Wednesday, December 21, 2016

MWANAFUNZI WA KIKE WA KIISLAMU AGOMA KUMPA MKONO RAIS WA UJERUMANI.

Mwanafunzi wa kike wa kiislamu mwenye asili ya Syria wa shule ya Theodor Heuss nchini Ujerumani amekataa kusalimiana kwa kumpa Rais wa nchi hiyo pale alipozuru katika shule yao.



Tukio hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi uliopita pale Rais Joachim Gauck alipotembelea mji wa Offenbach na shule hiyo inayounganisha wahamiaji na jamii ya kijerumani.

Rais Joachim alitembelea shule ya Theodor Heuss kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuwasaidia na kusomesha watoto wa wahamiaji lugha ya kijerumani na tamaduni za nchi hiyo.


Kamera za TV zilichukua tukio hilo pale Rais alipoanza kuwasalimia wanafunzi waliojipanga kumpokea ndipo alipofika kwa binti huyo aliyevaa Baibui na hijabu. Jina la binti huyo halikuweza kupatikana mara moja.

Alipojaribu kutoa mkono kumsalimia, binti huyo hakutoa mkono wake bali aliweka mkono wake kifuani na kutingisha kichwa chake kama ishara ya kumsalimu rais huyo badala ya kumpa mkono.


Kimsingi binti huyo hakumvunjia heshima Rais wa Ujerumani bali alitekeleza mafundisho ya Kiislamu ambayo yanaharamisha mwanamke Mwislamu kumpa mkono mwanaume ajnabi kama ambavyo mwanaume Mwislamu haruhusiwi kumpa mkono mwanamke ajnabi.

Hali hiyo ikamfanya Rais kuendelea na mwanafunzi mwingine.

Katika mafundisho ya dini ya kiislamu hairuhusiwi kushikana

mkono mwanamke na mwanaume ambao hawajaoana.

Tukio hilo limeibua maoni ya watu wengi nchini Ujerumani ambapo Mwanasaikolojia Annette Trebel amezitaka mamlaka zinazohusika kujifunza tamaduni zingine kutoka kwa wahamiaji badala ya wahamiaji kujifunza tamaduni za kijerumani.

Aidha wengi walitoa wito kwa wajerumani kujifunza kiarabu ili kusaidia wahamiaji ambao hawataki kujifunza kijerumani. Pia kuweka ishara za lugha ya kiarabu ili kusaidia wahamiaji wanaowasili nchini humo.

Sunday, November 6, 2016

HADIYTH AL-QUDSIY HADIYTH YA 37: EE BIN AADAM! SITOJALI DHAMBI ZAKO MADAMU UTANIKARIBIA KUOMBA MAGHFIRAH.

Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 37
Ee Bin Aadam! Sitojali Dhambi Zako Madamu Utanikaribia Kuomba Maghfirah

عن أَنَس بْن مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))    
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]

WEWE PEKEE TUNAKUABUDU NA WEWE PEKEE TUNAKUOMBA MSAADA: 12 - WASIYLAH NA TAWASSUL.


إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu
Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada
12 - Wasiylah Na Tawassul

 Maana ya Wasiylah
 Kwanza:  Ni daraja au cheo cha juu kabisa atakachopewa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huko Jannah kutokana na Hadiyth:
    عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ (رضي الله عنه)  أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا, ثُمَّ سَلُوا اللَّهَ لِي الْوَسِيلَةَ فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ لاَ تَنْبَغِي إِلاَّ لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ فَمَنْ سَأَلَ لِي الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ))
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mnapomsikia Muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni kwani atakayeniswalia Swalaah moja, Allaah Atamswalia mara kumi, kisha niombeeni kwa Allaah Al-Wasiylah  kwani hiyo ni daraja au cheo ambacho mja mmoja pekee wa Allaah  atakayefikia, na nataraji niwe mimi, basi atakayeniombea Wasiylah atastahiki kupata Shafaa-‘ah (uombezi)) [Muslim]
Pili:  Ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa twaa’ah na ‘ibaadah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake njia za kumkurubia; na fanyeni jihaad katika njia Yake ili mpate kufaulu. [Al-Maaidah: 35]
‘Ulamaa wamekubaliana kuhusu maana ya wasiylah kwamba ni kufuata maamrisho na kujiepusha na aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Aayah hiyo ya Al-Maaidah 35:
“Allaah Anawaamrisha waja Wake Waumini wamkhofu Yeye kwa taqwa ambayo inapotajwa na vitendo vya utiifu, inamaanisha kujiepusha na yaliyoharamishwa na kuacha yote yaliyokatazwa.
 Kisha Akasema:
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia

Sufyaan Ath-Thawriy amepokea kutoka kwa Twalhah, kutoka kwa ‘Atwaa, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba ni: njia za kujikurubisha. Na akasema hivyo Mujaahid na Abu Waail na Al-Hasan na Qataadah na ‘Abdullaah bin Kathiyr na As-Sudiy na Ibn Zayd na wengineo wamesema maana hiyo hiyo ya Al-Wasiylah.  Qataadah amesema kuwa Aayah inamaanisha:  Tafuteni njia za kujikurubisha Kwake na mtiini Yeye na tendeni 'amali za kumridhisha. Na Ibn Zayd akasoma:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾
Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako daima ni ya kutahadhariwa. [Al-Israa: 57]
 Na hivi ndivyo ambavyo wamesema hawa Maimaam, hakuna khitilafu baina ya Mufassiriyn (wafasiri wa Qur-aan).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
 Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema kuhusu maana ya:  
وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ
tafuteni njia za kumkurubia
“Na ombeni haja zenu kutoka kwa Allaah kwani Yeye Pekee Ambaye Anaweza kukupeni, na hii inabainisha kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ  
“Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnazua uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye[Al-‘Ankabuwt: 17]
 Na kauli Yake:
وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ  
Na muombeni Allaah fadhila Zake. [An-Nisaa: 32]

Na katika Hadiyth:
((وَإِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ))
((Unapoomba basi muombe Allaah))  [Ahmad, Swahiyh At-Tirmidhiy (2516)]
 Tawassul ni kuomba haja au du’aa kwa kutumia njia za kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na tawassul ziko aina mbili; zinazokubalika katika shariy’ah ambazo zinatokana na mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na zisizokubalika, ambazo ni zile zilizotoka nje ya mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na hivyo hugeuka kuwa ni tawassul za shirki au bid’ah.

HUKMU YA KUMLAZIMISHA MSICHANA KUOLEWA.

====================
من فتاوى فضيلة الشيخ العلامة صالح الفوزان حفظه الله.
Kutoka katika fataawa za sheikh Mwanachuoni Swaaleh Alfauzaan-Allaah amuhifadhi.
📌 السؤال :
هل للأب إجبار ابنته على الزواج؟
*Suali:*
Je inajuzu kwa Baba kumlazimisha mtoto wake wakike kuolewa?
☑️ الجواب: لا يملك الإجبار في هذا وإنما يمتنع من أن يزوجها من لا يصلح، وأما مسألة الإجبار فلا يجوز، إلا ما ذكر من أن الأب له أن يجبر البكر.
*Jawabu
Hakuna anaemiliki kulazimisha katika hili bali baba atakiwa tu akatae kumuozesha (mwanawe) Mwanamume ambaye sio mwema,
Ama mas'ala ya kulazimishana hiyo haijuzu, isipokuwa yaliyo tajwa kwamba (kuna kauli isemayo kuwa) Baba nijuu yake kumlazimisha (binti yake) bikra (katika hilo).
ولكن الصحيح خلاف هذا، وأنه ليس للأب ولا لغيره أن يجبر موليته على الزواج بمن لا تريده،
*Lakini Kauli iliyo swahihi*
(Na haki)Nikinyume na maneno hayo, Na nikwamba *Haifai kwa Baba wala mwengine yoyote kumlazimisha anaemsimamia juu ya kuolewa nimtu ambaye (labda) mwenyewe hamtaki.*
ولكن يعرض عليه ويكرر عليه وينصحها في هذا إلى أن تقتنع، فلابد أن تستشار ولا بد أن يؤخذ رأيها في هذا؛ لأن النبي صلى الله عليه وسلم: أعطى من زُوِّجَتْهُ بغير رضاها حق الفسخ.
Lakini (inayo takikana) Anamletea jambo hilo na analikariri kwake yeye na (kama hataki) anampa nasaha juu ya hilo mpaka pale atakapo kinai, Nilazima amtake ushauri na nilazima achukuwe rai yake katika hilo , Kwasababu Mtume swala na salamu zimwendee :Alimpa mwenye kuozeshwa bila ya ridhaa yake hukmu ya kuaribika ndowa.
المصدر : المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان (5/244)
*Chimbuko:*
Almuntaqaa min fataawaa sheikh Alfauzaan(5/244).📚.

TAHIYYATUL MASJID NA SUNNATUL UDHUI


TAHIYYATUL MASJID

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Yeyote miongoni mwenu atakapoingia Msikitini, hapaswi kukaa mpaka aswali rakaa mbili.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Jaabir (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema: “Mtu mmoja aliingia Msikitini siku ya Ijumaa wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatoa khutba, akamuuliza: "Je, umeswali?"

Monday, September 5, 2016

'ARAFAH ITAKUWA JUMAPILI (11.09.2016) NA 'IYD AL-ADHW-HAA NI JUMATATU (12.09.2016M)




 Tunapenda kuwajulisha kuwa tarehe 1 Dhul-Hijjah itakuwa ni Jumamosi 03.09.2016.
Vilevile tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kufunga siku ya 'Arafah ambayo itakuwa siku ya Jumapili tarehe 9 Dhul-Hijjah 1437 H (11.09.2016 M) In Shaa Allaah. Fadhila yake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili; uliopita na unaofuatia.

Thursday, August 25, 2016

SIKU KUMI BORA KABISA ZA ALLAAH - 01 - 10 DHUL-HIJJAH.

Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo vitendo vyake vyema huwa na thawabu nyingi sana. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa mbele ya Allaah ambazo 'amali yoyote inayotendwa humo ni yenye kupendwa mno na Allaah:            
عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ)) يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ قَالُوا:  يَا رَسُولَ اللَّهِ وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟  قَالَ: ((وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْ)) البخاري
Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Mjumbe wa Allaah amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy]


Zifuatazo ni fadhila kuu za masiku hayo kumi ya Dhul-Hijjah. Ee ndugu Muislamu! Utakapojipwekesha katika 'ibaadah na kutenda amali njema zenye ikhlaasw na zinazotokana na mafunzo Sahihi ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi bila shaka utajichumia thawabu maradufu na ambazo zitakuwa nzito In Shaa Allaah katika mizani yako.


Allaah Ameziapia Siku Kumi Hizi

Kwa jinsi zilivyokuwa na umuhimu mkubwa siku hizo kumi, hadi kwamba Allaah (Subhaanah wa Ta'alaa) Ameziapia katika Qur-aan Anaposema:

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ((وَالْفَجْرِ)) ((وَلَيَالٍ عَشْرٍ))

BisimiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym. ((Naapa kwa Alfajiri)) ((Na kwa masiku kumi)) [Al-Fajr: 1-2]

Wanachuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo ni Siku kumi za Dhul-Hijjah.


Siku Za Manufaa Na Kumkumbuka Allaah

Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’alaa) kwa kukumbuka Neema Zake zisizohesabika:

((لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ))

((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28]

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kasema: “Hizo ni siku kumi za Dhul-Hijjah”. Na Amesema: “Manufaa ya dunia hii na ya Aakhirah” . Manufaa ya Akhera yanajumuisha kupata Radhi za Allaah. Manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]


'Amali Zake Ni Bora Kuliko Kwenda Katika Jihaad Fiy SabiliLLaah

Kutokana na ilivyotajwa katika usimulizi wa Hadiyth ifuatayo, kwamba amali yoyote utendayo katika masiku kumi hayo, ni bora kuliko kwenda kupigana jihadi vitani. Ukizingatia kwenda kupigana Jihaad ni jambo zito mtu kuliitikia, kwani huko kuna mashaka mbali mbali, ikiwemo khofu ya kujeruhiwa na kupoteza viungo vya mwili, kufariki, kupoteza mali n.k. Ila hilo si zito kwa mwenye imani ya hali ya juu kabisa kutaka kuyakabili mashaka hayo na kutamani kufa shahidi. Kwa hiyo usidharau amali yoyote hata iwe ndogo vipi itekeleze kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) ni Al-Jawwaad (Mwingi Wa Ukarimu), Al-Kariym (Karimu), Al-Wahhaab (Mwingi Wa Kutunuka, Mpaji Wa Yote), Al-Majiyd (Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu).

عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:)) ما من أيام العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام)) - يعني أيام العشر-. قالوا: يا رسول الله، ولا الجهاد في سبيل الله ؟ قال: ((ولا الجهاد في سبيل الله، إلا رجل خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع من ذلك بشيء)) البخاري

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Mjumbe wa Allaah amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy]


'Ibaadah Zote Zimejumuika Katika Siku Hizi

'Ibaadah zote zimejumuika katika siku kumi hizi nazo ni Swalah, Swawm, Swadaqah, Hajj, wala hazijumuiki hizi wakati mwingine.


Vitendo Vyema Vya Kutenda Katika Siku Kumi Hizi

1- Kutekeleza Hajj na 'Umrah (kwa mwenye uwezo)

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال ((العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما. والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة)) أخرجه البخاري و مسلم

Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: (('Umrah hadi 'Umrah hufuta (madhambi) baina yake, na Hajjum-Mabruwr haina jazaa ila Pepo)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: "سئل رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي الأعمال أفضل؟ قال: ((إيمان بالله ورسـوله)). قيل: ثم مـاذا؟ قال: ((الجهاد في سبيل الله)) قيل: ثم ماذا؟ قال: ((حج مبـرور)) متفق علية

Imetoka kwa Abu Hurayrah(Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amali gani ni bora kabisa?" Kasema: ((Kumuamini Allaah na Mtume Wake)), Akaulizwa:"Kisha nini?" Kasema: ((Jihaad katika njia ya Allaah)). Akaulizwa: "Kisha nini?" Kasema: ((Hajj Mabruwr)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


2- Kuomba Tawbah ya kweli na kujiepusha na maasi

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):

(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))

((Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah tawbah iliyo ya kweli!)) [At-Tahriym: 8]

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametupa matumaini makubwa ya kufutiwa madhambi na makosa yetu katika usimulizi ufuatao:
     
عن أنس رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((قال الله: يا ابن آدم إنك ما دعوتني ورجوتني غفرت لك على ما كان منك ولا أبالي، يا ابن آدم لو بلغت ذنوبك عنان السماء، ثم استغفرتني غفرت لك ولا أبالي، يا ابن آدم إنك لو أتيتني بقراب الأرض خطايا، ثم لقيتني لا تشرك بي شيئاً لأتيتك بقرابها مغفرة)) أخرجه الترمذي وحسنه الألباني في الصحيحة

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Amesema: Ee Mwana Adam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakusamehe yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee Mwana Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfira, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee Mwana Aadam, Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na msamaha unaolingana nao)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]


3- Kumkumbuka sana Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa)

Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr (kusema: Subhaana Allaah, AlhamduliLlaah, Laa Ilaaha Illa Allaah, Allaahu Akbar)

عن ابْنِ عُمَرَ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: (( مَا مِنْ أَيَّامٍ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ وَلَا أَحَبُّ إِلَيْهِ مِنَ الْعَمَلِ فِيهِنَّ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ الْعَشْرِ فَأَكْثِرُوا فِيهِنَّ مِنَ التَّهْلِيلِ وَالتَّكْبِيرِ وَ التَّحْمِيدِ )) أخرجه أحمد

Imetoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna siku zilizokuwa tukufu kwa Allaah na zilizokuwa vitendo vyake vipenzi kabisa Kwake kama siku hizi, basi zidisheni Tahliyl na Takbiyr na Tahmiyd)) [Ahmad]

Inavyopasa kufanya Takbiyr:

الله أكبر. الله أكبر. لا إله إلا الله. والله أكبر. الله أكبر ولله الحمد

“Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Laa Ilaaha Illa Allaah Wa-Allaahu Akbar, Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd”

Takbiyr hii ni aina mbili:

Takbiyratul-Mutwlaq -  Za Nyakati Zote

Takbiyr wakati wote usiku au mchana tokea Magharibi unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah  na inaendelea mpaka siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah) inapoingia Magharibi.


Takbiyratul-Muqayyad -  Za Nyakati Maalumu

Takbiyr kuanzia Alfajiri ya siku ya 'Arafah mpaka inapoingia Magharibi ya siku ya mwisho ya Tashriyq.


4- Kufufua Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Wanaume wanatakiwa waseme kwa sauti ili kuwakumbusha wengine na kufufua Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wanawake waseme kimya kimya isipokuwa wakiwa na mahaarim wao. Kufufua Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  ni muhimu kwani bila ya kufanya hivyo tutakuwa kwanza tunakosa fadhila zake, pili zitapotea Sunnah za kipenzi chetu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Atakayemuongoza mwenzake kufanya jambo jema atapata thawabu sawa sawa na za yule atakayetenda hilo jambo jema)) [Muslim]

كان ابن عمر وأبو هريرة رضي الله عنهما يخرجان إلى السوق في أيام العشر يكبران، ويكبر الناس بتكبيرهما (البخاري)

Ibn 'Umar na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walikuwa wakienda sokoni katika siku kumi na kufanya Takbiyr kwa sauti na watu wakiwaigiza)) [Al-Bukhaariy]


5- Kufunga siku hizi khaswa siku ya 'Arafah

Kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili:

 عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Imetoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]

Swawm pia ni kuwekwa mbali na Moto.

عن أبي سعيد الخضري رضي الله عنه قال: قال عليه الصلاة والسلام ((من صام يوما في سبيل الله باعد الله وجهه عن النار سبعين خريفا) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abu Sa'iydil-Khudhwriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Mwenye kufunga siku kwa ajili ya Allaah, basi Allaah Atamuokoa uso wake kutokana na moto kwa umbali wa miaka sabini)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na Swawm piia ina thawabu maradufu.

قال صلى الله عليه وسلم: (( كل عمل ابن آدم له الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائة ضعف. يقول الله عز وجل: إلا الصيام فإنه لي وأنا أجزي به)) أخرجه البخاري ومسلم

Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Kila 'amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye nitakayemlipa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


6- Kuzidisha vitendo vyema mbali mbali

Mbali ya kutekeleza fardhi ya Swalah kwa kuswali kwa wakati wake, kuswali Sunnah zaidi, kusoma Qur-aan, Swadaqah, Du'aa, kutii wazazi na kuwafanyia wema, kuwasiliana na jamaa (kuunga undugu), kuwafanyia wema jirani, kuamrishana mema na kukatazana maovu, kufanyiana wema na ihsani na kadhalika.


7- Kuchinja baada ya Swalah ya 'Iyd

Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'alaa):
((فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ))

((Basi Swali kwa ajili ya Mola wako na uchinje)) [Al-Kawthar: 2]


Pia, usimulizi ufuatao tunapata maelezo ya aina ya mnyama wa kuchinja na uchinjaji wake. 

فعَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: (( ضَحَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ وَسَمَّى وَكَبَّرَ وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا )) متفق عليه

Imetokea kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alichinja kondoo wawili weupe* wenye pembe, amewachinja kwa mikono yake, akasema BismiLLaah na Allaahu Akbar na akaweka mguu wake upande wa nyuma yao". [Al-Bukhaariy na Muslim]

*Baadhi ya Wanachuoni wamesema kuwa ni weupe ulio na alama nyeusi, wengine wamesema uliochanganyika na wekundu.

Kitendo hiki cha kuchinja ni 'Ibaadah tukufu na ni Sunnah iliyosisitizwa hata wanachuoni wameona kuwa ni Waajib kwa kila aliyekuwa na uwezo wa kuchinja.


Yanayompasa kufanya mwenye kutaka kuchinja

Baada ya kutia niyyah ya kuchinja, asikate mtu nywele wala kucha mpaka amalize kuchinja kama tulivyoamrishwa katika Hadiyth ifuatayo:

عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (( إذا رأيتم هلال ذي الحجة وأراد أحدكـم أن يضحّي فليمسك عــن شعره وأظفاره))، وفي راوية ((فلا يأخذ من شعره ولا من أظفـاره حتى يضحّي)) مسلم

Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake).

Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja)) [Muslim na wengineo]

Hii ni fadhila na neema kwetu maana tunakuwa katika hali ya ‘Ihraam’ kama waliokuwa kwenye Hijjah. Ikiwa amesahau mtu, mfano akakata kucha basi aendelee tu na niyyah yake mpaka amalize kuchinja.


8- Kuhudhuria Swalah ya 'Iyd

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewahimiza mpaka wanawake walio katika hedhi na wazee waende kusikiliza khutbah ya Swalah. Wakati wa Swalah ukifika, wanawake hao wenye hedhi wajitenge kando hadi itakapomalizika Swalah na kisha wajiunge na wenzao kusikiliza khutbah.


Siku Ya ‘Arafah Ni Siku Ya Tisa Dhul-Hijjah

a) Madhambi ya miaka miwili hufutiwa atakayefunga

Siku hii tukufu ni siku iliyokamilika Dini yetu. Thawabu za kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili.

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Imetoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema kuhusu Swawm ya 'Arafah kuwa ((inafuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake)) [Muslim]


b) Siku ambayo huachiliwa watu wengi huru na moto

عن عائشة رضي الله عنها أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((ما من يوم أكثر من أن يعتق الله فيه عبداً من النار من يوم عرفة)) رواة مسلم

Imetoka kwa Mama wa Waumini, 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna siku Allaah Anayowaacha huru waja na moto kama siku ya ‘Arafah)) [Muslim]


c) Du'aa bora kabisa ni Du'aa katika siku ya 'Arafah

Vile vile inapasa kumtaja sana Allaah siku hii kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa:

((خير الدعاء دعاء يوم عرفة، وخير ما قلت أنا والنبيون من قبلي: لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير)) روى الترمذي

((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Mitume kabla yangu ni:

'Laa Ilaaha Illa Allaah Wah-dahu Laa Shariyka Lahu, Lahul-Mulku Wa-Lahul-hamdu Wa Huwa 'Alaa Kulli Shay-in Qadiyr’)) [At-Tirmidhiy]


Siku Ya Kuchinja Ni Siku Kuu Ya ‘Iyd

Kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((إن أعظم الأيام عند الله يوم النحر، ثم يوم الْقَرّ)) سنن أبي داود

((Siku iliyo tukufu kabisa kwa Allaah ni siku ya kuchinja, kisha siku ya kutulia)) (yaani siku ya kukaa Minaa) [Abu Daawuwd]


Siku Za Tashriyq

Ni siku ya kumi na moja na kumi na mbili na kumi na tatu ya Dhul-Hijjah yaani baada ya siku ya 'Iyd. Na siku hizi tatu zimeitwa siku za Tashriyq kwa sababu watu walikuwa wakikatakata nyama na kuzianika juani. Siku za kuanika (nyama) juani. Na pi siku hizi hujulikana kwa 'siku za Minaa'.


a) Kumkumbuka sana Allaah

Katika siku hizi inampasa Muislamu azidishe kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kama Anavyosema:

((وَاذْكُرُواْ اللّهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ))

((Na mtajeni Allaah katika zile siku zinazohisabiwa)) [Al-Baqarah: 203]

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kasema: Siku zinazohisabiwa ni siku za Tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na Siku zinazojulikana ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Al-Qurtwubiy: 3.3]


b) Haifai kufunga katika siku hizi

Haifai kufunga katika siku hizi hata kama mtu alikuwa na mazowea ya kufunga Sunnah za Jumatatu na Alkhamiys au Ayyaamul-Biydh kutokana na makatazo kama haya:

عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم بعث عبد الله بن حُذافة يطوف في منى: ((لا تصوموا هذه الأيام، فإنها أيام أكل وشرب، وذكر الله، عز وجل))

Imetoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma 'Abdullaah bin Hudhaafah azunguke Minaa na atangaze "Msifunge siku hizi, kwani hizi ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka Allaah Mwenye Nguvu Mtukufu' [At-Twabariy 4: 211]

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Atupe umri na afya na uwezo wa kuweza kufanya mengi ya kumridhisha katika siku hizi tukufu na siku zote nyingine ili tujipatie thawabu nyingi na Atujaaliye tuwe katika wale wanaosikiliza kauli na daima wakafuata zile zilizo njema. Aamiyin
Powered by Blog - Designer