Sunday, November 6, 2016

WEWE PEKEE TUNAKUABUDU NA WEWE PEKEE TUNAKUOMBA MSAADA: 12 - WASIYLAH NA TAWASSUL.


إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu
Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada
12 - Wasiylah Na Tawassul

 Maana ya Wasiylah
 Kwanza:  Ni daraja au cheo cha juu kabisa atakachopewa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huko Jannah kutokana na Hadiyth:
    عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ (رضي الله عنه)  أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا, ثُمَّ سَلُوا اللَّهَ لِي الْوَسِيلَةَ فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ لاَ تَنْبَغِي إِلاَّ لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ فَمَنْ سَأَلَ لِي الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ))
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mnapomsikia Muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni kwani atakayeniswalia Swalaah moja, Allaah Atamswalia mara kumi, kisha niombeeni kwa Allaah Al-Wasiylah  kwani hiyo ni daraja au cheo ambacho mja mmoja pekee wa Allaah  atakayefikia, na nataraji niwe mimi, basi atakayeniombea Wasiylah atastahiki kupata Shafaa-‘ah (uombezi)) [Muslim]
Pili:  Ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwtwaa’ah na ‘ibaadah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake njia za kumkurubia; na fanyeni jihaad katika njia Yake ili mpate kufaulu. [Al-Maaidah: 35]
‘Ulamaa wamekubaliana kuhusu maana ya wasiylah kwamba ni kufuata maamrisho na kujiepusha na aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Aayah hiyo ya Al-Maaidah 35:
“Allaah Anawaamrisha waja Wake Waumini wamkhofu Yeye kwa taqwa ambayo inapotajwa na vitendo vya utiifu, inamaanisha kujiepusha na yaliyoharamishwa na kuacha yote yaliyokatazwa.
 Kisha Akasema:
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia

Sufyaan Ath-Thawriy amepokea kutoka kwa Twalhah, kutoka kwa ‘Atwaa, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba ni: njia za kujikurubisha. Na akasema hivyo Mujaahid na Abu Waail na Al-Hasan na Qataadah na ‘Abdullaah bin Kathiyr na As-Sudiy na Ibn Zayd na wengineo wamesema maana hiyo hiyo ya Al-Wasiylah.  Qataadah amesema kuwa Aayah inamaanisha:  Tafuteni njia za kujikurubisha Kwake na mtiini Yeye na tendeni 'amali za kumridhisha. Na Ibn Zayd akasoma:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾
Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako daima ni ya kutahadhariwa. [Al-Israa: 57]
 Na hivi ndivyo ambavyo wamesema hawa Maimaam, hakuna khitilafu baina ya Mufassiriyn (wafasiri wa Qur-aan).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
 Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema kuhusu maana ya:  
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia
“Na ombeni haja zenu kutoka kwa Allaah kwani Yeye Pekee Ambaye Anaweza kukupeni, na hii inabainisha kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ  
“Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnazua uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye[Al-‘Ankabuwt: 17]
 Na kauli Yake:
وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ  
Na muombeni Allaah fadhila Zake. [An-Nisaa: 32]

Na katika Hadiyth:
((وَإِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ))
((Unapoomba basi muombe Allaah))  [Ahmad, Swahiyh At-Tirmidhiy (2516)]
 Tawassul ni kuomba haja au du’aa kwa kutumia njia za kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na tawassul ziko aina mbili; zinazokubalika katika shariy’ah ambazo zinatokana na mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na zisizokubalika, ambazo ni zile zilizotoka nje ya mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na hivyo hugeuka kuwa ni tawassul za shirki au bid’ah.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blog - Designer