Monday, July 15, 2013

ZINGATIA HAYA KATIKA MWEZI WA RAMADHANI UPATE FADHILA

Imewekwa na yusouf
-Anza kwa kuzingatia mwezi huu mtukufu uwe wa kujihesabu, kutenda amali nyingi na kujirekebisha hali yako na uhusiano wako na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) uwe bora zaidi:
- Kumbuka kwamba huu mwezi ni mgeni ambaye amekutembelea kisha ataondoka, hivyo mpokee mgeni wako na mkirimu kwa mazuri yote anayostahiki.
-Tahadhari na kutokufunga bila ya sababu au udhuru wowote, kwani kufanya hivyo, Swawm yako haitolipika hata ukifunga mwaka mzima.
-Swali kwa wakati wake, usiache Swalah ikakupita. Na jua kuwa ukiwa huswali Ramadhaan huna Swawm kwa mujibu wa fatw za Maulamaa wengi.

NINI WAJIBU NA KHERI YA FAMILIA KATIKA MWEZI WA RAMADHANI

Imeandaliwa na   Ummu 'Abdil-Wahhaab na kuwekwa na yusouf sanga
  
Shukrani zote ni za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
Ni katika baraka zake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa Muislamu Kumuwezesha kufunga mwezi wa Ramadhani na kuutumia wakati wake wa usiku kwa Swalah. Ni mwezi ambao ndani yake amali njema huzidishwa malipo  na watu hupandishwa daraja (vyeo). Ni wakati ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Huwaachia huru baadhi ya watu kutokana na Moto. Kwa hivyo Muislamu ni lazima ajitahidi sana kufanya mambo mema katika mwezi huu; ni lazima afanye hima katika kuutumia wakati wa uhai wake wenye ibada. Kuna watu wangapi ambao wamenyimika katika mwezi huu kutokana na maradhi, mauti au kukosa maelekezo mema.

Muislamu ni lazima ajitahidi sana (kufanya matendo mema) katika wakati wake wote ndani ya mwezi huu; anayo majukumu yasiyoweza kuepukika juu ya watoto wake, kuwalea  vizuri na kuwatunza vyema,  kuwahimiza kufanya kila aina ya vitendo vyema na kuwafanya waendelee kukuwa navyo – kwa sababu  mtoto hukulia katika mwenendo ambao wazazi wake wamemzoeza.

Thursday, July 11, 2013

Mwezi Wa Ramadhaan Imeteremshwa Qur-aan - Jichumie Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  
(( شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 184]
Kwa hivyo basi ndugu Muislamu, jitahidi ufanye ibada hii adhimu usome na kuhifadhi Qur-aan kwa wingi kabisa kwani thawabu na fadhila zake ni nyingi na adhimu mno kama tunavyozinukuu humu. Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) japo mara moja Qur-aan nzima kabla ya mwezi wa Ramadhaan kwisha.  
Zifautazo Ni Fadhila Mbali mbali Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)    
(( الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلاَوَتِهِ أُوْلَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ))
 ((Wale tuliowapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao ndio kweli wanakiamini)) [Al-Baqarah:121]
Powered by Blog - Designer