Monday, August 20, 2018

FADHILA ZA SIKU YA 'ARAFAH NA YAWMUN-NAHR (SIKU YA KUCHINJA)


‘Arafah ni jabali ambalo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama katikati ya bonde lake kuhutubia Maswahaba katika Hajjatul-widaa’i. (hajj ya kuaga), na hapo ndipo wanaposimama Mahujaji kutimiza fardhi ya Hajj. Kusimama hapo ndio nguzo mojawapo kuu ya Hajj. Bila ya kusimama ‘Arafah hijjah ya mtu itakuwa haikutimia kwa dalili ifuatayo:

عن عبد الرحمن بن يعمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((الْحَجُّ عَرَفَة، مَنْ جَاءَ قَبْلَ طُلُوعِ الْفَجْرِ مِنْ لَيْلَةِ جَمْعٍ فَقَدْ أَدْرَكَ الْحَجّ)) صحيح الجامع   
‘Abdur-Rahmaan bin Ya’mur (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Al-Hajj ni ‘Arafah, atakayekuja kabla kutoka Alfajiri usiku wa kujumuika atakuwa ameipata Hajj)) [Swahiyh Al-Jaami’].

 
Fadhila Za Siku ya ‘Arafah:

Thursday, August 24, 2017

HUKMU YA KUFUPISHA THANAA (KUMTUKUZA ALLAAH) NA KUMSWALIA MTUME (SWALLA ALLAAHU 'ALAYHI WA SALLAM) NA MAAMKIZI YA KIISLAM.

Image result for Hukmu Ya Kufupisha Thanaa (Kumtukuza Allaah) Na Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Na Maamkizi Ya Kiislam

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Haifai kabisa kufupisha thanaa kwa maana kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kuandika (s.w.t). Au kufupisha Jalla Jalaahu kwa kuandika (J.J). Vile vile haifai kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuandika (s.a.w) au (s).

Friday, April 7, 2017

JIFUNZE QURAN (SURAH AN-NAHL)

 (80) Na Allah amekujaalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda.

(81) Na Allah amekufanyieni vivuli katika vitu alivyo viumba, na amekufanyieni maskani milimani, na amekufanyieni nguo za kukingeni na joto, na nguo za kukingeni katika vita vyenu. Ndio hivyo anakutimizieni neema zake ili mpate kut'ii.

(82) Basi wakikengeuka lilio juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi.

(83) Wanazijua neema za Allah, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni makafiri.

(84) Na siku tutakapo wainua kutokana na kila umma shahidi, kisha hawataruhusiwa walio kufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi.

(85) Na walio dhulumu watakapo iona adhabu hawatapunguziwa hiyo adhabu, wala hawatapewa muhula.

(86) Na walio shirikisha watakapo waona hao walio washirikisha na Allah, watasema: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaabudu badala yako. Ndipo wale watakapo watupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo!

(87) Na siku hiyo watasalimu amri mbele ya Allah, na yatapotea waliyo kuwa wakiyazua.

Saturday, January 7, 2017

ADABU ZA NDOA KATIKA SUNNAH ILIYOTAKASIKA.

Darsa :01
( UTANGULIZI WA DARSA LETU )
Sifa zote zamstahiki Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Ambaye Amesema katika aayah iliyo wazi kwenye Kitabu Chake:
(( ﻭَﻣِﻦْ ﺁﻳَﺎﺗِﻪِ ﺃَﻥْ ﺧَﻠَﻖَ ﻟَﻜُﻢ ﻣِّﻦْ ﺃَﻧﻔُﺴِﻜُﻢْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟًﺎ ﻟِّﺘَﺴْﻜُﻨُﻮﺍ ﺇِﻟَﻴْﻬَﺎ ﻭَﺟَﻌَﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢ ﻣَّﻮَﺩَّﺓً ﻭَﺭَﺣْﻤَﺔً ﺇِﻥَّ ﻓِﻲ ﺫَﻟِﻚَ ﻟَﺂﻳَﺎﺕٍ ﻟِّﻘَﻮْﻡٍ ﻳَﺘَﻔَﻜَّﺮُﻭﻥَ ))
((Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri))
(Ar-Ruum 30: 21).
Na Swalah na Salaam zimwendee kipenzi Chake Muhammad ambaye amesema katika Hadiyth Swahiyh:
(( ﺗَﺰَﻭَّﺟُﻮﺍ ﺍﻟْﻮَﺩُﻭﺩَ ﺍﻟْﻮَﻟُﻮﺩَ ﻓَﺈِﻧﻲ ﻣُﻜَﺎﺛِﺮٌ ﺑِﻜُﻢُ ﺍﻷَﻧْﺒِﻴَﺎﺀَ ﻳَﻮْﻡَ ﺍﻟْﻘِﻴَﺎﻣَﺔِ ))
((Oeni wapenzi wazaao, kwani nitashindana na Mitume wengine kwa idadi ya wafuasi siku ya Qiyaamah)).
Ahmad na At-Twabaraaniy kwa
isnaad iliyo hasan, na Ibn Hibbaan amekiri kuwa ni Swahiyh kutoka kwa Anas.
BAADA YA UTANGULIZI HUU:
Katika Uislamu kuna desturi na taratibu ambazo zatakikana kufuatwa na za mtu anayeoa au anayetaka kufunga ndoa.
Waislamu wengi leo hata wale ambao wanajitahidi katika ibada mbali mbali, hawajui kabisa hizi desturi za Kiislamu.
Kwa hiyo, nimeamua kuandika makala hii ndefu yenye faida kwa kuelezea wazi mambo haya katika mnasaba wa harusi ya mtu ambaye ni kipenzi changu.
Natumai kuwa itamsaidia yeye na ndugu wengineo waumini katika kumfuata Bwana wa Mitume alivyotuamrisha kutokana na amri ya Mola Wa Ulimwengu.
Baada ya hapo nimetahadharisha kuhusu baadhi ya mas-ala muhimu kwa kila anayeoa, na ambayo yamekuwa ni mitihani kwa wake wengi.
Namuomba Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Ajaaliye kitabu hiki kiwe ni chenye manufaa na Ajaaliye kazi hii iwe ya ikhlaas yenye kumridhisha Yeye Pekee kwani Yeye Ndiye Mwema na Rahiym.
Ifahamike kwamba kuna desturi nyingi katika sherehe za ndoa, lakini yaliyonishughulisha zaidi katika uandishi huu wa haraka, ni yale mambo yaliyo Sahihi katika Sunnah za Mtume ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ Muhammad ambayo hayawezi kukanushwa kutokana na msimamo maalumu wa mfululizo wa usimulizi (sanad) ambao hauna shaka katika muundo wake na maana yake.
Hivyo yeyote atakayesoma na kufuata maelezo haya atakuwa katika msingi uliothibiti wa Dini yake na atakuwa katika hali ya matumaini ya uhalali wa vitendo vyake.
Namuomba Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Amkhitimishe kwa furaha na thawaab kwa kuanza maisha yake ya ndoa kwa kufuata Sunnah na Amjaaliye miongoni mwa waja Wake Aliyewaelezea katika kauli Yake:
(( ﻭَﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻳَﻘُﻮﻟُﻮﻥَ ﺭَﺑَّﻨَﺎ ﻫَﺐْ ﻟَﻨَﺎ ﻣِﻦْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟِﻨَﺎ ﻭَﺫُﺭِّﻳَّﺎﺗِﻨَﺎ ﻗُﺮَّﺓَ ﺃَﻋْﻴُﻦٍ ﻭَﺍﺟْﻌَﻠْﻨَﺎ ﻟِﻠْﻤُﺘَّﻘِﻴﻦَ ﺇِﻣَﺎﻣًﺎ ))
((Na wale wanaosema: Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho, na Utujaalie tuwe waongozi kwa wachaji Allaah))
(Al-Furqaan 25: 74)
Na mwisho mwema ni wa waja wanaomcha Allaah kama Anavyosema Mola wa Ulimwengu:
(( ﺇِﻥَّ ﺍﻟْﻤُﺘَّﻘِﻴﻦَ ﻓِﻲ ﻇِﻠَﺎﻝٍ ﻭَﻋُﻴُﻮﻥٍ ﴿ 41 ﴾ ﻭَﻓَﻮَﺍﻛِﻪَ ﻣِﻤَّﺎ ﻳَﺸْﺘَﻬُﻮﻥَ ﴿42 ﴾ ﻛُﻠُﻮﺍ ﻭَﺍﺷْﺮَﺑُﻮﺍ ﻫَﻨِﻴﺌًﺎ ﺑِﻤَﺎ ﻛُﻨﺘُﻢْ ﺗَﻌْﻤَﻠُﻮﻥَ ﴿43 ﴾ ﺇِﻧَّﺎ ﻛَﺬَﻟِﻚَ ﻧَﺠْﺰِﻱ ﺍﻟْﻤُﺤْﺴِﻨﻴﻦَ ))
((Hakika wachaji Allaah watakuwa katika vivuli na chemchem. Na matunda wanayoyapenda. Kuleni na
kunyweni kwa furaha kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. Hakika ndio kama hivyo Tunavyowalipa watendao mema))
(Al-Mursalaat 77: 41-44).
Adabu na desturi hizo ni darsa letu lajao In Shaa Allaah.
Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Wabillaahi Tawfiyq.

Wednesday, December 21, 2016

MWANAFUNZI WA KIKE WA KIISLAMU AGOMA KUMPA MKONO RAIS WA UJERUMANI.

Mwanafunzi wa kike wa kiislamu mwenye asili ya Syria wa shule ya Theodor Heuss nchini Ujerumani amekataa kusalimiana kwa kumpa Rais wa nchi hiyo pale alipozuru katika shule yao.



Tukio hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi uliopita pale Rais Joachim Gauck alipotembelea mji wa Offenbach na shule hiyo inayounganisha wahamiaji na jamii ya kijerumani.

Rais Joachim alitembelea shule ya Theodor Heuss kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuwasaidia na kusomesha watoto wa wahamiaji lugha ya kijerumani na tamaduni za nchi hiyo.


Kamera za TV zilichukua tukio hilo pale Rais alipoanza kuwasalimia wanafunzi waliojipanga kumpokea ndipo alipofika kwa binti huyo aliyevaa Baibui na hijabu. Jina la binti huyo halikuweza kupatikana mara moja.

Alipojaribu kutoa mkono kumsalimia, binti huyo hakutoa mkono wake bali aliweka mkono wake kifuani na kutingisha kichwa chake kama ishara ya kumsalimu rais huyo badala ya kumpa mkono.


Kimsingi binti huyo hakumvunjia heshima Rais wa Ujerumani bali alitekeleza mafundisho ya Kiislamu ambayo yanaharamisha mwanamke Mwislamu kumpa mkono mwanaume ajnabi kama ambavyo mwanaume Mwislamu haruhusiwi kumpa mkono mwanamke ajnabi.

Hali hiyo ikamfanya Rais kuendelea na mwanafunzi mwingine.

Katika mafundisho ya dini ya kiislamu hairuhusiwi kushikana

mkono mwanamke na mwanaume ambao hawajaoana.

Tukio hilo limeibua maoni ya watu wengi nchini Ujerumani ambapo Mwanasaikolojia Annette Trebel amezitaka mamlaka zinazohusika kujifunza tamaduni zingine kutoka kwa wahamiaji badala ya wahamiaji kujifunza tamaduni za kijerumani.

Aidha wengi walitoa wito kwa wajerumani kujifunza kiarabu ili kusaidia wahamiaji ambao hawataki kujifunza kijerumani. Pia kuweka ishara za lugha ya kiarabu ili kusaidia wahamiaji wanaowasili nchini humo.

Sunday, November 6, 2016

HADIYTH AL-QUDSIY HADIYTH YA 37: EE BIN AADAM! SITOJALI DHAMBI ZAKO MADAMU UTANIKARIBIA KUOMBA MAGHFIRAH.

Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 37
Ee Bin Aadam! Sitojali Dhambi Zako Madamu Utanikaribia Kuomba Maghfirah

عن أَنَس بْن مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))    
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]

WEWE PEKEE TUNAKUABUDU NA WEWE PEKEE TUNAKUOMBA MSAADA: 12 - WASIYLAH NA TAWASSUL.


إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu
Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada
12 - Wasiylah Na Tawassul

 Maana ya Wasiylah
 Kwanza:  Ni daraja au cheo cha juu kabisa atakachopewa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huko Jannah kutokana na Hadiyth:
    عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ (رضي الله عنه)  أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا, ثُمَّ سَلُوا اللَّهَ لِي الْوَسِيلَةَ فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ لاَ تَنْبَغِي إِلاَّ لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ فَمَنْ سَأَلَ لِي الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ))
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mnapomsikia Muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni kwani atakayeniswalia Swalaah moja, Allaah Atamswalia mara kumi, kisha niombeeni kwa Allaah Al-Wasiylah  kwani hiyo ni daraja au cheo ambacho mja mmoja pekee wa Allaah  atakayefikia, na nataraji niwe mimi, basi atakayeniombea Wasiylah atastahiki kupata Shafaa-‘ah (uombezi)) [Muslim]
Pili:  Ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwtwaa’ah na ‘ibaadah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake njia za kumkurubia; na fanyeni jihaad katika njia Yake ili mpate kufaulu. [Al-Maaidah: 35]
‘Ulamaa wamekubaliana kuhusu maana ya wasiylah kwamba ni kufuata maamrisho na kujiepusha na aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Aayah hiyo ya Al-Maaidah 35:
“Allaah Anawaamrisha waja Wake Waumini wamkhofu Yeye kwa taqwa ambayo inapotajwa na vitendo vya utiifu, inamaanisha kujiepusha na yaliyoharamishwa na kuacha yote yaliyokatazwa.
 Kisha Akasema:
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia

Sufyaan Ath-Thawriy amepokea kutoka kwa Twalhah, kutoka kwa ‘Atwaa, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba ni: njia za kujikurubisha. Na akasema hivyo Mujaahid na Abu Waail na Al-Hasan na Qataadah na ‘Abdullaah bin Kathiyr na As-Sudiy na Ibn Zayd na wengineo wamesema maana hiyo hiyo ya Al-Wasiylah.  Qataadah amesema kuwa Aayah inamaanisha:  Tafuteni njia za kujikurubisha Kwake na mtiini Yeye na tendeni 'amali za kumridhisha. Na Ibn Zayd akasoma:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾
Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako daima ni ya kutahadhariwa. [Al-Israa: 57]
 Na hivi ndivyo ambavyo wamesema hawa Maimaam, hakuna khitilafu baina ya Mufassiriyn (wafasiri wa Qur-aan).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
 Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema kuhusu maana ya:  
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia
“Na ombeni haja zenu kutoka kwa Allaah kwani Yeye Pekee Ambaye Anaweza kukupeni, na hii inabainisha kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ  
“Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnazua uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye[Al-‘Ankabuwt: 17]
 Na kauli Yake:
وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ  
Na muombeni Allaah fadhila Zake. [An-Nisaa: 32]

Na katika Hadiyth:
((وَإِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ))
((Unapoomba basi muombe Allaah))  [Ahmad, Swahiyh At-Tirmidhiy (2516)]
 Tawassul ni kuomba haja au du’aa kwa kutumia njia za kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na tawassul ziko aina mbili; zinazokubalika katika shariy’ah ambazo zinatokana na mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na zisizokubalika, ambazo ni zile zilizotoka nje ya mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na hivyo hugeuka kuwa ni tawassul za shirki au bid’ah.
Powered by Blog - Designer