Sunday, November 6, 2016

HADIYTH AL-QUDSIY HADIYTH YA 37: EE BIN AADAM! SITOJALI DHAMBI ZAKO MADAMU UTANIKARIBIA KUOMBA MAGHFIRAH.

Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 37
Ee Bin Aadam! Sitojali Dhambi Zako Madamu Utanikaribia Kuomba Maghfirah

عن أَنَس بْن مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))    
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]

WEWE PEKEE TUNAKUABUDU NA WEWE PEKEE TUNAKUOMBA MSAADA: 12 - WASIYLAH NA TAWASSUL.


إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu
Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada
12 - Wasiylah Na Tawassul

 Maana ya Wasiylah
 Kwanza:  Ni daraja au cheo cha juu kabisa atakachopewa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huko Jannah kutokana na Hadiyth:
    عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ (رضي الله عنه)  أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا, ثُمَّ سَلُوا اللَّهَ لِي الْوَسِيلَةَ فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ لاَ تَنْبَغِي إِلاَّ لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ فَمَنْ سَأَلَ لِي الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ))
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mnapomsikia Muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni kwani atakayeniswalia Swalaah moja, Allaah Atamswalia mara kumi, kisha niombeeni kwa Allaah Al-Wasiylah  kwani hiyo ni daraja au cheo ambacho mja mmoja pekee wa Allaah  atakayefikia, na nataraji niwe mimi, basi atakayeniombea Wasiylah atastahiki kupata Shafaa-‘ah (uombezi)) [Muslim]
Pili:  Ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwtwaa’ah na ‘ibaadah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake njia za kumkurubia; na fanyeni jihaad katika njia Yake ili mpate kufaulu. [Al-Maaidah: 35]
‘Ulamaa wamekubaliana kuhusu maana ya wasiylah kwamba ni kufuata maamrisho na kujiepusha na aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Aayah hiyo ya Al-Maaidah 35:
“Allaah Anawaamrisha waja Wake Waumini wamkhofu Yeye kwa taqwa ambayo inapotajwa na vitendo vya utiifu, inamaanisha kujiepusha na yaliyoharamishwa na kuacha yote yaliyokatazwa.
 Kisha Akasema:
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia

Sufyaan Ath-Thawriy amepokea kutoka kwa Twalhah, kutoka kwa ‘Atwaa, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba ni: njia za kujikurubisha. Na akasema hivyo Mujaahid na Abu Waail na Al-Hasan na Qataadah na ‘Abdullaah bin Kathiyr na As-Sudiy na Ibn Zayd na wengineo wamesema maana hiyo hiyo ya Al-Wasiylah.  Qataadah amesema kuwa Aayah inamaanisha:  Tafuteni njia za kujikurubisha Kwake na mtiini Yeye na tendeni 'amali za kumridhisha. Na Ibn Zayd akasoma:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾
Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako daima ni ya kutahadhariwa. [Al-Israa: 57]
 Na hivi ndivyo ambavyo wamesema hawa Maimaam, hakuna khitilafu baina ya Mufassiriyn (wafasiri wa Qur-aan).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
 Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema kuhusu maana ya:  
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia
“Na ombeni haja zenu kutoka kwa Allaah kwani Yeye Pekee Ambaye Anaweza kukupeni, na hii inabainisha kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ  
“Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnazua uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye[Al-‘Ankabuwt: 17]
 Na kauli Yake:
وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ  
Na muombeni Allaah fadhila Zake. [An-Nisaa: 32]

Na katika Hadiyth:
((وَإِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ))
((Unapoomba basi muombe Allaah))  [Ahmad, Swahiyh At-Tirmidhiy (2516)]
 Tawassul ni kuomba haja au du’aa kwa kutumia njia za kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na tawassul ziko aina mbili; zinazokubalika katika shariy’ah ambazo zinatokana na mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na zisizokubalika, ambazo ni zile zilizotoka nje ya mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na hivyo hugeuka kuwa ni tawassul za shirki au bid’ah.

HUKMU YA KUMLAZIMISHA MSICHANA KUOLEWA.

====================
من فتاوى فضيلة الشيخ العلامة صالح الفوزان حفظه الله.
Kutoka katika fataawa za sheikh Mwanachuoni Swaaleh Alfauzaan-Allaah amuhifadhi.
📌 السؤال :
هل للأب إجبار ابنته على الزواج؟
*Suali:*
Je inajuzu kwa Baba kumlazimisha mtoto wake wakike kuolewa?
☑️ الجواب: لا يملك الإجبار في هذا وإنما يمتنع من أن يزوجها من لا يصلح، وأما مسألة الإجبار فلا يجوز، إلا ما ذكر من أن الأب له أن يجبر البكر.
*Jawabu
Hakuna anaemiliki kulazimisha katika hili bali baba atakiwa tu akatae kumuozesha (mwanawe) Mwanamume ambaye sio mwema,
Ama mas'ala ya kulazimishana hiyo haijuzu, isipokuwa yaliyo tajwa kwamba (kuna kauli isemayo kuwa) Baba nijuu yake kumlazimisha (binti yake) bikra (katika hilo).
ولكن الصحيح خلاف هذا، وأنه ليس للأب ولا لغيره أن يجبر موليته على الزواج بمن لا تريده،
*Lakini Kauli iliyo swahihi*
(Na haki)Nikinyume na maneno hayo, Na nikwamba *Haifai kwa Baba wala mwengine yoyote kumlazimisha anaemsimamia juu ya kuolewa nimtu ambaye (labda) mwenyewe hamtaki.*
ولكن يعرض عليه ويكرر عليه وينصحها في هذا إلى أن تقتنع، فلابد أن تستشار ولا بد أن يؤخذ رأيها في هذا؛ لأن النبي صلى الله عليه وسلم: أعطى من زُوِّجَتْهُ بغير رضاها حق الفسخ.
Lakini (inayo takikana) Anamletea jambo hilo na analikariri kwake yeye na (kama hataki) anampa nasaha juu ya hilo mpaka pale atakapo kinai, Nilazima amtake ushauri na nilazima achukuwe rai yake katika hilo , Kwasababu Mtume swala na salamu zimwendee :Alimpa mwenye kuozeshwa bila ya ridhaa yake hukmu ya kuaribika ndowa.
المصدر : المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان (5/244)
*Chimbuko:*
Almuntaqaa min fataawaa sheikh Alfauzaan(5/244).📚.

TAHIYYATUL MASJID NA SUNNATUL UDHUI


TAHIYYATUL MASJID

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Yeyote miongoni mwenu atakapoingia Msikitini, hapaswi kukaa mpaka aswali rakaa mbili.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Jaabir (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema: “Mtu mmoja aliingia Msikitini siku ya Ijumaa wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatoa khutba, akamuuliza: "Je, umeswali?"
Powered by Blog - Designer