarehe 1 Dhul-Hijjah itakuwa ni Jumamosi 03.09.2016.
Vilevile tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kufunga siku ya 'Arafah ambayo itakuwa siku ya Jumapili tarehe 9 Dhul-Hijjah 1437 H (11.09.2016 M) In Shaa Allaah. Fadhila yake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili; uliopita na unaofuatia.


Kadhalika, tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa (anayewakilisha mtu kumchinjia), kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele za mwili na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo: 
عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ ))  وفي رواية :  ((فَلا يَمَسَّ مِنْ شَعَرِهِ وَبَشَرِهِ شَيْئًا))
Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)) na katika riwaaya nyengine ya Muslim (1977); ((basi asitoe kitu katika nywele zake wala ngozi yake)) [Muslim]

Kadhalika tusisahau kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta  Takbiyrah inayotakiwa kusomwa kuanzia Alfajiri ya siku ya 'Arafah hadi mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake.
Inavyopasa kufanya Takbiyrah:
   اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ،  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd

Bonyeza upate takbiyrah kwa sauti:

Takbiyra Ya 'Iyd


Inapasa kuwakumbusha ndugu wengine mafunzo haya na kuwasisitiza ili kila mmoja apate thawabu za kufufua Sunnah hizi ambazo wengi wamegafilika nazo.
Thawabu hizo zitazidi kuongezeka kwa yule atakayeanza kumfundisha mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kufundishwa: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ .
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Atakayetenda kitendo kizuri (Sunnatun-Hasanah) katika Uislaam kisha nacho kikafuatwa kutendwa, ataandikiwa mfano wa ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao.”  [Muslim]

Mafunzo Mbalimbali Yanayohusiana Na 'Ibaadah Ya Hajj
Kwa Munaasabah wa ‘Ibaadah tukufu ya Hajj, Alhidaaya imewatayarishia mafundisho mbalimbali yenye manufaa kuhusiana na nguzo hiyo muhimu ya Uislamu ili Haaj (Hujaji) aweze kuijua na kuitekeleza ‘Ibaadah hiyo katika njia sahihi na safi kama ilivyotufikia kutoka kwa kipenzi chetu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Tunawaombea Mahujaji wote, Hajj yenye kutaqabaliwa na wawe ni wenye kufutiwa madhambi yao.
Vitabu Na Makala

Alhidaaya Katika Manaasik Za Hajj Na 'Umrah - Kitabu Kamili
Makala za Hajj
Fataawa Za Hajj Na 'Umrah
Maswali Na Majibu Ya Hajj

Mawaidha

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer